KONGAMANO LA UJASIRIAMALI KENYA NA UJIO WA BARACK OBAMA | JIFUNZE UJASIRIAMALI

KONGAMANO LA UJASIRIAMALI KENYA NA UJIO WA BARACK OBAMA

Wakenya wakiwa wanasubiri ujio wa ndugu yao Barack Obama na ambaye pia nia Rais wa Taifa kubwa Duniani  Marekani, tayari shamra shamra hizo zimekwishaanza jijini Nairobi  kwa Kongamano la Ujasiriamali la Dunia (GES), ambapo wajasiriamali na wafanyabiashara mbalimbali wamekwisha anza kuziweka bidhaa zao tayari kwa ajili ya kuonyeshwa kwa wageni mbalimbali watakaoambatana na ugeni huo mkubwa ikiwa ni pamoja na wajasiriamali kutoka maeneo mbalimbali Duniani.

Maandalizi ya kongamano la ujasiriamali la Dunia(GES) na ujio wa Rais Barack Obama Kenya sasa yameiva.

Lengo kuu la kongamano hilo lililoasisiwa na Marekani chini ya utawala wa Obama hapo mwaka 2010 ni kuendeleza na kuchochea zaidi ujasiriamali kote Duniani. Nchini Kenya litafanyika Julai 25 mpaka 26 likiwa ni la sita likikusanya wajasiriamali wa ngazi zote kutoka kote duniani, wakiwamo, viongozi wa makampuni, wawekezaji, mamilionea, watoamisaada, na maafisa wakuu wa serikali.

UMUHIMU WAKE.
Kongamano hili ni fursa kubwa kwa wajasiriamali wa Kenya, Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla kuweza kukutana ana kwa ana na wawekezaji na wajasiriamali wakubwa wa Dunia waliokuwa na uzoefu mkubwa katika maswala mbalimbali ya ujasiriamali na uwekezaji kwa ujumla.

Ni kama linavyofanyika kombe la Dunia vile, kongamano hili pia litachochea biashara, uwekezaji kwa mabilioni ya dola, kukuza utalii pamoja na utamaduni. “Tunataka kuwekeza na kuzisaidia kampuni ndogo za kiafrika  ziweze kuwa kubwa katika sekta ya nishati”  anasema Larry Page mwanzilishi wa mtandao wa Google. Katika kongamano hilo Rais Obama mwenyewe atahutubia pamoja na wageni wengine. 

0 Response to "KONGAMANO LA UJASIRIAMALI KENYA NA UJIO WA BARACK OBAMA"

Post a Comment