UTAJIRI WA HARAKA NI HATARI KUSHINDA UMASIKINI (SABABU 30 ZA KUSHINDWA KUFANIKIWA) | JIFUNZE UJASIRIAMALI

UTAJIRI WA HARAKA NI HATARI KUSHINDA UMASIKINI (SABABU 30 ZA KUSHINDWA KUFANIKIWA)

fikiri utajirike


16. UANGALIFU ULIOPINDUKIA
Mtu Asiyechukua hatari kwa ujumla huchukua chochote kile kinachosalia baada ya wengine kumaliza kuchagua. Kuwa mwangalif kupita kiasi ni mbaya sawa tu na ilivyokuwa kutokuwa mwangalifu vya kutosha. Vyote ni kupindukia kiasi kusikokuwa salama. Maisha yenyewe yamejazwa kwa viasili vya bahati.

17. UCHAGUZI MBAYA WA MSHIRIKA KATIKA BIASHARA
Hii ni moja kati ya sababu kubwa zaidi ya kuanguka katika biashara. Katika kutafuta soko la bidhaa zako, unapaswa kuchukua tahadhari ya hali ya juu kuchagua mwajiri ambaye atakuwa mtu wa kukutia moyo, na ambaye ni mwerefu na aliyefanikiwa. Tuna iga mifano ya wale tunaoshirikiana nao zaidi kwa karibu. Chukua mfanyakazi yule aliye na sifa zinazostahili kuigwa.

18. USHIRIKINA NA CHUKI.
Ushirikina ni aina ya hofu, pia ni dalili ya ujinga. Watu wanaofanikiwa ni waungwana na hawaogopi chochote.


19. UCHAGUZI MBAYA WA KAZI.
Hakuna mtu anayeweza kufanikiwa katika kufuata fani asiyoipenda. Hatua muhimu zaidi katika kutafuta soko la huduma zako ni kuchagua kazi ambazo unaweza ukajizamisha mwenyewe kwa moyo wako wote.

20. KUTOKUELEKEZA NGUVU ZAKO ZOTE KATIKA LENGO MOJA.
Mtu anayejaribu kufanya kila kitu ni mara chache hufanikiwa kwenye chochote. Elekeza nguvu zako zote katika lengo moja kuu lililokuwa dhahiri.

21. TABIA YA KUTOKUJALI MATUMIZI
Wafujaji wa mali hawawezi kufanikiwa, kwa kiasi kikubwa kutokana na sabababu kwamba wanasimama kwenye hofu ya umasikini daima. Jenga tabia ya kuweka akiba kwa mpangilio  kwa kuweka kando asilimia fulani ya kipato chako. Fedha katika benki hukupa msingi salama wa ujasiri wakati unafanya mapatano kwa ajili ya mauzo ya huduma zako. Bila pesa ni lazima utachukua kile unachopewa na kufurahia kukipata.  

22. KUKOSA SHAUKU
Pasipo shauku mtu hawezi kushawishi zaidi, shauku huambukiza na mtu aliye nayo kwa kiasi kikubwa hukaribishwa katika kundi lolote lile la watu.

23. KUKOSA UVUMILIVU
Mtu aliye na akili iliyojifungia katika jambo lolote ni mara chache sana husonga mbele. Kutokuwa na uvumilivu maana yake ni kwamba mtu ameacha kujifunza maarifa. Aina haribifu zaidi za kukosa uvumilivu ni zile zinazohusiana na dini, kabila, na tofauti za mawazo ya kisiasa.

24. ULAFI
Aina haribifu zaidi ya ulafi inahusiana na kula, vinywaji vikali na shughuli za mapenzi. Kuendekeza kupita kiasi katika moja ya vitu hivi ni hatari kwa mafanikio.

25. KUKOSA USHIRIKIANO NA WENGINE
Watu wengi hupoteza nafasi zao na fursa zao kubwa maishani kutokana na kosa hili kuliko kutokana na sababu nyingine zote ukiziweka pamoja. Ni kosa ambalo hakuna kiongozi au mmiliki wa biashara aliyefunzwa vyema atakayelivumilia.

26. KUMILIKI UWEZO AMBAO MTU HAKUUPATA KUPITIA JUHUDI BINAFSI.
(Wavulana na mabinti wa familia zenye uwezo na wengine wanaorithi pesa ambazo hawakuzifanyia kazi) Uwezo katika mikono ya mtu ambaye hakuupata taratibu mara nyingi ni hatari kwa mafanikio. Utajiri wa haraka ni hatari zaidi kushinda umasikini.

27. KUDANGANYA KWA MAKUSUDI
Hakuna mbadala kwa uaminifu. Mtu anaweza kukosa uaminifu kwa muda kwa kusukumwa na mazingira ambayo hawezi kuyazuia pasipokuwa na madhara ya kudumu. Lakini hakuna matumaini kwa watu wasiokuwa na uaminifu kwa makusudi. Ipo siku matendo yao yatabainika na watalipa kwa kukosa heshima, na pengine hata kukosa uhuru.

28. UBINAFSI NA MAJIVUNO
Tabia hizi hutumika kama alama nyekundu inayowatahadharisha wengine kujiweka mbali. Ni hatari kwa mafanikio.

29. KUKISIA BADALA YA KUFIKIRI
Watu wengi hawajali kabisa au ni wavivu  kutafuta ukweli  ambao watautumia kufikiria kwa usahihi. Huamua kutenda kwa kutegemea maoni yaliyotokana na kubashiri au maamuzi ya ghafla.

30. UKOSEFU WA MTAJI
Hii ni sababu kubwa ya kuanguka miongoni mwa wale wanaoanza biashara kwa mara ya kwanza bila ya kuwa na mtaji wa ziada wa kutosha kukabiliana na athari za makosa yao na kuwawezesha kuendelea mbele mpaka wamejijengea jina.

 31. Chini yah ii, taja sababu yeyote ya kuanguka ambayo umewahi kukumbana nayo ambayo haijawekwa kwenye orodha iliyotajwa hivi punde.

Katika hizi sababu 30 za kuanguka, kunapatikana maelezo ya janga la maisha ambalo linaendana na karibu kila mtu anayejaribu na kufeli. Itakuwa jambo la maana ikiwa utamshawishi mtu mwingine anayekufahamu vizuri kuipitia orodha hii na wewe, na kusaidia kukutathmini kwa kutumia sababu 30 za kuanguka. Laweza kuwa ni jambo lenye faida zaidi kuliko kama utajaribu hili ukiwa mwenyewe. Watu wengi hawawezi kujiona wenyewe kama wengine wanavyowaona. Unaweza kuwa miongoni mwa wale wasioweza.

Usemi wa wahenga ni, “Jifahamu mwenyewe kwanza” Ikiwa unatafuta soko la bidhaa kwa mafanikio, ni lazima uzifahamu bidhaa hizo. Hali ni hivyo hivyo ilivyo katika kutafuta soko la huduma. Unapaswa kufahamu madhaifu yako yote kusudi uweze aidha kuyarekebisha au kuyaondoa kabisa . Unapaswa kujua nguvu zako kusudi uweze kuzitumia wakati unapouza huduma zako. Unaweza kujitambua mwenyewe tu kupiti tathmini sahihi.

Ujinga unaoambatana na ubinafsi ulionyeshwa na kijana mdogo aliyeomba kazi kwa meneja  wa kampuni inyofahamika vizuri. Alionyesha muonekano mzuri sana mpaka meneja akamuuliza ni mshahara kiasi gani aliokuwa akitegemea kupata. Alijibu kwamba hakua na kiwango maalumu akilini(kukosa lengo lililokuwa wazi) Kisha meneja alisema, “tutakulipa kile unachostahili baada ya kukujaribu kwa wiki moja” “Sitakubali” kijana alijibu “Kwasababu napata kiasi zaidi ya hicho kule nilikoajiriwa sasa”  

Kabla hata hujaanza maelewano kwa ajili ya marekebisho ya mshahara wako katika nafasi yako uliyonayo sasa, au kutafuta ajira mahali pengine, hakikisha thamani yako ni kubwa kushinda kile unachokipata sasa.

Kutaka pesa ni kitu kimoja – kila mtu hutaka zaidi – lakini ni kitu kingine tofauti kabisa kuwa na thamani zaidi. Thamani yako inabainishwa kwa kiasi kikubwa na uwezo wako wa kutoa huduma zenye manufaa au uwezo wako wa kuwashawishi wengine kutoa huduma kama hizo.



Ndugu msomaji wa tafsiri hii ya think & grow rich, tunaomba radhi kwani sehemu hii ya 4 ya sura ya 7 ilikuwa iwekwe siku ya Jumatatu, ratiba yetu ya kuweka tafsiri kila Jumatatu na Alhamisi sasa tumeanza kuiheshimu na ikiwezekana tutaongeza tena siku moja iwe mara 3 kwa juma kutokana na maombi ya wasomaji wengi waliotaka kusoma sura zote za kitabu kwa lugha ya Kiswahili, Usikose siku ya Alhamisi sehemu ya 5 ya sura hii.



 soma sura na sehemu za kitau chote hapa


Watu bado wanajiandikisha katika lile kundi la Whatsapp la semina za michanganuo ya miradi bunifu kwa mwaka wote wa 2018, nafasi zimebaki chache wahi, ni kwa ada ya sh elfu 10. tu unapewa na kitabu cha michanganuo free, pamoja na kupata access ya kuingia blogu maalumu ya semina bila gharama zozote za ziada. Whatsapp: 0765553030

0 Response to "UTAJIRI WA HARAKA NI HATARI KUSHINDA UMASIKINI (SABABU 30 ZA KUSHINDWA KUFANIKIWA)"

Post a Comment