TUJULISHE POPOTE ULIPO DAR TUKULETEE VITABU HIVI VIZURI VYA BIASHARA NA UJASIRIAMALI | JIFUNZE UJASIRIAMALI

TUJULISHE POPOTE ULIPO DAR TUKULETEE VITABU HIVI VIZURI VYA BIASHARA NA UJASIRIAMALI

Habari ndugu msomaji, Natumaini unaendelea vyema na shughuli zako za kila siku, iwe ni za kiuchumi kama vile biashara, kazi na taaluma mbalimbali au hata shughuli za kimafunzo kama vile wanafunzi  mashuleni, vyuoni na taasisi mbalimbali za elimu.

Sasa hivi  vitabu vyako (VYA KARATASI) kutoka kampuni ya Self Help Books, kwa wateja waliopo jijini Dar esa salaam wanaweza wakavipata kwa njia rahisi zaidi kuliko ilivyokuwa hapo awali kwa kuletewa mpaka pale walipo. Utaratibu huo utakuwa ukitumika sambamba na taratibu zinginezo za zamani ambazo zilikuwa ni mteja kuvinunua kutoka kwa mawakala wetu au kuvifuata ofisi yetu iliyopo Buguruni.

Ukihitaji kuletewa kitabu shochote kile kati ya hivyo vilivyotajwa hapo juu, wasiliana na sisi kwa simu, na mmoja katika timu yetu atakuletea kitabu ukipendacho mara moja. Hautadaiwa gharama za ziada wala nauli. Utaratibu huu wa kuwapelekea wateja walipo ni ofa maalumu na ofa hiyo itaaaendelea kwa kipindi fulani.

Mteja usije ukahofia labda ukiniambia nikuletee hicho kitabu cha shilingi elfu tano wakati upo pengine Tegeta au Mbagala nitaona ni mbali, hapana, hii ni kazi yetu na tumedhamiria kukuhudumia bila kuchoka hadi pale tutakapohakikisha umepata kile unachokihitaji kwa ajili ya kuboresha biashara na maisha yako kwa ujumla.

Kwa wale wateja wa mikoani tutaendelea na utaratibu ule ule wa kutuma kwa kutumia mabasi, kumwagiza mtu anayekuja Dar, au kwa njia ya E-mail kwa vitabu vya Mifereji ya Pesa pamoja na  Siri ya mafanikio ya Biashara ya rejareja. Unaweza kucheki vizuri zaidi vitabu hivyo na maelezo yake kwa undani katika ukurasa huu hapa wa, SMART BOOKSTZ.


0 Response to "TUJULISHE POPOTE ULIPO DAR TUKULETEE VITABU HIVI VIZURI VYA BIASHARA NA UJASIRIAMALI"

Post a Comment