UNAJUA BIASHARA YENYE FAIDA KUBWA NA YA HARAKA MARA 2 YA MTAJI UTAKAOWEKEZA? | JIFUNZE UJASIRIAMALI

UNAJUA BIASHARA YENYE FAIDA KUBWA NA YA HARAKA MARA 2 YA MTAJI UTAKAOWEKEZA?

biashara zenye faida kubwa na ya haraka
“Hivi ni biashara gani yenye faida kubwa na ya haraka  ninayoweza kuanzisha?” Hili ni swali ambalo bila shaka yeyote ile kila  anayefikiria kuanzisha biashara mpya au hata mwenye biashara lakini angependa kujitanua zaidi hujiuliza. 

Ingawa kimsingi hakuna biashara isiyokuwa na faida, lakini faida ya biashara katika sekta tofauti hutofautiana kulingana na tofauti pia katika mahitaji, nikiwa namaanisha gharama mbalimbali zinazohusika katika kuanzisha na kuendesha biashra zenyewe. Kuna biashara ambazo gharama za kuanzisha ni kubwa, hali kadhalika pia zipo biashara  ambazo gharama za uendeshaji wake ni kubwa na kuna biashara nyingine utakuta gharama zake zote wakati wa kuanzisha na hata kwenye uendeshaji ziko chini sana.

Hatua ya kuanza biashara ndiyo hatua ngumu kushinda hatua zingine zote na sababu kuu inayotengeneza ugumu huo si nyingine bali ni mtaji au rasilimali za kuanzia ambazo mara nyingi na kwa watu wengi wanaoanza biashara huwa changamoto yao kubwa ni namna ya kuweza kupata rasilimali za kutosha kuisimamisha biashara husika.

Kwa sababu hiyo ndiyo maana utakuta watu wengi wakiumiza vichwa kutaka kufahamu biashara watakazofanya kwa rasilimali(mtaji) kidogo waliokuwa nao lakini wakati huo huo wakipata faida kubwa katika kipindi kifupi inavyowezekana.



Mtaji kidogo ni chanzo kikubwa cha ‘vifo’ vya biashara nyingi ndogo ndogo zinazoanza na pia ndiyo chanzo kikuu cha wamiliki wa biashara hizo kushindwa kutenganisha matumizi ya fedha za biashara na yale ya kwao binafsi  kwani kwa mfano pale mtu anapokumbana na hali ya ugojwa wa mpendwa wake mathalani mtoto, inakuwa vigumu mno kusita kutumia pesa ya biashara kuokoa maisha ya mtoto huyo. Ni kipi bora, afe mtoto au ife biashara?

Ili basi kuepukana na changamoto zote hizi ndipo sasa utakuta watu wakijiuliza “Ni biashara gani iliyokuwa na faida kubwa inayoweza ikafanyika haraka katika kipindi kifupi na kurudisa mtaji wote uliowekezwa?.”

Katika kutafiti ni biashara ipi nzuri inayolipa haraka, yapo  mazingira na vigezo  vingi  mtu anavyotakiwa kuzingatia wakati anapotaka kuanzisha biashara iitakayomlipa vizuri. Kwa mfano wazo la ni biashara ipi mjasiriamali afanye, atatakiwa kutumia mbinu hizi nne kupata wazo bora la biashara itakayofaa.
1.  Anaweza akafikiria ni kitu gani anachopendelea zaidi kukifanya maishani kwake,
2.  Wazo linaweza likatokana na taaluma mtu aliyosomea,
3.  Uzoefu wa muda mrefu katika jambo fulani,
4.  Matatizo na mahitaji katika jamii nk.
Mjasiriamali hapaswi kuangalia tu faida peke yake kama kigezo cha kuamua ni wazo lipi la biashara itakayomfaa bali pia atatakiwa aangalie na vigezo vingine kama hivi vifuatavyo’
·       Je, biashara hiyo inaoana na ujuzi aliokuwa nao?
·       Ni aina gani ya leseni ya biashara inayohitajika katika biashara aliyochagua?
·       Kama kuna mafunzo yatakayohitajika, ni mafunzo ya aina gani?
·       Ni lazima achunguze pia jinsi biashara itakavyostahimili kipindi cha mdororo wa uchumi endapo utatokea.
Pamoja na mbinu na vigezo hivyo lakini mwishowe mtu huyo atapaswa kujitathmini mfukoni mwake ikiwa anazo rasilimali za kutosha kuanzisha mradi alioamua kuanzisha na hapo ndipo huja suala la kuangalia ni biashara ipi kati ya zile alizokuta zinaendana na mazingira yaliyokwishatajwa hapo juu ambayo anaweza akaianzisha.


TANGAZO.
biashara nzuri inayolipa



Biashara zenye faida kubwa na zinazolipa haraka kwa mtaji kidogo uliowekezwa.
Biashara  za utoaji wa huduma ndizo zinazoshikilia namba moja kwa kuwa na faida kubwa zaidi huku zingali zikigharimu mtaji kidogo kushinda biashara za aina nyinginezo kama za utengenezaji  na uuzaji wa bidhaa mbalimbali.

Asilimia ya faida kwa mauzo katika biashara nyingi za huduma utakuta zinafikia mpaka asilimia 20%. Hii ina maana kwamba katika kila mauzo ya shilingi 100 basi faida halisi ni shilingi 20, wakati  jumla ya gharama zote ni shilingi 80. Wakati kwa upande wa huduma asilimia ya faida kwa mauzo ikikadiriwa kufikia 20%, katika upande wa bidhaa utakuta inakadiriwa kuwa ni asilimia chini ya 10%.

Sababu kubwa 4 ni kwanini biashara za utoaji wa huduma zinakuwa na faida kubwa kiasi hicho?
                    I.        Biashara hizi kwa kiasi kikubwa zinaendeshwa kwa mtaji-rasilimaliwatu. Hakuna gharama kubwa za vifaa, malighafi wala usafirishaji.

                  II.        Gharama za uendeshaji kama vile mishahara, kodi, leseni na pango vipo chini sana, na ni kidogo jambo linalosababisha faida kuwa juu.


                III.        Gharama kidogo za kuanzisha, kwa mfano, nyingi ya biashara za huduma zinaweza zikaanzishwa majumbani- chumbani, sebuleni, barazani au hata katika kibanda cha stoo isiyotumika.

                IV.        Biashara za huduma huwa zinakuwa na wateja wanaojirudiarudia. Utakuta mteja anayenunua huduma kwako leo anarudi tena kwa huduma kama ileile baada ya muda fulani kupita hivyo kuendelea kukuingizia faida.



Hebu sasa tuanze kuzitazama baadhi ya hizo biashara za utoaji huduma zile zinazoongoza kwa kutengeneza faida nyingi zaidi. Kumbuka lakini biashara za huduma zipo nyingi sana zaidi ya hizo zilizotajwa hapo chini na mfano ni biashara kama hii ninayoifanya hapa(kwa kuwa mimi siyo mchoyo na kamwe nisingependa kuficha siri kama baadhi ya watu wengine wafanyavyo). 

Biashara ya kwenye mtandao wa intaneti ikiwa utaweza kutoa huduma watu wakazipenda, zina faida zaidi hata ya asilimia 50% nikiwa na maana mara 2 au 3 ya mtaji utakaowekeza. Kwa undani zaidi juu ya mada hiyo, unaweza ukasoma ndani ya kitabu chetu kilichojipatia umaarufu mkubwa cha "MIFEREJI 7 YA PESA NA SIRI MATAJIRI WASIYOPENDA KUITOA." bofya maandishi hayo kupata ufafanizi zaidi.

Biashara hizo ni pamoja na hizi zifuatazo;

1. UHASIBU, USIMAMIAJI WA MAKAMPUNI NA BIASHARA.
Haijalishi ikiwa hali ya kiuchumi ni mbaya kiasi gani, lakini watu ni lazima watahitaji huduma za uhasibu. Biashara hizi pia huhusisha shughuli zinazofanana nazo kama vile, Utunzaji wa mahesabu ya biashara, Ushauri wa kibiashara, huduma za ajira na matayarisho ya kodi. Hizi ndiyo biashara zinazoshikilia nafasi ya kwanza kabisa katika kutengeneza faida nono zaidi kidunia.


2. UWAKALA NA UDALALI WA ARDHI NA MAJENGO(Real estate agency and Brokers)
Uwekezaji halisi wenyewe katika biashara hii ya ardhi na majengo mafanikio yake yanategemea zaidi kuboreka kwa hali ya kiuchumi lakini siyo katika upande wa Madalali na Mawakala wake. Wao ni kinyume kwani hawana gharama kubwa za uendeshaji biashara zao. Hata hali ya uchumi idorore vipi madalali na mawakala wa biashara ya ardhi na majengo huendelea kupata faida nzuri. Kuanzisha biashara hii, mtaji pekee utakaohitajika ni fedha kwa ajili ya kupata leseni.

3. HUDUMA ZA KISHERIA.
Kama ilivyokuwa kwa upande wa huduma za uhasibu, pia huduma za kisheria gharama zake za ueneshaji na hata zile za kuanzia siyo kubwa sana na huwa wanapata wateja wanaorudi tena na tena hivyo kuifanya biashara hii nayo kuwa ni yenye faida kubwa. Biashara hii haiwahusishi mawakili wa kujitegemea tu peke yao, bali huwahusisha pia na mawakala wa shughuli za kisheria kama vile, madalali wa mahakama, wasuluhishi wa migogoro nk.

4.  UAZIMISHAJI NA UKODISHAJI WA MITAMBO.
Katika uchumi wa sasa usiotabirika kirahisi, watu wengi kununua mitambo kwa mfano, matrekta, vijiko na hata magari kwa ajili ya shughuli za muda mfupi huwa vigumu kidogo na badala yake huamua kutafuta mahali pa kuazima au kukodisha kwa muda fulani tu, na ndipo sasa utakuta wenye biashara hizi wanapata fedha nyingi na baada ya kipindi kifupi mitaji waliyotumia kununulia mitambo na vifaa husika hurudi halafu kinachofuata hapo ni faida kubwa. Unaweza ukaazimisha watu binafsi, vilevile hata makampuni.





5.  HUDUMA ZA KIAFYA.    
Katika Biashara hizi, kuna huduma mbalimbali mfano; Huduma za matibabu ya meno, Matabibu wanaotumia mimea na miti shamba, vituo vya mazoezi ya viungo kwa waliovunjika na wenye matatizo ya misuli, vituo binafsi vya afya na zahanati, huduma za ushauri wa kiafya nk. Kama ilivyo kwa huduma zingine zilizotangulia, linapokuja suala la afya, halina mjadala kabisa kwani, hata ikiwa mtu hana senti tano mfukoni lakini mbele ya kupona atafanya kila linalowezekana ili mradi tu amepata fedha kwa ajili ya matibabu.

6.  BIASHARA YA UZALISHAJI NA USAMBAZAJI WA NISHATI HUSUSANI ILE YA UMEME.
Gharama za awali zaweza kuwa kubwa kidogo lakini ni biashara itakayozalisha faida kubwa na endelevu kwa kipindi kirefu kitakachofuata kwani nishati hasa ya umeme ni hitaji la msingi na ambalo mtu atahitaji kila siku, ni kama vile ilivyokuwa chakula. Nishati ya umeme yaweza kuzalishwa kutokana na vyanzo mbalimbali kama vile; maporomoko ya maji ya mito, upepo, gesi, mafuta, jua(solar), “geothermal-energy(maji ya moto kutoka katika miamba ardhini)”, mawimbi ya bahari na nishati ya nyuklia(atomic energy).

7.  KUBUNI, KUDIZAINI NA KUCHORA ALAMA, NEMBO(LOGO) MBALIMBALI ZA BIASHARA NA MAKAMPUNI.
Kila biashara/kampuni huhitaji huduma hizi kuanzia kutengenezewa matangazo, mabango, kuandaa hati za usajili wa shughuli mbalimbali (mfano makampuni & Ngos), kutengeneza kurasa za magazeti, tovuti na blogs(graphics design), kudizaini na kuchora ramani za majengo, kudizaini michoro ya bidhaa mbalimbali za viwandani nk. Sehemu kubwa ya gharama katika shughuli zote hizi ni muda wako tu endapo tayari ujuzi unao pamoja na fedha kidogo za kununulia kompyuta ya mezani au ile ya kupakata “laptop”.

8.  TAASISI NA MASHIRIKA YA KIDINI.
Dhana kuwa mashirika ya kidini hayapo kwa ajili ya kutengeneza faida(non profit organization), haimaanishi kwamaba hayalengi kutengeneza faida kabisa bali kinachotazamwa zaidi ni kwa namna gani faida inayopatikana inavyotumika. Kwa mfano badala ya faida kugawiwa kwa wamiliki(wanahisa au waanzilishi) kama ilivyokuwa kwa makampuni ya kibiashara, faida hiyo inapaswa kuelekezwa  katika kuendeleza  na kukuza zaidi dhamira(mission) ya taasisi husika. Taasisi na Mashirika hayo huhusisha siyo tu Misikiti na Makanisa bali pia na taasisi zilizokuwa chini yake mfano, mashule, vyuo, vyuo vikuu, mahospitali na vituo vya afya.

…………………………………………………………………..

*Mpenzi  msomaji wa makala hii, kama ulikuwa hujasoma kitabu tulichokuandalia bure bila malipo cha “KANUNI YA KUJIFUNZA ELIMU YA PESA NA MAFANIKIO KWA UFANISI” basi, jiunge na blogu hii kwa kuweka e-mail yako, majina na namba ya simu katika fomu iliyopo mwanzoni mwa blogu upande wako wa kulia au mwishoni mwa makala hii iitwayo “KWANINI VITABU NA SEMINA ZA ELIMU YA PESA NA MAFANIKIO HAVIWASAIDII WATU WENGI?.”

Fuata maelekezo ikiwa ni pamoja na kufungua email yako hiyo na kisha uthibitishe kukubali kutumiwa kitabu pamoja na zawadi nyinginezo zitakazoambatanishwa nacho halafu utaweza kukipakua(download). Ikiwa tafadhali utapata ugumu kukipakua kitabu hicho aidha kwa kushindwa kujiunga ama kikwazo kingine chochote kile basi naomba tujulishe kupitia meseji au email, jifunzeujasiriamali@gmail,com

Pia vitabu vyetu vingine vyote vya kulipia vipo, ikiwa utahitaji kitabu chochote kile kimojawapo basi wasiliana na sisi kwa namba 0712 202244 au 0765 553030 na tutakutumia popote pale ulipo mikoani au kama upo hapa Dar es saam pia tuwasiliane.

Vitabu vyetu vyote vipo katika mfumo wa vitabu vya karatasi,(hardcopy) pamoja na mfumo wa kielektroniki (softcopy)“MIFEREJI 7 YA PESA”, “SIRI YA BIASHARA ZA REJAREJA” na MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI. Kwa maelezo zaidi tembelea ukurasa huu,  > >SMARTBOOKSTANZANIA


TUPO MBEZI KWA MSUGURI KARIBU KABISA NA KITUO CHA DALADALA, NI KITUO CHA PILI KUTOKA MBEZI MWISHO KAMA UNARUDI KIMARA TERMINAL.

0712 202244   &  0765 553030
jifunzeujasiriamali@gmail.com

11 Responses to "UNAJUA BIASHARA YENYE FAIDA KUBWA NA YA HARAKA MARA 2 YA MTAJI UTAKAOWEKEZA?"

  1. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete
  2. Comment tunazikaribisha kwa mikono miwili lakini siyo tangazo la biashara kama mwenzetu huyu alivyoliweka, bora basi angeanza kiubunifu kidogo hata kwa kuzungumzia kwanza post husika.

    ReplyDelete
  3. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete
  4. Unapataje mkopo au hatua zakufuata ni zipi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mikopo ukienda katika taasisi nyingi za fedha ikiwemo Mabenki kila moja ina utaratibu wake lakini mambo ya msingi wanayoangalia zaidi bila kujali umeenda benki au taasisi ipi ni, kwanza uwe na biashara ambayo tayari ulishaianzisha na inafanya kaz, Pili ni lazima uwe na dhamana, dhamana inaweza kuwa ni mali au mtu/watu wengine wanaoaminika. Tatu uwe unakopesheka isijekuwa umekimbia madeni kwingine au huna makazi maalumu na eneo unakofanyia biashara na Nne uwe unatambulika rasmi na serikali ya mtaa unakoishi

      Delete