KAHAWA NA KASHATA NI MOJA YA BIASHARA NDOGO ZINAZOLIPA SANA UKIFANYA KIUBUNIFU | JIFUNZE UJASIRIAMALI

KAHAWA NA KASHATA NI MOJA YA BIASHARA NDOGO ZINAZOLIPA SANA UKIFANYA KIUBUNIFU


Wazo la kuandika kuhusiana na biashara hii ya kuuza kahawa na kashata lilinijia akilini baada ya hivi karibuni nikiwa nakatiza stendi moja maeneo ya mbezi, ghafla nilianza kuhisi harufu nzuri na ya kuvutia ya kitu. Kahawa siyo kahawa, tangawizi siyo tangawizi; nikajawa na shauku kubwa ya kutaka kujua harufu ile nzuri ilikuwa inatokea wapi.

Nilipopepesa macho kidogo, kando ya kinjia cha uchochoro nilichokuwa nikielekea nikaona watu, wazee kwa vijana wameketi huku mikononi wakiwa wameshika vikombe vya kahawa wanakunywa. Sikusita mara moja nikasogea na kuketi kwenye benchi nikaagiza na mimi nipewe kikombe cha kahawa. Lakini muuza kahawa aliniuliza, “kahawa tupu au na tangawizi?”, nikamjibu “weka na tangawizi kidogo”, mimi nikifikiri ni tangawizi ya unga iliyosagwa na kutiwa kwenye kichupa kama niliyozoea kuiona kwa wauza kahawa wengi.

SOMA: Unajua biashara ya chipsi kuku na soda inavyolipa dar?

Muuza kahawa alimimina kahawa nusu kikombe na kisha nikaona akichukua birika jingine tena na kujazia sehemu iliyobakia, kumbe lile birika la pili lilikuwa na tangawizi ya maji iliyochemshwa na kuwiva vizuri. Mchanganyiko wa vitu hivi viwili, kahawa na tangawizi unatoa harufu nzuri na ladha ya kipekee ambayo mtu yeyote atavutika kunywa na inao uwezo wa kumvuta hata mtu aliyeko umbali wa mita kadhaa kutoka muuza kahawa alipo. Halafu kingine nilichoona ni ubunifu, mabirika ya tangawizi yapo mawili, moja hutia sukari na la pili ni tangawizi tupu isiyokuwa na sukari.

SOMA PIA: Hakuna biashara isiyokuwa na faida. 

Wakati anakumiminia tangawizi huwa anakuuliza ikiwa utapenda yenye sukari au isiyokuwa na sukari. Na kweli watu wengine hawapendi kahawa kwasababu huuzwa kavu bila ya sukari, inapochanganywa na tangawizi yenye sukari kundi hili la watu huvutika kunywa kahawa na kwa namna hiyo basi muuzaji anakuwa ameongeza idadi ya wateja ambao muuza kahawa wa kawaida tu asiyeweka ubunifu wa aina yeyote ule hawezi akawapata.

.................................................................................................

Kwa mawasiliano na sisi, au kuagiza vitabu, tumia njia zifuatazo;

SIMU:                 0712 202244,  au 0765 553030  au 0689 303098

TELEGRAM:      0712 202244 au @petertarimo

E-MAIL:              jifunzeujasiriamali@gmail.com

BOOKSHOP:     @Smartbookstz

Kupata vitabu vizuri bila malipo pamoja na makala "exclusive" kila wiki mara 2 jiunge na blogu hii hapa kwa kujaza email yako na jina.

0 Response to "KAHAWA NA KASHATA NI MOJA YA BIASHARA NDOGO ZINAZOLIPA SANA UKIFANYA KIUBUNIFU"

Post a Comment