DR. SLAA: LOWASSA HAKUWA ASSETI ALIKUWA LIABILITY(MZIGO) | JIFUNZE UJASIRIAMALI

DR. SLAA: LOWASSA HAKUWA ASSETI ALIKUWA LIABILITY(MZIGO)

Aliyekuwa katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na maendeleo Dr. Willbroad Slaa Leo hii ameibuka katika kikao na waandishi wa habari na kutolea ufafanuzi wa ni kwanini aliamua kujiuzulu uongozi katika chama chake baada ya aliyekuwa waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa kuhamia katika chama hicho kisha kupewa nafasi ya kugombea uraisi.

Akimlinganisha Lowassa na mbia wa biashara alisema kuwa katika biashara yeyote ile hata kama ni ya ufugaji wa kuku unapomkaribisha mtu ni lazima uhakikishe kuwa yule utakayemkaribisha ni lazima awe asseti yaani rasilimali na si Liability au ‘mzigo’. Amesema unaweza kuwa na mtaji wako wa kuku 200 ulioudunduliza kwa jasho kwa muda mrefu, sasa unapoamua kumkaribisha mbia, angalao basi aje na hata na mtaji wa kakuku kamoja. 

Lakini anasema baada ya kuchunguza katika hatua zile za kumkaribisha Lowassa alibaini hakuwa na majina yeyote ya wabunge aliokuwa amedai anahama nao CCM, bali alikuwa tu na namba ya watu. Kwa maana hiyo amesema Lowassa hakuwa mtaji bali hasara au mzigo kwa kuwa hakuwa na mtaji wa watu wengi kama ilivyokuwa imedhaniwa.

Alisema yeye siasa ya ulaghai haitaki ndiyo maana aliamua kujiondoa kwenye siasa. Dhana kwamba Chadema wanataka waiondoe kwanza CCM madarakani pasipokuwa hata na programu inayoeleweka huku wakitumia watu wale wale ni kujidanganya, ni upuuzi. Alisema ni afadhali apotee katia ramani ya siasa Duniani kuliko kuikana dhamira yake.

Alimalizia kwa kusema kuwa kama Taifa tuna kazi kubwa ya kuchambua na ukishaumwa na nyoka, usirudie tena kuumwa na nyoka akimaanisha kuwa kipindi kinachomalizika wananchi waliahidiwa maisha bora na sasa hawajayapata. Pia aliwaasa waandishi wa habari kufanya utafiti wa kutosha kabla ya kuandika habari zao. Amesema kwamba yeye amestaafu siasa, na hana chama chochote, ataendelea kuwatumikia wananchi wanyonge akisimamia misingi ya ukweli.

Awali wakati Mheshimiwa Edward Lowassa alipokuwa akihamia katika chama cha demokrasia na maendeleo Chadema, kulitokea mtikisiko mkubwa baada ya Dr. Wilbroad Slaa na Profesa Ibrahimu Lipumba wa chama cha CUF kuamua kujiuzulu nafasi zao katika vyama vyao chini ya muavuli wa umoja wa vyama vya upinzani uitwao Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA)



0 Response to "DR. SLAA: LOWASSA HAKUWA ASSETI ALIKUWA LIABILITY(MZIGO)"

Post a Comment