MCHANGANUO WA BIASHARA YA KILIMO CHA MATIKITI MAJI KIBADA KIGAMBONI | JIFUNZE UJASIRIAMALI

MCHANGANUO WA BIASHARA YA KILIMO CHA MATIKITI MAJI KIBADA KIGAMBONI


KILIMO BORA CHA TIKITI MAJI
Semina yetu ya kuandika michanganuo ya biashara zilizo na fursa kubwa ya kutengeneza faida inaendelea ndani ya Group la Whatsap la MICHANGANUO-ONLINE. Mchanganuo tunaoandika leo unahusu Biashara ya kilimo cha matikiti maji katika eneo la Kibada Kigamboni jijini Dar es salaa. Ni mchanganuo wa 3 kati ya 12 tutakayochanganuo katika kipindi cha miezi 6 ijayo. Semina imeanza leo tarehe 9/8/2018 na itamalizika rasmi siku ya tatu hapo tarehe 11 siku ya Jumamosi.



MAELEZO YA BIASHARA.
Kibada watermelon Fruits ni shamba jipya la heka 2 lililoanzishwa kwa lengo la kuzalisha na kuuza matunda ya tikiti maji yenye ubora wa hali ya juu katika jiji la Dar es salaam. Matikiti maji yetu yatakuwa na ukubwa utakaomvutia mteja kutokana na utunzaji makini na uwekaji wa virutubisho vya kutosha katika mimea ya matikiti maji.

Kampuni itakuwa na makao yake eneo la Kibada Kigamboni na itasajiliwa rasmi kwa msajili wa Makampuni ili kuweza kukidhi vigezo vya kufanya biashara na kila mtu yakiwemo makampuni yanayomiliki mahoteli pamoja na supermarkets.

Dhamira kuu.
Dhamira yetu ni kuzalisha matikiti maji makubwa yaliyo na ubora wa hali ya juu yatakayomvutia kila mteja kwa kutumia njia za kisasa kabisa za kilimo cha matikiti maji.

Dira
Dira yetu ni kuwa kampuni kubwa kabisa itakayouza matikiti maji yaliyo na ubora wa hali ya juu katika ukanda mzima wa Pwani ya Afrika Mashariki.

Malengo.
·       Kulima heka moja kwa kila mzunguko mmoja itakayotoa matikiti maji yapatayo 5500
·       Kupata faida ya shilingi milioni 11 kwa mwaka
·       Kulima matikiti maji mizunguko 3 ya siku 90 kwa mwaka.
·       Kulima matunda na mbogamboga za aina nyingine siku za baadae katika maeneo ya mashamba tunayoyapumzisha katika mzunguko wa matikiti maji.

Siri za mafanikio
·       Kutumia mbolea ya samadi sambamba na zile za viwandani kwa kiasi cha kutosha kuhakikisha matunda makubwa na yaliyo na ubora wa hali ya juu.
·       Kuwapelekea matikiti maji wateja hasa hoteli kubwa na supermarkets mpaka mlangoni.
·       Kuhakikisha soko la uhakika lipo pindi tu matikiti maji yanapoanza kutoa maua.


Umiliki wa biashara........

...................................................................................


Kujiunga na Group hili kwa ajili ya semina zote zitakazofuata na zile zilizokwishafanyika pamoja na masomo ya kila siku jiunge na group hili kwa kutoa kiingilio shilingi elfu 10 kupitia namba zetu za simu, 0712202244  au  0765553030 jina ni Peter Augustino Tarimo. Baada ya malipo tuma namba unayotumia wasap na anuani yako ya email kisha ujumbe unaosema, “NIUNGANISHE NA GROUP LA MICHANGANUO”

0 Response to "MCHANGANUO WA BIASHARA YA KILIMO CHA MATIKITI MAJI KIBADA KIGAMBONI"

Post a Comment