KUONDOA UMASIKINI, MAPINDUZI YA VIWANDA BILA KUWEKEZA KILIMO NI KAZI BURE-HUSSEIN BASHE | JIFUNZE UJASIRIAMALI

KUONDOA UMASIKINI, MAPINDUZI YA VIWANDA BILA KUWEKEZA KILIMO NI KAZI BURE-HUSSEIN BASHE

SAUTI
VIDEO

Kitu kinachonifurahisha katika dhana ya mihimili ya Dola ni ile kuwepo kwa kila mhimili kuwa huru katika kutekeleza majukumu yake katika kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo. Unapotazama bunge likiendelea pale Dodoma, inafurahisha kuona jinsi wabunge kutoka pande zote mbili, ule wa Chama tawala na Upinzani wanavyoikosoa na kuishauri serikali katika mambo ya msingi kama ya haya ya uchumi. Linapokuja suala la kuondoa umasikini wa Watanzania Wabunge huweka tofauti zao kando.

Serikali ya awamu ya 5 inafanya mambo makubwa sana, lakini haiwezi kufikia malengo yake yote kikamilifu kama haya ya kulifanya taifa kuwa na uchumi wa viwanda peke yake bila ya ushauri kutoka kwa  wadau wengine, mtu mmoja, chama kimoja, au mawazo ya upande mmoja tu hayataweza. Ni kwa njia ya kukosoa na wakati mwingine kukubaliana na mawazo mbadala ndiko kutakako tufanya kama Taifa kutoka pale tulipo.

SOMA: Dr. Slaa, Professa Lipumba, Ujasiriamali wa Kisiasa upo wapi?

Rais wetu na serikali yake tunaweza kumsaidia kufikia malengo yetu sote kwa kujenga utamaduni wa kutoa mawazo mbadala yenye tija bila kuchukuliwa kama usaliti, kama anavyofanya Bashe na wengineo wengi katika Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania. Nadhani mchango kama huu wa Hussein Bashe na hata wabunge wengine kama Mheshimiwa Sugu wa Mbeya mjini, Peter Serukamba wa Kigoma Kaskazini, Mh. Freeman Mbowe wa Hai na Richard Ndassa wa Sumve si ya kubomoa hata kidogo yana uwezo wa kusaidia kwa kiasi kikubwa katika kuhakikisha tunafika kule tunakotaka kufika kama Taifa. Wabunge hao walikuwa wakichangia  katika mjadala wa Mpango wa Maendeleo wa mwaka 2017/2018.

Hapa ni mchango wa Mheshimiwa Hussein Bashe, Mbunge wa jimbo la Singida Mjini, hotuba yake nzima tarehe 9 November 2017 akichangia kwenye Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Mwaka 2017 kuelekea 2018 uliowasilishwa na Mh. Waziri wa fedha na mipango Dr. Phillip Mpango;


"Mweshimiwa mwenyekiti, kwanza nitumie fursa hii, kuwapongeza waheshimiwa mawaziri ambao wamebaki kwenye nafasi zao, na mawaziri wapya na manaibu waziri walioteuliwa na mheshimiwa rais katika mabadiliko ya baraza la mawaziri la hivi karibuni niwatakie kila la heri katika kutimiza wajibu wao.

Mh. Mwenyekiti, mwaka 2016 wakati tunajadili mpango ndani ya bunge hili, nilimtahadharisha waziri wa mipango, nikimwambia kwamba mpango unaouleta, hautofikia economic growth  ya 7%.  Kwa sababu mpango huu unaacha sehemu kubwa ya Watanzania nje, siyo mpango inclusive. Mwaka 2017, mwaka 2016 wakati tunajadili bajeti nilirudia  maneno haya,  na mwaka huu wakati  tunajadili bajeti nilimwambia, kuna conflict kati ya  fiscal policy ambazo Wizara  ya fedha inazisimamia na Monetary policy,  these two policies zinapambana zenyewe na matokeo  yake  yataonekana.

Mheshimiwa Mweneyekiti naomba ninukuu takwimu zifuatazo, kama alivyosema ndugu Serukamba, “Uchumi wowote Duniani una mirror, kioo  na kioo cha uchumi wowote unaokua, ama unaosinyaa,  ama unaoshuka, moja ni financial  institution, mbili ni trade, tatu ni stock exchange. Mh. Mwenyekiti,  personal lending mwaka 2015 illikuwa ni asilimiaa 25%, today ni 8.9%, trade ilikuwa ni asilimia 24%, this is a lending to trade,  ilikuwa ni asilimiaa  24%, leo ni asilimia 9%, na maneno haya siyatoi kwingine, ni ripoti za BOT na quarter report ya BOT inayoishia June, lakini taarifa  zingine ni muongozo wa bajeti  alioleta yeye, na ni mpango wake alioleta yeye. 

Agriculture, leo ni negative nine (-9)%,  from 6% lending capacity ya mwaka 2015. Manufacturing, from 30% lending to 3%. Transport and communication, from 24% lending to negative twenty five(-25)%, building, from 22% to 16%. Mh. Mwenyekiti, our economy it is said inakua, ukisoma projections  ni 6.8%, lakini taarifa ya mwisho ya economic bulletin  for the quarter ending June 2017 imetuambia ni 5.7%, siyo maneno yangu.

Food inflation, let’s go categorically, it is 10.1%, siyo maneno yangu, taarifa ya Septemba ya BOT hii hapa. Mh. Mwenyekiti, why are we facing this, it’s not a rocket  science, Waziri wa fedha ukurasa wa sita wa mpango, unasema  Export, na Mwenyekiti naomba iingie kwenye  hansadi ya Bunge, nimeangalia taarifa za monthly za BOT toka mwaka 2011 mpaka Septemba mwaka huu, for  the first time in the history, hamjaweka performance ya export and Imports, why, mnaficha nini?.

SOMA: Hotuba ya Rais Obama nchini Kenya akifungua kongamano la Wajasiriamali.

Alisema ndugu Abdurahaman Kinana Mwenyekiti, wakati anaongea katika function ya Kigoda pale University of Dar  es salaam, alisema hivi, namnukuu katibu wa chama chetu; “Jambo muhimu la kiongozi ni kusikiliza watu wake, viongozi  hamna monopoly right ya wisdom, viongozi hawana monopoly right ya truth, viongozi  hawana monopoly right ya wao wako sahihi kila siku” Na Mheshimiwa Mwennyekiti hakuna jambo  muhimu katika kupanga mipango yeyote duniani kama takwimu. Ukurasa wa 7 wa document ya mapendendekezo ya mpango, unaonyesha mwenendo wa ukuaji wa pao la Taifa, toka mwaka 2011 mpaka 2017. 2011 our growth was 9.1%, today it is projected 6.8% lakini as per this report ni 5.7%.

Mwenyekiti naomba ninukuu maneno yafuatayo, ukurasa wa 7 unasema; “Kufikia June 2017 export zilikuwa zimeshuka kwa asilimia 29.8%, lakini Waziri anatupa a consoling statement  kwamba matarajio ni kurejea kwa exportation kuongezeka, eti kwasababu tunajenga  kukuza viwanda, sasa twendeni tukasome hivyo viwanda vya export.  Siyo maneno yangu, kwenye mpango Waziri ametaja viwanda, ukurasa wa 26, kiwanda  cha kuchenjua madini kilichopo  Geita, kusindika nyama  Kisivani, Shinyanga, Mitobotobo Farmers company ltd,  kuzalisha mafuta ya kula, kuchambua pamba, kiwannda cha kuzalisha vifungashio- Global packing, kiwada cha kuzalisha vinywaji baridi Sunny food company-Sayona. Hivi ndiyo tuta  export kurudisha asilimia 29%. Kuzalisha bidhaa za  ujenzi, brother!  tumeahidi kuondoa umasikini wa watu, Mwenyekiti siyo maneno yangu, mimi naquote maneno ya Waziri wa Mpango.

SOMA: Mjasiriamali unawahitaji wateja wote, CCM na UKAWA

Twendeni ukurasa wa 68, sekta ya kilimo, look at this, hii ndiyo sekta imeajiri asilimia 65% - 70% ya  wananchi wetu, na kwa tafiti zillizofanyika ndugu Mwenyekiti, Watanzania zaidi ya asilimia 80% walioko kwenye sekta ya kilimo, yaani ile 70%, 80% ya hiyo 70% inafanya kazi mbili, duo, inalima na inafuga  kama siyo ng’ombe, mbuzi, kuku, bata, na vitu vya namna  hiyo, anafanya  duo, now look at  these two things ndugu  Mwenyekiti, Sekta ya mifugo, serekali imepanga kufanya uhimilishaji wa mifugo laki nne, tunahimilisha, kufanya insemination, ng’ombe laki nne na elfu hamsini na kitu. Lakini tunapanga kuzalisha chakula, hey, Mwenyekiti, hey  ni yale majani ya ng’ombe. Tunapanga kuzalisha chakula kwa mwaka laki nne na elfu arobaini na tano, hey kaki nne na elfu arobaini na tano. Kitakwimu hey moja ina uzito wa kilo 25. Chakula hiki ukikigawa kwa siku 360, kinalisha ng’ombe 1600 huku  unapanga kuzalisha ng’ombe kaki nne, lakini unaandaa mpango wa chakula cha ng’ombe 1600.

Mwenyekiti hapa Wabunnge wamejadili suala la kilimo, hakuna sehemu Waziri wa kilimo anaplan on the, kuanzisha price stabilization ya mazao ya chakula. Leo kuzalisha kilo moja ya mahindi, gharama ya shambani, ni shilingi 357, haya siyo maneno yangu, it’s scientifically proved, halafu huyu mkulima anayetumia shilingi 357 kuzalisha kilo moja ya mahindi, bado gharama ya kupeleka stoo, gharama ya kuweka mifuko, gharama ya kuweka dawa, halafu atakapoweka stoo yake, kuna kauli inasemwa hapa walanguzi ndio wana mahindi. Mwenyekiti, this is total misconception ya business principle, kote duniani, kuna producer, kuna distributer, kuna retailer, kwahiyo unataka kuniambia mimi ninayelima Nzega na hata mahindi yangu niyabebe niende nikayauze Nairobi?. Kuna Intermediaries, and this is the duty of your fiscal policies, kufanya intermediaries wafanye biashara.

Mwenyekiti nataka nikupe mfano mwingine, nataka nikupe mfano mwingine, profitability ya financial institution imeshuka over 50%. Waziri ana hoja moja dhaifu sana anaitumia ndani ya mipango, money circulation imepungua, Mwenyekiti, kutoka billion 222 mpaka bilioni 12, na hoja anayosema ni nini, matumizi yasiyokuwa ya lazima ya serikali  yamepungua. Sasa, najiuliza, bajeti ya reccurent imepungua? Kutoka 2011,12, 13 imepungua recurrent bajeti? No, spending ya government ipo  kwa hiyo nilitarajia kwamba itakuwa wisely tutaiona imeleta positive impact, lakini hakuna. Sasa mimi ushauri wangu kwa Waziri wa fedha Dr. Mpango, narudia,  this is a third time, naheshimu your academic background, sijawahi kudoubt, kaka, hauwezi kuondoa umasikini wa nchi hii bila kuwekeza kwenye kilimo, never, hauwezi kuleta mapinduzi ya viwanda, mapinduzi ya viwanda, bila kuwekeza kwenye kilimo.

SOMA: Wajasiriamali wataka mwakilishi Bunge la katiba.

Mwenyekiti, mkulima wa nchi hii, ndio kageuka punching box ya nchi hii, tunacontrol inflation ya chakula kwa gharama ya mkulima. How come, haiwezekani, hatuwezi kufanikiwa kwa namna hii. Yaani sisi tunadhibiti mfumko wa bei kwa kumtia umasikini mkulima. Aina gani za economy hizi? Mwenyekiti nataka nikupe mfano mdogo tena, aangalie, hatuwezi kuondoka kwenye umasikini kama mawazo ya wizara ya fedha hayatokuwa ni productive oriented, badala ya kuwa tax based approach, Mwenyekiti angalia mpango huu unakuwa financed namna gani. Waheshimiwa wabunge tuchukue document ya mpango musome how are we going to finance mpango, page namba 29 ya Muongozo wa maandalizi. (Mwnyekiti niilindie dakika zangu dk. moja tu.)

Mh. Mwenyekiti, Waziri anasema kwamba how to finance, anazunguzia kwamba ata improve  EFD mashine, ataanzisha maabara ya TRA. It is all about Tax based approach. Haumsikii anasema kwamba tutawekeza bilioni moja kwenye kilimo cha mahindi, ili tuweze kuyield X, hausikii. Hauwezi kukamua maziwa ng’ombe usiyemlisha. Mh. Mwenyekiti, ukiangalia VAT, pay as you earn, zimeshuka, hazifikii target aliyojiwekea kwenye bajeti ya 17, na hapa anasema, kwamba makampuni yamepunguza wafanyakazi, na unajua  ni kwanini?. It’s not a rocket science Mwenyekiti, tulimshauri kwenye kamati ya bajeti, kwamba, unaongeza excess duty kwenye TBL, utapunguza uwezo wa uzalishaji wa hawa watu, hakusikia, tumemwambia kwenye kamati ya bajeti, I was there, tumemwambia Waziri wa fedh, unaua viwanda vya soft drink, kwa kuimpose 10% eti kwa udhaifu wao TRA wa kusimamia sukari inayoingia, wameweka asilimia 10% tena on top. Kwa hiyo cocacola akiingiza sukari kwenye nchi hii analipa 25%, instead of 15%, what kind of economy is this. Serekali, serekali Mwenyekiti, na mimi nataka niwaambie waheshimiwa wabunge hasa wa chama changu, tumepewa dhamana ya nchi hii na Watanzania, let’s not allow mistakes za Waziri Mpango kuharibu nafasi ya kuchaguliwa kwa rais wetu  mwaka 2020.

Mwenyekiti samahani, nikupe mfano mdogo, kampuni zote za vinywaji baridi, zilikuja mbele ya kamati ya bajeti, na sisi tukawaita Wizara ya fedha, hawana capacity ya kwenda kukagua bonded ware house, hawana capacity hiyo madhara yake unajua wamefanya nini Mwenyekiti?, wameamua kuanzisha kodi mpya ya kuwithhold, sasa hivi private sector inadai TRA over eight hundred billion shiliing, za returns on Tax, hawalipi, wanasuffocate, this is very wrong, na mimi nimalizie niseme Mwenyekiti samahani, kama Waziri wa fedha hatabadilika, hatuwezi kutoka hapa. Asante."

Credit: Picha na Mtandao wa Mtanzania, video by AyoTV

0 Response to "KUONDOA UMASIKINI, MAPINDUZI YA VIWANDA BILA KUWEKEZA KILIMO NI KAZI BURE-HUSSEIN BASHE"

Post a Comment