KITABU CHA MPANGO WA BIASHARA | JIFUNZE UJASIRIAMALI

KITABU CHA MPANGO WA BIASHARA

Kwa wiki kadhaa sasa baadhi ya wateja wetu wapendwa mlikuwa mkitupigia simu, na wengine kufika kwa mawakala wetu mkihitaji kununua kitabu cha namna ya kuandaa mipango ya biashara ambacho pia kina masomo mengine yote ya ujasiriamali ikiwemo namna ya kuanzisha kampuni au biashara na kuiendeleza mpaka unafanikiwa.

Nakala za vitabu vilivyokuwa vimechapishwa awali vilikuwa vimemalizika lakini wiki ijayo kuanzia Jumatatu ya tarehe 17/12/2015, vitakuwa tayari vimekwishachapwa vingine, hivyo tunawajulisha wateja wetu wote mliokuwa mmeweka oda ya vitabu na wale pia ambao mlikuwa mnahitaji vitabu hivyo kuwa sasa vinapatikana kwa wakala wetu mkuu Buguruni. Unaweza ukawasiliana kwa simu na namba hizi; “07 12 202244”  au “0765 553030”

Kitabu cha mpango wa biashara.

Kwa wale ambao ratiba zao ni ‘tight’ sana na wangehitaji vitabu tumeanzisha huduma sasa ya kuwaletea vitabu mpaka pale walipo, kinachotakiwa tu ni wewe kuwasiliana na sisi na kutujulisha iwapo unahitaji kitabu/vitabu lakini muda wa kuja kununua ni mdogo. Huduma hiyo ni kwa wale wateja wa Dar es salaam tu.

Kwa wateja wa Mikoani, tunawatumia kwa njia ya mabasi bila shida yeyote, tumeshawahi kuwatumia watu wengi mpaka sasa, tunao uzoefu wa kutosha. Cha kufanya kama upo mkoani, wasiliana na sisi tujue ni basi gani linalofika pale ulipo na baada ya hapo ukishatuma malipo, moja kwa moja tunakutumia kitabu/vitabu na hufika kwa asilimia 100% na hata kama itatokea (haijawahi kutokea mpaka sasa) hitilafu yeyote mfano kitabu kupotea, au kuharibika na mvua nk. Tunawajibika kwa kurudisha pesa au kutuma kitabu kingine upya.

0 Response to "KITABU CHA MPANGO WA BIASHARA "

Post a Comment