NI SIKU YA MWISHO YA SEMINA AWAMU YA 3 LEO LAKINI BADO HAIJACHACHA, NAFASI IPO | JIFUNZE UJASIRIAMALI

NI SIKU YA MWISHO YA SEMINA AWAMU YA 3 LEO LAKINI BADO HAIJACHACHA, NAFASI IPO


Semina yetu ya namna ya kuandaa mpango wa biashara au mchanganuo wa biashara katika blogu maalumu ya kiingilio iitwayo DARASA LASEMINA YA MICHANGANUO YA BIASHARA, leo hii ndiyo inafika mwisho wake lakini habari njema ni kuwa Semina hii jinsi mfumo wake ulivyotengenezwa ni kwamba HAICHACHI.

Ikiwa hujajiunga na una nia ya kupata semina hizo basi unaweza ukajiunga hata baada ya muda wa mwisho. Masomo yote toka awamu za nyuma yamehifadhiwa katika blogu hiyo maalumu. Unachopaswa tu kufanya ni kulipa kiingilio chako shilingi elfu 10 kupitia namba za simu 0712202244  au  0765553030, jina  litokee Peter Augustino Tarimo, unatuma na anuani yako ya e-mail kwa meseji kisha utatumiwa email yenye link ya kuingia katika BLOGU HII.


Siku ya tatu ya awamu hii ya 3 ya semina tutamalizia na vipengele vya Muhtasari, Biashara, Mikakati na Utekelezaji vya mchanganuo wa biashara ya saluni ya kike, Rse Hair & Beauty Saloon iliyopo maeneo ya Mwenge jijini Dar es salaam. Utaona toka mwazo hatukufuata mlolongo rsami wa vipengele kama unavyotakiwa kuwa nah ii ni kuonyesha kwamba unapoandika mchanganuo wa biashara siyo sheria au lazima kwamba ufuate mlolongo sawasawa kama ulivyo, unaweza ukaanza na kipengekle chochote kile.

Nachukua pia nafasi hii kuwashukuru sana washiriki wote tuliokuwa wote katika semina hii na awamu nyingine zote zilizopita, nawaahidi tutakuwa na semina nyingine nyingi hapo baadae zilizokuwa na manufaa makubwa kwa wote mtakaoshiriki na wale watakaojiunga baada ya hapa.

Mwisho nawatakia kheri wale wote waliofunga, Mfungo Mtukufu wa Ramadhani.


0 Response to "NI SIKU YA MWISHO YA SEMINA AWAMU YA 3 LEO LAKINI BADO HAIJACHACHA, NAFASI IPO"

Post a Comment