UKITAKA MAFANIKIO YA HARAKA MWAKA 2021 ACHANA NA MAMBO MENGI KOMAA NA SIRI HIZI (2) TU!

MWAKAMPYA 2021 MAFANIKIO HARAKA

Nimefanya uchunguzi wa kina kwa muda mrefu na kugundua kwamba malengo ya watu wengi hasahasa yale ya kibiashara huwa yanashindwa kutimizika haraka kutokana na vitu vikubwa viwili(siri kuu mbili( 2)) ingawa hata hivyo kuna sababu nyingine ndogondogo lakini hizo kubwa 2 mtu ukikomaa nazo kisawasawa utakuta vijisababu vingine vidogovidogo vinayeyuka vyenyewe.

Nyakati tunazoishi leo hii za kidigitali binadamu tumegubikwa mno na taarifa nyingi, karibu kila kitu mtu leo hii utakachohitaji kufahamu ni mwendo wa sekunde au dakika chache tu, tena kwa ncha ya vidole vyako unakuwa umeshakifahamu tofauti na vile ilivyokuwa hapo kale mpaka uende sijui, ma-library au kusoma malundo ya magazeti, vitabu na shajara za nakala ngumu.

Leo hii mtu hata utake kujua jinsi ya kuunda roketi sembuse sijui kupika maandazi, vitumbua, keki na mikate, ni suala tu la ‘ku-google’ mtandaoni na tayari unapata ujuzi uupendao. Huwezi kukuta mtu akilalamika tena ujuzi fulani ataupata wapi, ni bando lako tu la buku au buku mbili.

Kwa wingi na urahisi huo wa taarifa mtandaoni ingetegemewa kwamba, mtu kufanikiwa kibiashara au katika nyanja nyingine yeyote ile maishani nako pia kungelikuwa rahisi hivyohivyo lakini ukweli ni kinyume chake, na katu haijawahi kuwa rahisi hata siku moja kwa mtu kufanikiwa jambo kirahisirahisi pasi na kuweka juhudi, maarifa na muda wa kutosha.

Hebu niambie ni mara ngapi umekuwa ukisoma makala zangu hapa na zikakupa hamasa kubwa hata ukashawishika kuamini kabisa kwamba sasa utakwenda kufanikiwa malengo yako mara moja lakini baadae ukashangaa umeendelea kuwa vilevile ulivyokuwa awali? Umesoma vitabu vingi vya elimu ya pesa na mafanikio, umekuwa mfuasi wa makocha wengi wa nje na ndani ya nchi, ukasikiliza na kuona semina za motivational speakers wasio na idadi lakini hujaweza kuona mabadiliko yeyote yale kwenye maisha yako kichumi. Je, wajua ni sababu zipi hizo zinazokuzuia usifanikiwe kiasi kile unachohamasika?

Hebu jaribu kufikiria kama ungelichukua mafunzo uliyopata kutoka kwenye kitabu kimoja tu kizuri ulichowahi kusoma na ukaanza kuyafanyia kazi barabara kwa vitendo yale uliyojifunza humo bila ya kuchelewa wala kutaka kwanza ujifunze kitu kingine kikubwa ni nini kingelitokea? Vipi kama ungeliamua kufanyia kazi mawaidha ya mhamasishaji wako mmoja mzuri mpaka pale ambapo ungeona kwanza matokeo yake ndipo uhamie kwa mhamasishaji mwingine?   

Katika Ulimwengu huu wa kidijitali kitu kikubwa tunachokosa kukifanya ni UTEKELEZAJI na kutaka tu kila mara kusikia au kusoma tu kuhusiana na mikakati mipya tunayodhani pengine itakuwa bora kushinda ile iliyopita.

 

1. SIRI NAMBA MOJA

Kwahiyo siri ya kwanza niliyokuahidi pale mwanzoni kabisa mwa makala hii si nyingine bali ni; UTEKELEZAJI/ KUCHUKUA HATUA. Lenga kwenye kuchukua hatua za kivitendo kwa yale unayojifunza kwanza kabla ya kujifunza kitu kingine kipya, sisemi tusijifunze hapana, bali ukijifunza jambo kubwa linalohitaji ulitekeleze, usikubali libakie tu kichwani. 

Tunapoteza fursa nyingi kwa kutofanya maamuzi ya kutekeleza kwa vitendon yale tunayojifunza. Kila unachojifunza hakina maama yeyote ile kwako ikiwa hautakiweka katika vitendo haraka. Na siri moja kubwa ya kutekeleza vizuri kile ulichokipanga ni kufanya kidogokidogo, usitegemee kufanya kwa mkupuo ukitegemea matokea hapohapo(overnight success), hiyo haiwezekani, ni lazima itakuchukua muda fulani, huo ndio ukweli mchungu usiopingika.

Unaweza ukatatua tatizo lolote lile, au kuifikia ndoto yeyote uliyonayo maishani lakini kwanza unatakiwa kuchukua hatua na wala siyo kutia nia au matamanio tu peke yake. Katika utekelezaji huo itakubidi wakati mwingine uchukue maamuzi magumu na mazito kama vile kufanya kazi masaa mengi ikiwezekana hata kujinyima usingizi na vitu vingine mbalimbali unavyovipenda.

 

2. SIRI NAMBA MBILI

Ikiwa upo kwenye biashara muda mrefu (biashara yeyote ile) bila shaka utaelewa vizuri jambo ninaloenda kulielezea punde. Ni kitu ambacho hakuna biashara yeyote ile duniani inayoweza kuwepo bila hicho. Hii ndiyo rasilimali(asseti) kubwa mfanyabiashara au mjasiriamali yeyote yule anayoweza akajivunia. Mara utakapotambua umuhimu wake na kuitumia inavyotakiwa rasilimali hii ndipo utakapofurahia faida ya haraka na ya kushangaza katika soko dhidi ya washindani wako.

Bilionea wa kwanza kabisa Marekani Bwana Andrew Carnegie aliwahi kusema kwamba, unaweza ukamnyang’anya viwanda vyake vyote alivyokuwa navyo, nyumba zake zote, na hata kila kitu alichokuwa nacho lakini mwachie tu watu wake muhimu zaidi na kila kitu kitarudi tena upyandani ya muda mfupi tu. Carnegie alikuwa akimaanisha nini? Alimaanisha umchukulie kila kitu lakini umwachie WATEJA WAKE tu na utashangaa atakavyorudisha kila kitu ulichompora ndani ya muda mfupi sana. Wateja hapa namaanisha wale unaowauzia vitu lakini pia wale wanaofanya biashara na wewe kama wagavi, wafanyikazi nk.

Unataka pesa na pesa hutoka kwa watu, na ili watu wakubali kukupa pesa zao walizozipata kwa tabu inakubidi na wewe pia kwanza uwape kitu fulani, Je unawapa kitu gani? Siyo kuwapa tu kitu, wateja wana tabia moja ya ajabu zaidi, hata wajue utawapa kitu fulani kizuri vipi, lakini bado wanaweza wasikubali kununua, watataka kitu kingine cha ziada, watataka kukuzoea na pia kukuamini ndipo waweze kubadilishana pesa zao na kile ulichonacho wewe.

Sasa hili la pili ndio lenye shida, watu kukuzowea na kukuamini siyo jambo rahisirahisi, ni lazima ufanye jitihada za kutosha za kimasoko. Ninachotaka kukielezea hapa ni ile siri yangu ya pili na ambayo nadhani mpaka hapa umeshapata picha ni kitu gani, WATEJA. Siri ya pili ili mtu uweze kufanikiwa kwenye biashara kirahisi mwaka huu wa 2021 ni KUWAJALI WATEJA wako.

Inawezekana kabisa unacho kitu cha kuwapa wateja tena kizuri tu kushinda washindani wako lakini wateja hawajui, hapo kitu cha kwanza kufanya ni kutangaza ili wajue, na hata wakijua bado hawajakuzoea wala kukuamini. Sasa cha pili kufanya tena hapo ni kujenga jina(Branding). Ukishatengeneza brand yako tayari umefaulu na hapo sasa utaanza kuona mafanikio ya kweli kwenye biashara yako yakitiririka kama maji ya kijito.

Ili kujenga jina(brand) jitahidi sana kuwa karibu na wateja wako na kufanya mambo yatakayowafanya warudi tena na tena kununua kwenye biashara yako, na hii haijalishi ikiwa ni biashara ya aina gani unayoifanya.

Ukiona wateja wako ni wa mara moja tu na hamna njia wanaweza wakarudi tena basi ujue biashara yako hiyo ina kila dalili za upatu wa kitapeli (ponzy schemes), biashara ambazo hukazania tu kupata wateja wapya kwani wanajua fika mteja wakishamliza hamna namna ataweza kurudi tena, wateja wapya wakiisha au kupungua na biashara nayo imekufa. Tumeona mifano mingi hata hapa Tanzania kuna watu mpaka leo hii wanashinda huko mahakamani kwa kesi za uhujumu uchumi na utakatishaji fedha baada ya kuahidi watu kuvuna mapesa kirahisirahisi mithili ya karanga ilihali haiwezekani.


HITIMISHO

Mwaka huu wa 2021 mimi binafsi na timu nzima ya blog ya JIFUNZEUJASIRIAMALI tunakwenda kuelekeza nguvu zetu kubwa kwenye siri hizi mbili, yaani;

1.  UTEKELEZAJI KIVITENDO WA HARAKA WA MAMBO pamoja na

2.  KUMJALI MTEJA KWA KIWANGO CHA HALI YA JUU KABISA

Kwani tunaamini kuwa hivi ndiyo vitu muhimu zaidi kwenye kufanikiwa haraka kibiashara. Wewe je? Inawezekana kulingana na mazingira yako na wewe unazo Siri zako za mafanikio tofauti na hizi, ni vizuri pia lakini ikiwa utapendezwa na chaguo letu hili, basi nakukaribisha sana katika MASTERMIND GROUP LETU LA 2021, Group litakalokuwa pia na CHANNEL ya Telegram kwa ajili ya kudownload masomo, michanganuo, na vitabu mbalimbali bure.

Group pia litakuwa na masomo ya fedha kila siku pamoja na semina za mara kwa mara juu ya uandishi wa michanganuo ya biashara zinazolipa haraka.

Nafasi bado zipo ingawa si nyingi. Kiingilio kwa mwaka mzima ni shilingi elfu 10 (10,000/=) tu. Group likijaa hatutakuwa na magroup mawili kutokana na ugumu kiuendeshaji, hivyo ni vizuri kama unapenda kuwa nasi 2021 hii yote ukajiunga mapema.

Kujiunga lipia kiingilio kupitia moja ya namba zetu hapo chini, kisha tuma neno; “NIUNGE MASTERMINDGROUP 2021 WATSAP NA TELEGRAM”

 

WHATSAP: 0765553030

SMS:           0712202244

JINA:           Peter Augustino Tarimo


Asante sana na nakutakia Heri na Baraka tele kwa mwaka wote wa 2021, Amua hatma yako tengeneza mwaka uliokuwa bora zaidi kushindamingine yote!


0 Response to "UKITAKA MAFANIKIO YA HARAKA MWAKA 2021 ACHANA NA MAMBO MENGI KOMAA NA SIRI HIZI (2) TU!"

Post a Comment