JINSI 2020 UNAVYOWEZA KUGEUZA WAZO LAKO LA MUDA MREFU KUWA BIASHARA HALISI YENYE MAFANIKIO | JIFUNZE UJASIRIAMALI

JINSI 2020 UNAVYOWEZA KUGEUZA WAZO LAKO LA MUDA MREFU KUWA BIASHARA HALISI YENYE MAFANIKIO

MWANAMKE NA MAPINDUZI YA VIWANDA 2020
Yamkini kwa muda mrefu sasa umekuwa na wazo lako iwe ni biashara au jambo jingine lolote lile ambalo umetamani sana kulitimiza bila mafanikio na hujui uanzie wapi. Inaweza kuwa ni ndoto yako ya kupunguza uzito, azma yako ya kuanzisha kiwanda kidogo cha juisi ya matunda asilia, nia ya kuandika kitabu fulani juu ya mada unayoipenda, lengo lako na wewe kuwa na kwako/kumiliki kiwanja/nyumba au hata nia yako ya kumiliki biashara halisi yenye mafanikio.

Katika makala yangu ya leo hii pamoja na dondoo nyingine muhimu 4 nimekuandalia filosofia  yangu ambayo huwa naitumia wakati ninapotaka kukamilisha malengo yangu mbalimbali yakiwemo yale ya uandishi wa vitabu au projekti nyinginezo mbalimbali, na nafikiri phylosophy hiyo hutumiwa hata na watu wengine mbalimbali pia wanapotaka kuwa na kitu fulani au kutimiza  malengo yao, nayo ni hii namba 1 hapa chini;

1. KUJIWEKEA MALENGO
Kabla haujaanza mwaka wa 2020 unatakiwa kwanza uwe na picha halisi akilini ya kile kitu unachokitaka kwa mwaka huu(najua unataka vitu vingi lakini kuna kile muhimu zaidi kwako unachowaza kuwa nacho au kukifanya) Ukishakuwa na lengo sasa jiulize maswali yafuatayo;

·       Kwanini unakitaka  kitu hicho?
·       Ungetaka ukipate mpaka kufikia muda gani?

Kwa mujibu wa kitabu changu cha MIFEREJI 7 YA PESA itakuwa ni jambo gumu sana kufanikisha lengo lolote lile ikiwa kama hautaweza kabla kuliweka bayana lengo hilo liweze kupimika, kutekelezeka na kuwa na muda maalumu wa kulitekeleza. Kwa kimombo wanaita vitu hivi, Specific, Measurable, Attainable, Realistic and Time based(S.M.A.R.T)

Hebu tuchukulie kwa mfano unadaiwa deni la shilingi million 5 na umeweka lengo mwaka huu wa 2020 kulipunguza deni hilo au ikiwezekana kulifuta kabisa. Badala tu ya kusema utapunguza deni au ikiwezekana kulimaliza, sema utapunguza kiasi fulani mathalani, “nitapunguza milioni 2, 3 au zote 5”

Ikiwa labda umelenga mwaka wa 2020 ujiwekee pesa kwa ajili ya kujenga nyumba yako na wewe uwe na kwako kama wengine, panga kabisa kiasi kamili kinachotosha kujenge nyumba hiyo, ni lini utahitaji kiasi hicho na vilevile kitu cha muhimu sana ni lazima pia upange ni kiasi gani utakacholazimika kuweka akiba kidogokidogo kila siku/mwezi au mwaka ili kuweza kulifikia lengo lako hilo la kujenga kwa muda ulioupanga. Fikiria ni mabadiliko gani utakayoyafanya kwenye maisha yako  ya kila siku ili kuweza kutimiza lengo lako.

Hapa nitakupa mfano wangu mimi binafsi wakati ninapokuwa naandika vitabu vyangu . Nikishaweka lengo la kuandika kitabu fulani, huwa napanga kabisa kitabu hicho nikimalize kwa gani. Kisha kila siku najiwekea malengo madogomadogo kwa mfano ya kuandika kurasa mbili mbili  au aya kadhaa.

Kwahiyo hata ikiwa kitabu ni kikubwa kama kilivyo kile cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI zaidi ya kurasa 410, najikuta kwa kuandika kidogokidogo kila siku hatimaye namaliza kitabu kizima kwa urahisi kabisa. Kwahiyo Lengo na hata liwe kubwa kiasi gani au dogo ukifuatilia kanuni hii ni lazima tu ulitimize. Filosofia hii imenisaidia sana mimi  binafsi na ni matumaini yangu hata na wewe pia itakusaidia.

2. FANYA UFUATILIAJI
Ikiwa utapenda kufaulu kwenye jambo lolote lile maishani hususani malengo uliyojiwekea ni lazima ufanye ufuatiliaji wa kile ulicholenga. Hauwezi kujua unakoelekea ni wapi ikiwa hujui ulipo ni wapi. Ukishaweka malengo yako katika hatua ya kwanza, sasa fanya ufuatiliaji na upime ikiwa kama kweli yanaoana na vile vipengele vya S.M.A.R.T

Kama mfano lengo lako ni la kupunguza deni kama tulivyotangulia kusema pale mwanzoni, basi ni wakati wa kuhakikisha kama kweli unapunguza matumizi yako kwa kiasi ulichopanga, deni linapungua na mapato yako yanaongezeka kusudi uweze kupata pesa za ziada za kupunguza deni lenyewe. Hapa ni lazima utafute njia itakayokuwezesha kufanya huo ufuatiliaji mfano unaweza kutumia ‘app’ za kwenye simu, programu za kompyuta, credit card nk. Credit card husaidia ufuatiliaji kwani mwisho unaweza kucheki taarifa nzima ya mwezi mzima kiasi cha miamala uliyofanya bila kuandika-andika.

Lakini njia rahisi kabisa kuliko zote unayoweza kufanya ufuatiliaji ni ile ya jadi ya kuandika katika daftari la kawaida kwa kalamu, chora jedwali(spreadsheet) na ujaze taarifa zako kila siku, umetumia kiasi kadha wa kadha, umelipa hiki na kile nk. Ikiwa utazembea kuandika na kufanya ufuatiliaji hesabu zako zinaweza kukushangaza, hutajua umetumia kiasi gani wala upunguze wapi na kuongeza wapi. Kuandika vitu katika karatasi kuna maajabu mengi sana katika kutimiza malengo.

3. KUWEKA FEDHA AKIBA IWE NDIO KIPAUMBELE CHAKO CHA KWANZA
Kuweka pesa(Savings) ndiyo njia nyepesi zaidi ya kweli iliyojaribiwa na kuthibitika kote Ulimwenguni kwamba inaweza kutengeneza Utajiri. Wataalamu mbalimbali wanaweza kukushauri viwango tofautitofauti unavyopaswa mtu kujiwekea kama akiba, wengine watakuambia, “weka asilimia 10%” wengine asilimia 5%, asilimia 20% nk. Lakini ukweli ni kwamba kama unataka kweli kuwa huru kifedha haraka au kutimiza lengo lako la muda mrefu ‘faster’ basi  huna budi kujiwekea akiba ya pesa kiasi kingi kwa kadiri utakavyoweza wewe, hata kama utaweka asilimia 80% ya mapato yako na mambo yakaenda vizuri bila kuathiri maisha yako, wewe weka.

4. LIPA MADENI YAKO
Unapokuwa na deni hauna tofauti na mvuvi aliyetia nanga baharini wakati huohuo akitaka ashindane mbio za mashua majini. Nanga haitamuachia asogee mbele hata sentimita moja. Ni kama inakuvuta nyuma wakati wenzako wanakata maji. Tumia akiba yako kupunguza madeni hasa yale yaliyokuwa na riba kubwa zaidi kwanza.

5. WEKEZA PESA ZAKO

Sasa baada ya kulipa madeni yako yote, kile kiasi cha pesa ulichokuwa ukilipa madeni kiongezee kwenye biashara au vitegauchumi vyako vingine vyenye uwezo wa kuzalisha pesa zaidi ikiwa kama kweli upo ‘serious’ kuufikia uhuru wa kifedha. Vitegauchumi vizuri visivyokuwa na hatari kubwa ni ardhi na majengo kwani thamani yake huwa inaongezeka kadiri muda nao unavyozidi kusogea. Pia unaweza ukavitumia kama dhamana ukitaka kwenda kukopa kwenye taasisi za fedha au benki.

Mwisho wa makala hii, Asante sana


................................................................................................


Taarifa muhimu !
OFFA YA MWISHO KABISA KWA MWAKA 2019
(Haitakaa itokee tena offa kama hii!)

Katika vipindi tofauti mwaka 2019 tulikuwa tukitoa offa hii kubwa ya kujiunga na GROUP LA MICHANGANUO-ONLINE  na watu wengi sana waliweza kuichangamkia. Group la mwaka 2019 ndio tayari limefikia tamati mwezi huu wa Desemba na sasa tunaanza tena rasmi kusajili wanachama kwa ajili ya Group la mwaka 2020.

Asilimia 95% ya wanachama wa group linaloisha muda wake wote wameamua kujiunga tena na group la 2020, hii inamaanisha kwamba nafasi kwa wanachama wapya safari hii zitakuwa chache na pengine hata isifike Machi 2020 kabla hazijamalizika kabisa kwani kama kawaida sisi hatunaga utaratibu wa kuendesha magroup mawili kwa wakati mmoja. MICHANGANUO-ONLINE ni moja tu na litaendelea kuwa moja siku zote.

Kujiunga na group la 2020 kiingilio ni Sh. 10,000/=(Elfu 10 tu) na ada hii ni ya MWAKA MZIMA wa 2020, hakuna malipo ya ziada wala yaliyojificha nyuma ya pazia na utashiriki programu zetu zote za masomo, mijadala pamoja na semina mbalimbali za kuandaa Michanganuo bunifu ya viwanda, kumbuka kaulimbiu yetu kuu 2020 ni “THE TANZANIA INDUSTIAL REVOLUTION 2020”


OFFA YENYEWE NI HII HAPA
Unapojiunga kabla ya tarehe 15 January 2020 utapata Offa yetu kubwa ya Vitabu na Michanganuo mbalimbali ifuatayo. Offa hii ilitakiwa iwe imeshafungwa rasmi Desemba na Group la 2019 lakini kutokana na rai za wadau wengi hasa walio kwenye utaratibu wangu wa kutumiwa masomo kwa njia ya email, basi nimeona ni busara kuisogeza mbele kidogo ili wale kwa sababu mbalimbali hawakuweza kupata kiingilio basi wawe wamepata.

Baada ya hapo mtu atakayehitaji vitu vilivyoko ndani ya offa hii itabidi avinunue kimoja kimoja kwenye DUKA LETU HILI HAPA LA VITABU NA MICHANGANUO ambapo, badala ya sh. elfu kumi atalipa sh. elfu 10 kwa kila kimoja sawa na sh. elfu 95 ikiwa atapenda kupata vitu(items) zote 15.

OFFA ina vitu vifuatavyo;

1.  Kitabu cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI kwa lugha ya Kiswahili.

2.  Kitabu kipya (Saikolojia na Utambuzi wa hali ya juu Kifedha(Advanced Money Literacy & Psychology)

3.  Kitabu cha masomo ya Mzunguko chanya wa fedha 2018 part 1

4.  Kitabu cha Masomo yam ZUNGUKO chanya wa fedha 2018 part 2

5.  Kitabu cha jinsi ya kuandika michanganuo ya biashara hatua kwa hatua.

6.  Kitabu mashuhuri zaidi duniani, HOW TO WRITTE A BUSINESS PLAN kwa lugha ya kiingereza, ndio kinachotumika vyuo vikuu vingi duniani.

7.  SEMINA: Masomo 11 ya jinsi ya kuandika mpango wa biashara.

8.  Kifurushi maarufu cha michanganuo 3 ya ufugaji wa kuku(MKOMBOZI CHICKS PLAN 3PACKS)

9.  Mchanganuo wa biashara ya mgahawa(JANE RESTAURANT) kwa Kiswahili na kiigereza

10.      Mchanganuo wa biashara ya kilimo cha matikiti maji.
11.      Semina na Mchaganuo mzima wa Kiwanda cha tofali(KILUVYA QUALITY BRICKS)

12.      Vielezo(Templates) za michanganuo ya biashara inayokuwezesha kuandika michanganuo kwa muda mfupi.

13.      Mfumo mpya wa usimamizi wa duka la rejareja(2 IN ONE STORE MANAGEMENT SYSTEM) unaomwezesha mmiliki wa duka dogo la rejareja au la kati kuthibiti mapato yake pasipo msaidizi kudokoa hata senti 5

14.      Somo muhimu sana la mzunguko wa fedha.

15.      Ukurasa mmoja wa mchanganuo.


Ukijumlisha gharama ya vitu vyote katika offa jumla yake ni sh. 95,000/=. Kwa hiyo ukiwahi offa ni sawa na kusema umeokoa sh. elfu 85, (85,000/=) Mjasiriamali Unasubiri nini ? Tembelea hapa Duka letu la Vitabu & Michanganuo Mtandaoni la Self Help Books Tanzania (Smart Books Tz)  kujionea bei halisi ya vitu vilivyoko kwenye offa hii ya kutupa!

0 Response to "JINSI 2020 UNAVYOWEZA KUGEUZA WAZO LAKO LA MUDA MREFU KUWA BIASHARA HALISI YENYE MAFANIKIO"

Post a Comment