JINSI YA KUJENGA MFUMO WA BIASHARA NDOGO YA REJAREJA KUZUIA UDOKOZI + MFANO | JIFUNZE UJASIRIAMALI

JINSI YA KUJENGA MFUMO WA BIASHARA NDOGO YA REJAREJA KUZUIA UDOKOZI + MFANO

 

Mfumo wa biashara ni sawa na mifumo inayounda mashine au injini ya gari
Ni matumaini yangu unaendelea na shughuli zako vizuri na leo nimekuletea somo hili kwa ajili ya kujenga mifumo inayowezesha biashara zetu kufanya kazi mithili ya vile mashine au injini iliyotiwa oil vizuri na kufanyiwa service inavyofanya kazi kiulani. Karibu sana tusome pamoja mpaka mwisho!

Biashara za rejareja mfano maduka ya vyakula mitaani maarufu kama maduka ya kina Mangi, duka la Mpemba nk. ni moja ya biashara zilizo na faida nzuri sana lakini changamoto yake kubwa ni jinsi ya kudhibiti mapato yasiibiwe au kupotea hasa pale mmiliki anapoamua kumuajiri msaidizi.

Biashara za rejareja zipo za aina nyingi na siyo maduka ya vyakula tu, kuna maduka ya dawa ya rejareja, magenge, vioski na karibu biashara nyingine zote ndogondogo zipo katika kundi la biashara za rejareja ikiwemo hata kuuza ubuyu, karanga na maji ya “Kandoro” barabarani.

Watu wana mbinu nyingi za kudhibiti biashara zao za rejereja na kubwa zaidi ni ile ya Mmiliki mwenyewe kukomaa na biashara yake pasipo kumuajiri mtu yeyote. Mbinu hii inafanya kazi vizuri sana lakini ubaya wake tu ni kwamba mmiliki anageuka kuwa mtumwa wa biashara yake mwenyewe na anakuwa hana uwezo wa kuipanua biashara yake kwa kuongeza matawi. Humchukua muda mrefu kutajirika na ikitokea kwa bahati mbaya akapoteza maisha na biashara yake nayo inakuwa imekufa.

Suluhisho la tatizo hili ni kuwa na mifumo itakayohakikisha biashara inajiendesha bila ya vizuizi (smoothly) mithili ya vile uonavyo gari au mashine iliyotiwa oil.

Mfumo maana yake ni nini?

Wengi tunaposikia neno mfumo wa biashara, tunafikiria tu ni mifumo ile ya kidigitali ya mahesabu (Accounting Software), lakini siyo hiyo peke yake, ni zaidi ya hiyo. Unaweza ukatengeneza mfumo wowote wa kuleta ufanisi kwenye biashara yako hata kama hutumii kompyuta wala simu janja.

Mfumo ni mjumuisho wa taratibu, Vifaa, na Kanuni zinazosaidia kazi fulani kutimizwa kwa wepesi na ufanisi.

Kwa hiyo unapojiundia utaratibu wa kufanya jukumu fulani kila siku, utaratibu rahisi ambao haubadilishwi ovyo na unaoweza kufuatwa na mtu mwingine yeyote anapotaka kutimiza jukumu hilohilo na kupata matokeo sawa na yale unayopata wewe, basi huo unakuwa ni mfumo.

Unapojijengea mifumo mbalimbali katika biashara yako ndogo inarahisisha kazi ya udhibiti wa mapato yako. Katika biashara ndogo ya rejarea kuna shughuli nyingi unazoweza ukazijengea mifumo na kubwa zaidi ya zote ni ile ya usimamizi au udhibiti wa pesa/mapato, lakini pia kuna shughuli nyingine kama vile, Ununuzi wa bidhaa, Kupiga stoku ya bidhaa, Usimamizi wa biashara, Kuajiri wasaidizi nk.

Mfano na Jinsi ya kujenga Mfumo

Mbali na mifumo ya kiuhasibu ya kompyuta, unaweza pia kujijengea mifumo mingine ya kawaida kwa ajili ya kutimiza malengo mbalimbali ya biashara yako kwa kupitia hatua zifuatazo, Hatua hizi nimeorodhesha kwa kifupi sana, maelezo kwa kirefu yapo katika kitabu cha Mafanikio ya Duka la Rejareja ;    

1.  Weka lengo

2.  Yavunjevunje hayo malengo/ majukumu

3.  Fanya maboresho

4.  Majaribio na mafunzo

Mfano wa Mfumo katika Biashara ya Duka la rejareja

Hapa natumia mfumo unaorahisisha kazi ya Ununuzi wa bidhaa kutoka katika maduka ya jumla huku mmiliki au muuzaji akipata muda zaidi wa kuhudumia wateja dukani.

 

Lengo la mfumo:                                                               

Kuleta ufanisi katika kazi ununuaji wa bidhaa za dukani na kumpa muuzaji muda zaidi wa kuhudumia wateja

 

Shughuli:         

Kufuatilia na kununua bidhaa katika maduka ya jumla kwa ajili ya duka la rejareja

 

Vifaa:

Baiskeli, Pikipiki au kwa miguu

 

Watu:

Mfanyakazi mmoja

 

Mikakati:

              i)      Mfanyakazi kila siku asubuhi atapewa orodha ya bidhaa zinazohitajika kwenda kununua madukani pamoja nakiasi cha fedha

             ii)     Anaporudi ataonyesha Ankara zote zilizotolewa wakati akinunua bidhaa ili zioanishwe na kiasi cha fedha zilizotumika.

            iii)    Mwenye duka au muuzaji ni lazima awe na uelewa wa bei za bidhaa mbalimbali kutokana na uzoefu wa siku za nyuma

            iv)    Mfanyakazi atalipwa kulingana na makubaliano na mwenye duka.

Huo ni mfano mmojawapo wa mfumo na unaweza kujitengenezea mfumo wowote katika biashara yako utakaokusaidia kutimiza malengo mbalimbali.

Kitabu cha MAFANIKIO YA BIASHARA YA DUKA LA REJAREJA toleo la 2022 kimeboreshwa upya (Updated). Mambo mbalimbali yameongezwa na kubwa zaidi ni Mifumo ya Usimamizi wa Mapato yasipotee kiholela. Tumeongeza mfumo  wetu mpya mmoja mbali na ule wa 2 IN ONE STORE MANAGEMENT SYSTEM. Kumbuka mifumo hiyo tulioiasisi wenyewe na kuthibitisha ufanisi wake siyo ile ya kidigitali ingawa inaweza kutumiwa sambamba nayo.

Lakini pia Tumezungumzia kwa kina mifumo ya Kidigitali (Accounting Software), mifano na aina zinazotumiwa zaidi hapa Tanzania. Kwa upande wa kuthibiti mapato tumefafanua kwa uwazi zaidi Jinsi ya kupiga stoku na namna rahisi kabisa ya kubaini kisha kuzuia udokozi au upotevu wa mapato ya duka/biashara yako. Tumeongezea masomo kama vile, mbinu za kuongeza mapato ya duka na mengine mengi.

Jinsi unavyoweza kukipata kitabu hiki

1.  SOFTCOPY:  kwa njia ya email kwenye simu au kompyuta yako: Lipia shilingi elfu 5 kupitia namba, 0765553030 au 0712202244 nakutumia kitabu muda huohuo bila kuchelewa.

 

2.  HARDCOPY: Tunakuletea kitabu cha karatasi popote pale ulipo Dar es salaa kwa shilingi elfu 12. Mikoa mingine tunatuma kwa mabasi kwa shilingi elfu 22

 

HABARI NYINGINE NJEMA

OFFA YA KUFUNGA USAJILI WA WANAGROUP LA MICHANGANUO-ONLINE

Group  la watsap na na Channel ya Telegram ya Michanganuo-online kwa ajili ya masomo ya kila siku ya fedha na michanganuo litasitisha rasmi kupokea wanachama wapya ifikapo tarehe 15/2/2022. Kwa kipindi kilichobaki tunaendelea kupoea watu kwa kiingilio cha sh. elfu 15 na watapata OFFA ya vitu (15) ikiwamo Vitabu na michanganuo kama ifuatayo

 

                     1.     KITABU cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI –cha kiswahili

 

                     2.     KITABU: MIFEREJI 7 YA PESA NA SIRI MATAJIRI WASIYOPENDA KUITOA –cha kiswahili

 

                     3.     KITABU mashuhuri zaidi duniani, HOW TO WRITE A BUSINESS PLAN  ndio hutumika vyuo vikuu vingi duniani.-cha kiingereza

 

                     4.     Mchanganuo wa Biashara: Kiwanda kidogo cha kutengeneza WINE na JUISI ya ROSELA-kiswahili

 

                     5.     Mchanganuo wa biashara: Kiwanda kidogo cha kukoboa Mpunga (Kikundi cha Akina Mama) -kwakiswahili

 

                     6.     Mchanganuo kamili wa biashara ya usagishaji nafaka –(USADO Milling))-kwakiswahili

 

                     7.     Michanganuo 3 ya ufugaji wa kuku, kuku wa mayai, kuku wa nyama na kuku wakienyeji-yote kwa kiswahili

 

                     8.     Mchanganuo kamili wa kilimo cha tikitimaji (KIBADA WATERMELON)-kwa kiswahili

 

                     9.     Mchanganuo wa biashara ya mgahawa(JANE RESTAURANT) –kwa Kiswahili & kiingereza

 

                   10.   Mchanganuo kamili wa Biashara ya kiwanda cha tofali za sementi (KILUVYA Bricks)-kwa Kiswahili

 

                   11.   Mchanganuo kamili wa Biashara ya Chipsi (AMANI CHIPS CENTRE)-kwaKiswahili

 

                   12.   Vielezo vya michanganuo ya biashara vinayokuwezesha kuandika michanganuo kwa muda mfupi. -Kwa Kiswahili & kiingereza

 

                   13.   Vipengele  vya Mpango wowote ule wa Biashara kwa kiswahili na kwakiingereza. Hata ikiwa hujui kabisa kuandika busiMchanganuo  unaweza kuvifuatisha ukaandika.

 

                   14.   Somo maalumu la mzunguko wa fedha. -Kwa Kiswahili

 

                   15.   Kuunganishwa group na Channel ya Michanganuo-online mwaka mzima

 

Asante Sana

PETER TARIMO

0 Response to "JINSI YA KUJENGA MFUMO WA BIASHARA NDOGO YA REJAREJA KUZUIA UDOKOZI + MFANO"

Post a Comment