THINK AND GROW RICH, MAPITIO YA KITABU SURA YA KWANZA (1) | JIFUNZE UJASIRIAMALI

THINK AND GROW RICH, MAPITIO YA KITABU SURA YA KWANZA (1)

UTANGULIZI.

v Mawazo yasiyoshikika yanaweza yakageuzwa kuwa kitu kinachoshikika kama vile mali au pesa kwa kutumia kanuni maalum.

v Chanzo  kikubwa cha kuanguka  ni tabia ya kukata tamaa baada ya kukutana na vikwazo vya muda mfupi.

v Badala ya kukata tama unapoanguka, tumia uzoefu ulioupata kufanya vizuri zaidi.

v Utajiri unapoanza kukujia  kwa wingi kiasi ambacho unaweza ukashangaa ni kwa nini haukuja siku zote ulizosubiri, na utajiri huo huanza na wazo kichwani pamoja na lengo  mahususi pasipo hata chembe ya kazi ngumu.

v Mafanikio humjia mtu anayewaza mafanikio, ubongo huambukizwa mawazo tunayofikiri midhili ya sumaku, na sumaku hiyo huvuta nguvu, watu na mazingira yeyote yale yanayohusiana na mafanikio.

v Kwa hiyo kabla hatujaanza kutengeneza utajiri ni sharti kwanza tuziambukize akili zetu hamu kubwa  ya  kutaka kutajirika baada ya hapo, kuwa na lengo na kisha kukomalia lengo hilo bila kukata tamaa mpaka pale tutakapofanikiwa. Waambukize na watu wengine uliokuwa nao karibu (washirika) ili wakusaidie kukamilisha lengo lako.


>>>EndeleaSura ya 2 hapa>>>>>                                 

<<<Rudi sehemu iliyopita hapa<<                                 

0 Response to "THINK AND GROW RICH, MAPITIO YA KITABU SURA YA KWANZA (1)"

Post a Comment