DAWA MPYA YA MALARIA YAGUNDULIWA NA WANASAYANSI | JIFUNZE UJASIRIAMALI

DAWA MPYA YA MALARIA YAGUNDULIWA NA WANASAYANSI

Watafiti katika Chuo kikuu cha Dundee nchini Scotland wamegundua dawa mpya yenye uwezo wa kutibu malaria na wakati huohuo pia ikiwa na uwezo wa kuzuia watu wasiambukizwe kwa kutumia dozi moja pekee. Dawa hiyo, inayojulikana kitaalamu kama DDD107498” imetengenezwa  na  kitengo  cha madawa cha chuo kikuu hicho pamoja na taasisi nyingine iitwayo “Medicines for Malaria Venture”


Wanasayansi, wagunduzi hao wakiwa kazini.
Wanasayansi walisema  dawa hiyo mpya “ya kushangaza”  inauwezo wa kufanya kazi vizuri dhidi ya vimelea wa malaria ambao kwa sasa wameonyesha usugu kwa dawa nyingine zilizokuwepo. Ina uwezo wa kufanya kazi kwa njia  tofauti  kabisa na dawa nyingine za malaria zilizoposokoni na hivyo kuwa na uwezekano mkubwa wa kukabiliana na tatizo la usugu wa dawa zilizopo kwa wadudu wa malaria.
Maelezo kwa kina kuhusiana na dawa hiyo yamechapishwa katika jarida la kisayansi la “Journal Nature”



Dr. Keavin Read, kiongozi mwenza katika mradi huo alisema kwamba dawa hiyo inahitajika haraka, kwani  usugu wa dawa zilizokuwepo sasa umekuwa tishio la kweli. Aliongeza kuwa  Malaria inaendelea kuhatarisha  karibu nusu ya idadi yote ya watu Duniani na ambayo pia ndiyo  isiyokuwa na uwezo wa kumudu gharama za kuutibu.

Chanzo cha habari hii ni BBC

0 Response to "DAWA MPYA YA MALARIA YAGUNDULIWA NA WANASAYANSI"

Post a Comment