2014 UWE NI MWAKA WA KUFANYA MAPINDUZI MAKUBWA KATIKA MAISHA YAKO KIUCHUMI.. | JIFUNZE UJASIRIAMALI

2014 UWE NI MWAKA WA KUFANYA MAPINDUZI MAKUBWA KATIKA MAISHA YAKO KIUCHUMI..







Hakuna njia nyingine ila ni kwa kupata maarifa sahihi juu ya pesa pekee, ndipo mtu unaweza akajinasua kutoka katika minyororo ya umasikini ambayo ndiyo chanzo kikubwa cha mateso mengi binadamu tunayokumbana nayo katika maisha ya kila siku.

MWAKA HUU MPYA wa 2014
 Blogu yenu ya "Jifunzeujasiriamali" itaendelea kuwaletea mambo mbalimbali yahusuyo ujasiriamali, biashara na uchumi; habari na makala za wafanyibiashara wadogowadogo na wakati. Makala na habari hizo zitakuwa katika mtindo wa kumtia moyo na kumuelimisha mjasiriamali na wale wote watakaotembelea blogu hii kwa lengo la kuwafanya wawe na maisha bora kiuchumi, kiafya na mwishowe waweze kuishi maisha marefu yenye furaha.

Ni wakati wa kufanya tathmini/kupima ni kwa kiasi gani umeweza kutimiza malengo uliyojiwekea mwaka uliopita, iwe ni katika maisha yako kwa ujumla au katika biashara yako. Je, Mpango wa biashara yako ulienda sawa na hali halisi? ni malengo yapi ulishindwa kuyatimiza?

Mpango wa biashara unatakiwa kufanyiwa marekebisho kadiri hali halisi inavyojitokeza, sasa hakikisha kama hukuwa umeandika mpango/mchanganuo kwa ajili ya biashara yako basi unafanya hivyo mwaka huu ili uweze kufanya biashara kwa uhakika zaidi na hivyo kuwa na uwezekano mkubwa zaidi wa kupata mafanikio, mpango wa biashara ni Dira ya kule uendako kibiashara.

Kila mtu anayeanzisha biashara au anayemiliki biashara tayari anao mpango wa biashara yake kichwani, kinachotakiwa tu hapa na kilichokuwa muhimu sana ni kuuweka mpango huo katika maandishi kwenye karatasi, kuna maswala kwa mfano yahusuyo fedha ambayo huhitaji utaalamu kidogo katika kuyapanga lakini wala hayawezi kumfanya mtu asiandike mchanganuo wa biashara yake, kinachotakiwa tu ni mtu ajue kujumlisha na kutoa, basi.

Maarifa hayo na mengine yote yanayohusu ujasiriamali na biashara mtu anaweza akayapata kupitia njia mbalimbali siku hizi, zikiwemo, semina, makongamano, mafunzo rasmi darasani, katika maonyesho mbalimbali ya wajasiriamali na biashara, kupitia vyombo vya habari kama mitandao ya kijamii, tovuti, radio, televisheni, majarida, magazeti, vitabu na hata siku hizi katika mitandao ya simu wameweka utaratibu mtu unaweza kujiunga wakawa wanakutumia dondoo mbalimbali zinazohusu biashara na ujasiriamali.

Kampuni ya "Self Help Books Publishers Limited" chini ya kampeni yake ya 'KUTOKOMEZAUMASIKINI' bado imejikita katika kuandaa mambo mbalimbali kama vile vitabu, mitandao ya kijamii na tovuti, katika kuhakikisha inatoa mchango wake katika kukidhi haja ya wajasiriamali hasa wale wadogo wasiokuwa na mitaji mikubwa katika kupata njia rahisi na za haraka za kuelekea kufanya biashara za uhakika na ambazo zina uwezo wa kukopesheka na taasisi kubwa kubwa za kifedha. 

Ikiwa wewe ni mmoja wapo wa wafanyabiashara ndogo na ungependa kupiga hatua za haraka basi nakushauri ujiunge bure na kampeni hizi kwa kusoma makala zetu katika blogu hii na tovuti ya jifunzeujasiriamali.com, vile vile, punde tu tutakuwa pia katika facebook, twitter naYou tube. Zipo pia na bidhaa kama vitabu lakini vya kununua na baadaye tutakuwa na DVD na CD vyote hivyo lengo lake kuu likiwa ni kumfanya mjasiriamali aweze kujikomboa katika lindi kubwa la umasikini wa kutisha ambalo limekuwa ni chanzo cha mahangaiko mengi na majanga ya kila aina.

Ndugu msomaji, katika kuondokana na umasikini, huwezi kufanya hivyo kwa kupata maarifa kutoka chanzo kimoja tu, nakushauri pia uweze kutafuta maarifa kutoka sehemu mbalimbali unazoona ni muafaka kwako, siku hizi kuna semina na makongamano mengi, kama yanafanyika karibu na ulipo, jaribu, huwezi kujua inaweza ikawa ndiyo tiketi yako ya kuondokana na umasikini. Soma pia vitabu na majarida kutoka kwa waandaaji mbalimbali, mfano ni vitabu kutoka 'self help books' na hata kwingineko pia.

0 Response to "2014 UWE NI MWAKA WA KUFANYA MAPINDUZI MAKUBWA KATIKA MAISHA YAKO KIUCHUMI.."

Post a Comment