HATUA 10 ZA KUANZISHA BIASHARA YA REJAREJA (DUKA) | JIFUNZE UJASIRIAMALI

HATUA 10 ZA KUANZISHA BIASHARA YA REJAREJA (DUKA)

duka zuri la vyakula rejareja
SEHEMU YA 1
Ndoto za kuanzisha biashara ya rejareja hususani duka zinaweza kuwa kweli haraka na kwa urahisi zaidi endapo mtu atafuata taratibu hizi pamoja na kufanya maandalizi ya kutosha ikiwa ni pamoja na kuandaa mpango kamili (mchanganuo) wa biashara yake iwe ni katika karatasi ama kichwani mwake.

1.  Chagua mfumo wa bishara kisheria
Kuchagua mfumo wa biashara yako kisheria ni uamuzi wa msingi kabisa kabla ya kuanza bishara, kwani kuja kubadili baadaye ni jambo la ghrama na usumbufu mkubwa.

Mifumo ya biashara kisheria ipo ya aina tatu;
(a)        Biashara ya mtu bianafsi.
(b)        Biashara ya ubia.
(c)        Biashara ya kampuni yenye dhima ya ukomo (Limited company)
Biashara nyingi za rejareja hasa zile ndogo ndogo wanatumia sana mfumo huu wa  biashara ya mtu mmoja au binafsi. Faida na harasa za mifumo  yote 3 imefafanuliwa kwa undani sana katika vitabu mbalimbali kikiwemo kitabu kikubwa “Jifunze Michanganuo ya Biashara na Ujasiriamali”

2. Chagua jina la biashara yako.
Unaweza ukawa na mpango mzuri sana wa biashara yako ya rejareja lakini ukaipa jina lisilofaa ukawa umeharibu kila kitu. Kuipa biashara jina ni hatua muhimu sana ingawa unaweza kuona ni kazi nyepesi tu kufanya hivyo. Ni kazi inayohitaji ufikirie kwa umakini mkubwa, unapotaka kuipa biashara yako ya rejareja jina linalofaa  zingatia vipengele hivi hapa chini;

·       Orodhesha  kwenye karatasi  bidhaa ama huduma unazotoa, maneno yote yanayohusiana na biashara unayotarajia kuifanya pamoja na mazingira na eneo itakapokuwa.
·       Fanya utafiti kwa kuangalia majina ya biashara kama ya kwako zilizokuzunguka, unanweza pia ukatazama kwenye mtandao wa intanet n.k mpaka utakapopata jina utakaliona unaridhika nalo.

    Jina linapaswa liwe;
ü Rahisi kueleweka kimatamshi na kimaandishi.
ü Usichague jina lenye mlengo hasi mfano mmoja ni  café moja jamaa alitumia jina linalokashifu timu fulani ya mpira.
ü Usichague jina litakalopotosha watu wala lenye maana zaidi ya moja.
ü Zingatia herufi jina la biashara yako litakapoanguakia kwenye orodha kama za yellow page n.k.
ü Chagua jina litakalowakilisha kile kitu hasa utakachofanya na siyo litakalominya baadhi ya shughuli zako.
ü Chagua jina utakalojivunia na siyo litakalokufanya uone aibu hata kuliwakilisha mbela za watu.
ü Usitumie majina ya jumla yanayowakilisha vitu jumla mfano; Nafuuu store, Bei rahisi duka n.k. majina kama hayo ni vigumu kuyasajili kama alama yako ya biashara.

Baada  ya kupata jina la biashara yako,  jaribu kuuliza watu wa karibu ikiwa  nao kama watalipenda. Wakiona linafaa basi lipitishe, ukiona wengi wamelitilia mashaka unaweza  ukarudi tena kwenye orodha yako upya.

3.  Ipe  biashara yako namba ya Utambulisho wa mlipa kodi TIN
Ni vizuri  ukaenda kuisajili biashara yako mamlaka ya mapato “TRA” tawi lililopo karibuni na wewe wakupe namba ya mlipa kodi (TIN). Hatua hii hulipi gharama yeyote, ni bure. Baada ya kujaza fomu zao wanakupa hati na  kukufungulia faili ambalo baadae ndilo huja kulitumia utakapokwenda kulipa kodi ya mapato. Ikiwa biashara yako ni ndogo sana unaweza ukaianza hivyo hivyo tu bila TIN lakini baadae ukaja kujisajili.

4. Uchaguzi wa  ni bidhaa gani utakazouza.       
Kwa biashara ya duka la rejareja la mtaani hakuna ukomo wa bidhaa unazotakiwa kuuza. Cha kuzingatia hapa ni kuangalia katika utafiti wako uliofanya ni bidhaa zipi unaona wakazi wa eneo husika wanapendelea zaidi kununua.

Vigezo vingine ni pamoja na faida, angalia ni bidhaa zipi zenye faida kubwa kwa mfano aina fulani ya maji yanaweza kuwa yananunuliwa kwa wingi sana lakini faida yake ni kidogo mno. Hivyo ni juu yako kuamua upate faida kidogo uuze sana au faida kubwa lakini mauzo kidogo.

Angalia pia bidha zinazoendana na wakati uliopo, ushindani: ukichagua bidhaa za kipekee unaweza ukashindana hata na biashara kubwa kubwa.

Katika vitu muhimu sana unavyopaswa kufanya kabla haujaanzisha duka lako ni kuandaa mpango kamili wa biashara, mpango unaweza kuwa upo kichwani mwako tayari lakini ni vizuri zaidi ukauandika katika karatasi hata kama  hautafuata taratibu rasmi za kuandika, unaweza tu ukaorodhesha mambo yako yote muhimu unayotarajia kuyafanya ili kukamilisha malengo ya biashara yako pamoja na gharama utakazotumia, pia faida au mauzo unayotarajia kwa siku, mwezi au mwaka, na tayari huo unatosha kuitwa mpango wa baishara yako.
dada muuza duka la vyakula mtaani.
Mwanamke akiuza duka la rejareja.
Ni kama vile unapotoka nyumbani kwenda sokoni kununua vitu vya nyumbani, unaorodhesha vitu vyote unavyotarajia kwenda kununua kwenye karatasi pamoja na bajeti ya fedha utakazotumia. Michanganuo ya biashara kwa undani zaidi pamoja na mifano yake hai imefafanuliwa katika kitabu  “Jifunze Michanganuo ya Biashara na Ujasiriamali”

6. Fahamu sheria na taratibu za mamlaka husika.
Watu wengi baaba ya kufungua maduka yao miezi miwli, mitatu hushangaa kuona afisa biashara anakuja  na kudai vitu kama leseni, au watu wa mamlaka ya mapato TRA wakidai TIN namba, wakati mwingine huja watu wa Halmashauri au serikali za mitaa na kudai leseni za kuuza vileo ama uwaonyesha sehemu ya wateja kujisaidia (choo) ikiwa biashara ni grosari  au mkahawa. Na wakati mwingine huja hata matapeli wajanja tu wa mjini kukutisha wakijua kabisa hukufuata taratibu za vibali ili uwape hongo ya pesa.

Usihatarishe biashara yako uliyoilipia pango fedha nyingi na kupoteza muda wako wa thamani, hakikisha unafuata taratibu zote hasa kupata vibali kama TIN namba, leseni kutoka ofisi ya serikali ya mtaa wako au manispaa na vibali vinginevyo ikiwa  ni biashara kwa mfano kama ya kuuza madawa ya binadamu itabidi uende mamlaka ya chakula na dawa TFDA.

hatua 10 za kufungua duka
Duka la rejareja la vyakula.


2 Responses to "HATUA 10 ZA KUANZISHA BIASHARA YA REJAREJA (DUKA) "