UHURU KIFEDHA, UTAJIRI, BIASHARA NA AJIRA NZURI VIPO KWA YULE ANAYEPANGA NA KUVIDAI


FIKIRI UTAJIRIKE SURA YA 8V
Kupitia filosofia hii utapatikana ushauri kwamba wazo likisaidiwa na shauku kubwa lina tabia ya kujigeuza lenyewe kuwa katika kitu chake halisi. Kabla ya kumalizia ningetamani kukuachia mapendekezo kwamba mtu anaweza akakuta kwenye simulizi hii, na katika simulizi ya kuundwa kwa Shirika la chuma cha pua la Marekani(United States Steel Corporation), maelezo kamili ya njia ambayo wazo hufanya badiliko la kushangaza.

Katika utafiti wako wa siri ya njia hii, usitegemee muujiza kwa sababu hautaupata. Utapata tu sheria za milele za Asili. Sheria hizi zipo kwa kila mtu mwenye Imani na Ujasiri wa kuitumia. Zinaweza kutumika kuleta uhuru kwa Taifa au kuleta utajiri. Hakuna gharama kuokoa muda unaohitajika kuzielewa na kuzishika.

Wale wanaofikia maamuzi mara moja na kufahamu wazi ni nini wanachotaka, na kwa ujumla hukipata. Viongozi katika kila nyanja ya kimaisha huamua haraka na kwa uthabiti. Hiyo ndiyo sababu kubwa kwanini ni viongozi. Dunia ina tabia ya kuweka nafasi kwaajili ya watu ambao maneno yao na vitendo huonyesha wanafahamu ni wapi wanakokwenda. Kutokuwa na uamuzi ni tabia ambayo kwa kawaida huanzia ujanani. Tabia hukomaa kwa kadiri ujana unavyokwenda kupitia shuleni na hata kupitia Chuo Kikuu au Chuo bila ya kuwa na ukamilifu wa lengo. Udhaifu mkubwa wa mifumo yote ya elimu ni kwamba hawafundishi watu kusisitiza tabia ya maamuzi kamili.

Lingekuwa ni jambo la faida ikiwa kungekuwa hamna Chuo kikuu au chuo ambacho kingeruhusu udahili wa mwanafunzi yeyote mpaka aweze kutamka malengo yake makubwa ya kumaliza masomo ni yapi. Ingelikuwa bado ni jambo lenye faida kubwa zaidi ikiwa kila mwanafunzi anayeanza shule angelazimishwa kukubali mafunzo katika mtindo wa maamuzi, na kulazimishwa kufaulu mtihani wa ridhaa katika somo hili kabla ya kumruhusu kuendelea.

Tabia ya kukosa uamuzi ilishikwa kwa sababu ya mapungufu ya mifumo ya mashule yetu kuwapeleka wanafunzi kwenye fani wanazochagua, ikiwa kweli wanachagua fani zao. Kwa ujumla vijana ambao ndio wanatoka kumaliza shule hufanya kazi yeyote inayoweza kupatikana. Wanachukua nafasi ya kwanza wanayopata kwasababu wameangukia katika tabia ya kutokuwa na uamuzi. Watu tisini na nane kati ya kila watu mia moja wanaofanya kazi ya kuajiriwa leo wapo katika nafasi wanazoshikilia kwasababu walikosa ukamilifu wa maamuzi ya kupanga nafasi kamili, na maarifa ya jinsi ya kuchagua mwajiri. 

Ukamilifu wa maamuzi mara nyingi huhitaji ujasiri, wakati mwingine ujasiri mkubwa sana. Watu 56 waliosaini tangazo la uhuru waliweka rehani maisha yao katika uamuzi wa kubandika saini zao kwenye lile tamko. Watu wanaofikia uamuzi kamili kujipatia kazi fulani na kufanya maisha yalipe gharama wanayoomba hawatahatarisha maisha yao katika uamuzi huo, wanahatarisha uhuru wao wa kiuchumi .

Uhuru wa kifedha, utajiri, biashara nzuri na nafasi za ajira hazipo ndani ya uwezo wa kuzifikia kwa mtu anayepuuzia au kukataa kutegemea kupanga na kuvidai vitu hivi. Mtu anayetamani utajiri katika roho ileile Samuel Adams aliyotamani Uhuru wa Makoloni ana uhakika wa kupata utajiri.

Katika Sura ya 7 ya Mpango madhubuti utakuta maelezo kamili kwa ajili ya kutafuta soko la kila aina ya huduma. Utapata pia maelezo ya kina juu ya kuchagua mwajiri unayemtaka na kazi unayotamani. Maelekezo haya yatakuwa hayana thamani kwako ikiwa kama HUTAAMUA MARA MOJA kuyaweka katika mpango wa kivitendo.


Leo tumemaliza sura ya 8 ya kitabu hiki Fikiri Utajirike au Think & Grow Rich, Alhamisi tukutane tena kwa Sura mpya ta 9


 UKITAKA KUSOMA SURA ZOTE ZA KITABU KIZIMA


...............................................................

*Semina yetu ya Michanganuo ya biashara inaendelea katika group la whatsapp la MICHANGANUO ONLINE, email na private blog kwa kiingilio cha sh. elfu 10. Masomo ni kila siku usiku saa 3. Ofa mbalimbali vikiwemo vitabu, templates na masomo ya semina zote zilizopita. kUJIUNGA tuma ujumbe wa wasap kwa namba 0765553030 au bonyeza link, https://chat.whatsapp.com/KO79AIJZOMVHBY2SlDdJBC

Kwa vitabu fungua SMART BOOKS TANZANIA.


0 Response to "UHURU KIFEDHA, UTAJIRI, BIASHARA NA AJIRA NZURI VIPO KWA YULE ANAYEPANGA NA KUVIDAI"

Post a Comment