NIMEIPENDA STAILI ALIVYOJIONGEZA DADA HUYU NA BIASHARA YAKE YA CHAKULA

Alianza biashara yake kama ilivyokuwa ada kwa wajasiriamali wengine wote wadogo wadogo wanapoanza, kwa kukodisha kioski kidogo cha mabati ya kontena, kidogo usije ukafikiri labda ni saizi ya kontena zima la futi 40 hapa. Mfano wake kama umewahi kuona vibanda hivi vya kuuzia vocha au kutoa na kuweka pesa kwenye simu vinavyowekwa kwa muda(temporally) katika maeneo yasiyoruhusiwa rasmi na serikali kwa urahisi wa kuvihamisha pindi lolote linapotokea. Hata kusimama wima ilikuwa ni shughuli.

Na mimi ndiyo maeneo ninakopita kuelekea stendi ya basi kwa hiyo huwa namuona pale kila mara nipitapo akihangaika na kompyuta yake ndogo, pembeni ameweka kiprinta kidogodogo pamoja na vifaa vingine vya steshenari. Ilikuwa ni biashara ya stationary lakini kwa haraka haraka kama hukutazama vizuri unaweza ukasema ni kibanda cha kuingiza nyimbo kwenye simu. Dada wa watu akapiga kazi kama mwaka na kitu hivi, mara siku napita pale nikakuta kesha hama, kahamia upande wa pili mahali palipokuwa na fremu ya duka ilyohamwa siyo siku nyingi, sasa palikuwa pa kutosha hata hewa alikuwa akivuta kwa kujinafasi.

Niliendelea kufuatilia maendeleo ya huyu dada kila nilipokuwa nikipita pale kwani niliona alikuwa na mwenendo fulani hivi usiokuwa wa kawaida ambao nitaeleza baadaye kidogo katika makala hii hii. Miezi mitatu tangu ahamie pale kabla haijamalizika nikagundua tena mabadiliko mengine ofisini kwa huyu dada wakati nikipita jambo lililonishawishi nitafute sababu ya kwenda pale nijifanye nahitaji kitu ili nimsome vizuri na mambo yake haya yasiyotabirika. Dada sambamba na vile vifaa vya steshenari alikuwa ameweka kabati dizaini fulani hivi kama la chipsi lakini lina ngazi mpaka chini za kupanga vinywaji mbalimbali, juu aliweka chipsi na vyakula vingine kama nyama za mishikaki, vitafunwa na ndizi za kukaanga. Kwa kweli vilikuwa vinavutia. Ilikuwa ni biashara ya chakula na vinywaji ndani ya biashara ya stationary. Sijui aliwaza nini dada huyu, nadhani watu wengi walikuwa wakimshangaa sana wengine wakibeza na wngine kusifia ila yeye hakujali, aliendelea kupiga kazi.

TABIA YAKE YA AJABU!
Nilikuahidi nitakueleza tabia yake ya ajabu. Hufanya maamuzi yake haraka sana akihisi ni maamuzi sahihi na kuchelewa kuyabadilisha, tabia iliyokuwa muhimu sana kwa mjasiriamali makini ambaye kufanikiwa kwake ni lazima kutokee hata kama siyo leo wala kesho. Akiona uamuzi alioufanya siyo sahihi au unampeleka kwenye hasara badala ya faida hachelei kuubadilisha mara moja na mwingine uliokuwa na tija.

Halafu isitoshe hafanyi hivyo kichwakichwa, hupima kwanza, na mfano ni pale unapoona anaamua kuchanganya biashara ya chakula na steshenari akijua kabisa hawezi kukurupuka kuifunga mara moja stationary yake angali hajui kama biashara ya vyakula na vinywaji itamletea mapato ya kutosha au la.

Bado naendelea kumfuatilia dada huyu nyendo zake mpaka nijue hatima yake ni nini, nakuahidi nitaendelea kukupa matokeo ya ufuatiliaji wangu huu kwa kadiri mapya yatakavyokuwa yakiendelea kujifunua kwani naamini kabisa dada huyu anayo stori nzuri ya kusimulia. Kumbuka ni wiki hii hii tu nilipopita pale na kumkuta akipanga panga vinywaji kwenye friji lake nilipojifanya nakwenda kutoa fotokopi pale.

Mwenendo wa huyu dada kilichonifanya uniguse kiasi hiki ni jinsi nilivyouhusianisha na yaliyowahi kunikuta mimi binafsi katika safari yangu ya ujasiriamali, kweli kuna wakati inabidi tujifunze kutokana na makosa tufanyayo ijapokuwa njia hiyo ni chungu na ndefu. Mimi nyakati fulani niliwahi kufanya kosa kubwa sana la kuachana na biashara niliyokuwa nikiifanya kwa matumaini kuwa biashara mpya iliyokuwa mbele yangu ingeweza kunipa mapato makubwa kushinda ile ya zamani wakati nilikuwa na nafasi nzuri tu ya kufanya kama huyu dada wa shoka alivyofanya. Matokeo yake nayajua mwenyewe, ipo siku nitakusimulia lakini kwa kweli hayakuwa mazuri kama nilivyokuwa nimedhania.

Uzoefu huu unafanya kazi vilevile hata na kwenye ajira, muulize mtu aliyeachana na ajira yake ghafla kwa matumaini ya kufanya biashara ya ndoto yake atakusimulia, ingawa inawezekana alikuja kujinasua lakini hebu muulize ilikuja kumchukua muda gani mpaka kurudisha tena hali yake ya zamani, kama alikuwa akila nyama kila mwisho wa wiki muulize baada ya kuachana na ajira yake kimhemko, je nyama aliiona tena? Hivyo yafaa tuwe makini sana tunapofanya (mabadiliko)transitions katika shughuli zetu na hususan biashara tunazozifanya bila kujali kama biashara hiyo ya awali inatupa fedha kiasi gani.

…………………………………………

Mpenzi msomaji wangu , naendelea kukuletea makala za kina katika blog yako hii, makala ambazo kwa kweli kama utakuwa ukizifuatilia mara kwa mara hutabakia kama ulivyo, ni kazi ninayoifanya kwa passion(kutoka moyoni kabisa) na wala si kama nasaka pesa kama vile mtu mwingine anavyoweza kufikiria. Ndiyo ni kweli tumeweka kiingilio kwa semina au malipo kwa baadhi ya vitabu vyetu kwa yule anayehitaji huduma hizi kwa kina kabisa lakini ni kutokana tu na kuzifanya huduma hizi ziweze kuwa endelevu kama vile ambavyo ungependa kibatari chako kiendelee kuwaka kwa kutia ndani yake mafuta ya taa kidogo.

Ili uweze kuwa karibu kabisa na mimi, Peter Augustino Tarimo pamoja na timu au kundi langu la kushauriana MASTERMIND GROUP la MICHANGANUO ONLINE, na wewe kuwa miongoni mwa kundi hilo, toa kiingilio kidogo cha shilingi elfu 10 tu, mjasiriamali ni lazima unapotoa fedha yako hata kama ni kidogo lakini uhakikishe unapata thamani halisi inayozidi pesa uliyotoa, hiyo ni sheria(principle) namba 1 katika kutengeneza nidhamu ya hali ya juu ya fedha, somo tunalosoma kila siku kundini.

Kundini tunajifunza pia mambo mengi ikiwamo namna ya kuchanganua biashara mbalimbali pamoja na michanganuo yenyewe halisi ya biashara bunifu za kipekee zilizokuwa na uwezo mkubwa wa kutengeneza mzunguko chanya wa fedha. Kundi lina wataalamu na wazoefu waliobobea katika fani mbalimbali za ujasiriamali kama vile ufugaji wa kuku aina zote, tunao watu kama kina FRANK MAPUNDA ambao hakuna kitu kinachowashinda katika ufugaji wa kuku aina zote.

Njia ya pili ya kuwa karibu zaidi na Peter na kundi lake ni kwa kusoma vitabu vyetu vya self help books Tanzania, bonyeza maandishi hayo kuviona vitabu vyote, unaweza kununua kimoja kimoja au vyote kwa pamoja na vingine ni free, hulipi chochote. Vile vya kununua ukitaka vyote 3 ni sh. Elfu 18 tu, unatumiwa kwenye email yako na kuvisoma jinsi unavyosoma hapa baada ya kutuma pesa kwa njia ya simu. Ukitaka vya karatasi tuwasiliane nitakupa utaratibu wa kuvipata.

Siku ya leo Jumapili ya tarehe 4 Feb. 2018, Kundini tunajifunza somo la jinsi ya kuufanya mtiririko wa fedha katika biahsra zetu kuwa chanya, kwa mada isemayo hivi;

 “ THE SKY IS VERY WIDE, EVERY STAR CAN SHINE(MBINGU NI PANA VYAKUTOSHA, KILA NYOTA INAWEZA KUNG’ARA

0 Response to "NIMEIPENDA STAILI ALIVYOJIONGEZA DADA HUYU NA BIASHARA YAKE YA CHAKULA"

Post a Comment