NASHUKURU KITENDAWILI CHA MTEJA WETU WA MANZESE TIP TOP KIMETEGUKA | JIFUNZE UJASIRIAMALI

NASHUKURU KITENDAWILI CHA MTEJA WETU WA MANZESE TIP TOP KIMETEGUKA

Jana baada ya kukumbwa na mkasa wa kuibiwa simu,mwakilishi wetu maeneo ya Magomeni usalama,  kitendo “kilichopelekea” kupotea kwa namba ya mteja tuliyekuwa tukimpelekea kitabu alichokuwa ametuagiza, nikalazimika kuweka ujumbe hapa katika blogu ili angalao kama mteja huyo atasoma atambue kilichotusibu, hatimaye leo majira ya saa nane za mchana tumefanikiwa kumfikishia kitabu hicho maeneo ya Kidongochekundu Mnazimmoja.

Kumbe ni mfanyabiashara mkoani Mbeya aliyefika  kuchukua bidhaa zake jiini na aliposoma tangazo letu akaagiza kitabu, ratiba yake ilikuwa finyu kiasi kwamba hata leo ingepita basi tusingeliweza kumpata tena kwani hata hivyo kitabu tulimpelekea maeneo ya Kidongochekundu alikokuwa akifunga mizigo yake tayari kwa kusafirisha kuelekea Mkoani Mbeya baada ya kuwasiliana tena  na sisi leo asubuhi. Bila shaka Manzese Tip top patakuwa ndipo sehemu aliposhukia kutimiza  hayo malengo yake ya kibiashara.

Sote tulifurahi baada ya kuonana  ingawa kidogo alisema kwa utani, “ mimi nilidhani nyie ni wahuni, mnaweka matangazo na kisha vitabu vyenyewe havionekani” badaye nilimulewesha kwa kina yaiyokuwa yametokea, ikiwa ni pamoja na kumtaka radhi basi kila kitu kikawa sawasawa.

0 Response to "NASHUKURU KITENDAWILI CHA MTEJA WETU WA MANZESE TIP TOP KIMETEGUKA"

Post a Comment