KAMWE, KAMWE, USIKATE TAMAA(NEVER, NEVER GIVE UP) | JIFUNZE UJASIRIAMALI

KAMWE, KAMWE, USIKATE TAMAA(NEVER, NEVER GIVE UP)

Ndugu na msomaji wa blogu ya jifunzeujasiriamali, hayo siyo maneno yangu bali ni maneno ya Rais Mteule wa Marekani Bwana Donald  Trump na wala hajaanza kuyatamka leo, ni maneno anayopenda kuyataja karibu kipindi chote cha maisha yake.


Makala hii si ngeni niliwahi kuituma kwa wanachama wa blogu hii kupitia e-mail na ni kipindi kirefu sasa nadhani toka kumalizika tu kwa uchaguzi wa marekani, nilituma ijumaa ya Novemba 2016. Kilichonifanya kuvunja mwiko na kuirudia makala hii hapa(kwani nilishaahidi kutokuziweka humu makala maalumu za wale wanaojiunga na blogu hii kwa email) ni kuona makala hii hii ikikopiwa kwa sehemu kubwa kama ilivyo na baadhi ya ‘bloggers’ wengine, ambao nadhani pia watakuwa wamejiunga na blogu hii kwa e-mail. Hivyo ikapoteza ule 'uspesho' wake hata hivyo nashukuru kwani ni wanachama wangu walioanza kuisoma.
 
Katika moja ya vitabu vyake Trump alieleza namna alivyokumbana na vikwazo vya kila aina katika maisha yake na jinsi alivyotumia ubunifu, na uking’ang’anizi wake kuvigeuza vikwazo hivyo kuwa ushindi. Leo hii tena Trump anatudhihirishia tabia yake hii baada ya kushinda uraisi wa Marekani.


SOMA: Maajabu ya kufikiria mambo makubwa na ni kwanini ujiwekee malengo makubwa maishani.
 
Ukimfuatilia Trump japo kwa kweli huwezi ukakubaliana naye kwa asilimia kubwa yale anayoyaamini(Hata mimi binafsi kwa kweli hanivutii kwa baadhi ya misimamo yake)  lakini kuna kitu kikubwa cha kujifunza kutoka kwake kwamba “Lolote lile akili yako inaloweza kulifikiria basi na ujue jambo hilo unao uwezo wa kulitimiza licha ya vikwazo vingi unavyoweza kukutana navyo njiani”
 
Hata katika kipindi cha katikati cha kampeni akiwa ameelemewa kabisa na kambi ya mpinzani wake Hilary Clinton alikuwa haachi kutamka maneno ya kumtia nguvu yeye na wafuasi wake kama haya; “Tutashinda, tutaushitua Ulimwengu”. Sidhani kama kuna kitu Trump alicholenga kukipata maishani mwake akakikosa labda iwe ni kuishi milele pasipo kufa ndiko kutakakomshinda, kama ni pesa amezipata nyingi, na sasa ameweza kuishika nafasi ya kisiasa ya juu zaidi duniani.


SOMA: Kuna wakati mtangazania Donald Trump alizomewa kama chizi vile lakini katu hakukata tamaa.

Hakuna siri kubwa hapa zaidi ya ‘kuamini anaweza’ pamoja na ‘kutokukata tamaa’ Kama umesoma kitabu “Think & GrowRich” nadhani utafahamu vizuri sana mbinu aliyotumia Donald Trump kufika pale alipo sasa. Hata wewe na mimi tunaweza kufanya mambo makubwa hapa Duniani ikiwa tu tutajifunza mbinu hizi alizotumia Trump hata ikiwa hatukubaliani na mitazamo yake.
 
Mpendwa msomaji na mwanachama wa Blogu ya Jifunzeujasiriamali sasa utakua ukipokea mara kwa mara makala za kutia moyo ndani ya e-mail yako. Makala hizo ni maalumu tu kwa wanachama wala hazichapishwi katika blogu ya jifunzeujasiriamali.
 
Naomba pia kuchukua fursa hii kukujulisha kuwa tumeanzisha darasa maalumu la kujifunza Michanganuo ya Biashara kwa kina katika blogu nyingine iitwayo,’ MICHANGANUO YA BIASHARA’ Blogu hii au darasa ni kwa ajili tu ya wale wanaohitaji kujifunza namna ya kuandaa mpango wa biashara na kiingilio chake au ada ni shilingi elfu 10 ambazo mshiriki anapewa na kitabu cha Michanganuo ya biashara na Ujasiriamali bure. Kufahamu zaidi juu ya darasa hili bonyeza maandishi yafuatayo. 
(Tanzania Online School Of Business Planning(TOSOBP))

0 Response to "KAMWE, KAMWE, USIKATE TAMAA(NEVER, NEVER GIVE UP)"

Post a Comment