JE, UNAIJUA NJIA HII RAHISI ZAIDI YA KUANDIKA MCHANGANUO WA BIASHARA YAKO? | JIFUNZE UJASIRIAMALI

JE, UNAIJUA NJIA HII RAHISI ZAIDI YA KUANDIKA MCHANGANUO WA BIASHARA YAKO?

Wajasiriamali wakiuza matunda kiubunifu

Makala ya leo nitakushirikisha kile nilichoandika katika ufunguzi rasmi wa MICHANGANUO BUNIFU 10 YA BIASHARA ZINAZOONEKANA ZA KAWAIDA SANA LAKINI ZENYE FURSA KUBWA KUTOKANA NA UBUNIFU ULIOTUMIKA. Katika Group la Michanganuo-online nimeandika kama ifuatavyo;- 

Leo ndio tunaanza rasmi masomo yetu ya Michanganuo kwa mwaka huu ingawa tulishaanza pale Januari lakini kutokana na group kuwa halikuwa na watu wa kutosha tukasitisha kidogo.

January niliahidi tutajadili kwanza Michanganuo 10 ya biashara ndogondogo zenye ubunifu wa kipekee na tayari tulishaandika Mchanganuo mmoja wa biashara ya kuuza dagaa mchele na samaki wa maji chumvi. Siku ya leo tunakwenda kuona Mchanganuo wa biashara nyingine, nayo ni; BIASHARA YA KUUZA MATUNDA KWA UBUNIFU KUONGEZA FAIDA MARA DUFU.

Biashara hizi unaweza ukaziona kama ni za kawaida sana na zinafanyika na watu lukuki mitaani lakini sisi tumeamua kuzifanya tofauti kabisa kuongezea ubunifu utakaozifanya ziwe ni za kipekee na zinazomlipa zaidi yule anayeamua kuzifanya.

Kwa mtindo huo biashara hizi hizi ambazo watu wengi wamekuwa wakizifanya miaka nenda, miaka rudi kwa minajili ya kupata tu mlo wa kila siku sasa zitakwenda kuwa na uwezo wa kumfanya mjasiriamali mdogo asiyekuwa na mtaji aweze kupata mtaji haraka huku akiipanua biashara yake au kuanzisha biashara nyingine kubwa itakayomfanya hatimaye kupiga hatua kubwa kiuchumi.

Kwahiyo unaweza ukasema michanganuo hii ama course hizi ni kimbilio la mjasiriamali yeyote yule anayehangaika (kustruggle) kupata mtaji wa kufanya biashara kubwa.

Katika Michanganuo hii nitatumia mtindo maalumu uitwao , One Page Business Plan au kwa kiswahili Mchanganuo Mfupi wa Biashara. One page simaanishi ni lazima uwe ni wa ukurasa mmoja tu hapana, ingawa pia unaweza ukaufanya kuwa hivyo.

Hii ni aina ya mchanganuo mfupi, kidogo ungefanana na Muhtasari ule wa kawaida wa Mpango wa biashara unaokaa pale mwanzoni mwa kila mchanganuo wa biashara lakini huu unaweza kuwa mrefu hata zaidi ya page moja.

Nimeamua kutumia mtindo huu  katika michanganuo hii 10 kwakuwa ni rahisi mwanafunzi kuelewa misingi muhimu ya uandishi wa michanganuo ya biashara kutokana na sababu kwamba vipengele vinavyotumika huwa ni vilevile sawa na vinavyopatikana katika mchanganuo mrefu lakini maelezo yake huwa ni mafupi na unaandika zile pointi muhimu tu kwanza. Baadae unaweza “ukauextend” ukaongeza maelezo na mchanganuo huo ukawa mchanganuo kamili mrefu.

Mchanganuo mfupi wa Biashara unakidhi haja ileile ambayo mchanganuo mrefu wa biashara ungekidhi, kwa mfano  sehemu nyingi wanazoitisha mtu upeleka business plan kama mabenki na Taasisi nyingine za fedha , wasomaji wa michanganuo hiyo hupendelea zaidi kusoma  ufupisho wa mchanganuo unaopeleka ili kupata picha halisi ya biashara yako na ufupisho huo unafanana sana na aina hii ya mchanganuo  mfupi ninaouzungumzia.

Hata hivyo katika hili group letu tutaendelea kuwa na vipindi vya masomo ya jinsi ya kuandaa michanganuo ya kawaida mirefu ya biashara sawa na ile inayopatikana katika kitabu chetu cha Michanganuo ya Biashara na ujasiriamali.

Je, Kuna Tofauti gani kati ya Mchanganuo Mfupi  na Mchanganuo Mrefu?

·       Tofauti kubwa ni wingi au uchache wa maelezo tu lakini aina zote mbili ni kitu kilekile kimoja kwa maana ya maudhui kwani mchanganuo mfupi hugusa kila kipengele muhimu kinachopatikana katika mchanganuo mrefu.

·       Mchanganuo mfupi huchukua muda mchache zaidi kuandaa

·       Unaweza kubadili mchanganuo mfupi  kuwa mchanganuo mrefu au kinyume chake pia

 Faida za Mchanganuo mfupi;

·       Humwezesha mjasiriamali kupata picha  kamili/ ramani ya biashara yake kwa haraka

·       Humwezesha hadhira/msomaji wa mchanganuo wako kuifahamu biashara yako kwa urahisi.

·       Ni rahisi kuandaliwa hata na mtu ambaye hana uzoefu mkubwa wa kuandaa michanganuo mirefu ya kawaida

Kwanini huwa tunaandika Michanganuo ya Biashara?

·       Faida ya kwanza na kubwa zaidi ya kuandika Mpango/Mchanganuo wa Biashara ni ili uweze kutusaidia katika uendeshaji wa biashara zetu kwani mchanganuo wa biashara ni sawa na ramani/dira inayotuonyesha njia kule tuendako kibiashara.

·       Unapojifunza au kuandika Mpango wa biashara ni sawasawa tu na mtu anayejifunza biashara kwani mchanganuo hugusa kila kipengele kinachohusiana na biashara kuanzia bidhaa/Huduma mpaka maswala ya fedha na Usimamizi.

·       Umuhimu mwingine ni kama vile, kuombea fedha mabenki au taasisi za kifedha, kuvutia wabia, kwa ajili ya mafunzo nk.

Kwa maelezo hayo ndugu mdau wangu wa Michanganuo-online nikuombe tu kwamba usikose mfululizo wa masomo haya kila siku usiku kuanzia saa 2 mpaka saa 4. Pia tafadhali sana wajulishe na wale uwapendao juu ya darasa hili la kipekee kwa mwaka 2022.

Kiingilio hiki cha shilingi elfu 10 kwa mwaka mzima ukilinganisha na manufaa ya darasa hili vikiwemo vitabu na Michanganuo, hakika unaweza kudhania ni karibu kabisa na bure.

·       Je, ungependa kuufahamu ni ubunifu wa aina gani uliotumika kwenye biashara hii ya kuuza matunda?

·       Na je, ungependa kujifunza hatua kwa hatua jinsi mchanganuo wa biashara hii unavyoandikwa?

·       Na je, Ungependa kuuliza swali lolote kuhusiana na biashara hii au mchanganuo wa biashara kwa ujumla?

·       Na je, Ungependa kufahamu kwa kina hatua mbalimbali biashara inazopitia , siyo ya matunda tu bali hata na aina nyinginezo za biashara ili uweze kuandaa mpango wa biashara yeyote ile nyingine kwa wepesi?

Ikiwa majibu ni ndiyo basi huna haja ya kuchelewa, jiunge na MICHANGANUO-ONLINE MASTERMIND GROUP LEO Kwa kulipa kiingilio chako sh. Elfu 10 tu mwaka mzima. Namba zetu ni 0765553030 au 0712202244 Jina NI Peter Augustino Tarimo kisha tuma ujumbe wasap au sms usemao;

“NIUNGANISHE NA GROUP LA MASOMO 2022 PAMOJA NA OFFA YA KUFUNGA USAJILI”

Nimetoa offa mara nyingi siku zilizopita na wengi walizichangamkia, OFFA hii hapa chini itakuwa ndio ya mwisho kwa kipindi cha hivi karibuni kwani pia tunatarajia kufunga usajili rasmi wa Wanagroup ifikapo tarehe 15/3/2022 hivyo unaweza kuona jinsi ambavyo nafasi ya kujiunga na group letu hili inavyozidi kupungua.

Ningefurahi sana kuona pia unapata masomo yote mazuri ya kipekee ndani ya MICHANGANUO-ONLINE kama unavyopata masomo kupitia blogu yako hii.

NB: Ikiwa utahitaji offa hii peke yake, hupendi kujiunga na magroup basi nijulishe pia.

 

OFFA YA KUFUNGIA USAJILI WA WANAGROUP LA MICHANGANUO-ONLINE MPAKA- 15/2/2022

 

                             1.     KITABU cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI –cha kiswahili

        

                             2.     KITABU: MIFEREJI 7 YA PESA NA SIRI MATAJIRI WASIYOPENDA KUITOA –cha kiswahili

 

                             3.     KITABU mashuhuri zaidi duniani, HOW TO WRITE A BUSINESS PLAN  ndio hutumika vyuo vikuu vingi duniani.-cha kiingereza

 

                             4.     Mchanganuo wa Biashara: Kiwanda kidogo cha kutengeneza WINE na JUISI ya ROSELA-kiswahili

 

                             5.     Mchanganuo wa biashara: Kiwanda kidogo cha kukoboa Mpunga (Kikundi cha Akina Mama) -kwakiswahili

 

                             6.     Mchanganuo kamili wa biashara ya usagishaji nafaka –(USADO Milling))-kwakiswahili

 

                             7.     Michanganuo 3 ya ufugaji wa kuku, kuku wa mayai, kuku wa nyama na kuku wakienyeji-yote kwa kiswahili

 

                             8.     Mchanganuo kamili wa kilimo cha tikitimaji (KIBADA WATERMELON)-kwa kiswahili

 

                             9.     Mchanganuo wa biashara ya mgahawa(JANE RESTAURANT) –kwa Kiswahili & kiingereza

 

                           10.   Mchanganuo kamili wa Biashara ya kiwanda cha tofali za sementi (KILUVYA Bricks)-kwa Kiswahili

 

                           11.   Mchanganuo kamili wa Biashara ya Chipsi (AMANI CHIPS CENTRE)-kwaKiswahili

 

                           12.   Vielezo vya michanganuo ya biashara vinayokuwezesha kuandika michanganuo kwa muda mfupi. -Kwa Kiswahili & kiingereza

 

                           13.   Vipengele  vya Mpango wowote ule wa Biashara kwa kiswahili na kwakiingereza. Hata ikiwa hujui kabisa kuandika busiMchanganuo  unaweza kuvifuatisha ukaandika.

 

                           14.   Somo maalumu la mzunguko wa fedha. -Kwa Kiswahili

 

                           15.   Kuunganishwa group na Channel ya Michanganuo-online mwaka mzima

0 Response to "JE, UNAIJUA NJIA HII RAHISI ZAIDI YA KUANDIKA MCHANGANUO WA BIASHARA YAKO?"

Post a Comment