SANAA NI AJIRA NA FURSA NZURI KWA VIJANA WAKIJITUMA | JIFUNZE UJASIRIAMALI

SANAA NI AJIRA NA FURSA NZURI KWA VIJANA WAKIJITUMA

Sanaa na hasa hasa katika nyanja za muziki na uigizaji hapa nchini imedhihirika wazi kwamba ni fursa nzuri ya ajira kwa vijana endapo watajituma  kwa nguvu zao zote, mifano ipo mingi tu, kuna wasanii wakubwa na wadogo, wote kazi zao zinathibitisha kauli hii. Mfano wa wasanii hao ni Jefryder, msanii ambaye tangu anaanza kazi zake za muziki  mpaka hivi leo blogu hii imekuwa ikifuatilia na kuandika habari zake.
 
Jefryder akiwa na wenzake
Jefryder kwa jina lake halisi Jafary  Ahmed, amewahi kutamba na nyimbo kadhaa nzuri zikiwamo, NIPE  LOVE na NIPE  MIC  ambazo aliwashirikisha wenzake, Darasa & Steve RNB,  pamoja na  Nester & Mack Jeans. Sasa hivi Jef ameipua video ya wimbo wake mpya unaoitwa MIPANGO IMEBUMA, aliomshirikisha Gitaa.

Hebu itazame Mipango imebuma hapa


Video hiyo ambayo ndani anaonekana kimwana, mshindi wa shindano la Manywele Kigoli mwaka 2013 ‘Suzie’ imekonga nyoyo za watu wengi waliobahatika kuiona kiasi cha kutokuamini kama imeshutiwa hapa Bongo, “Jefryde atakuwa vipande vingine ameshuti Bondeni kwa mzee Zuma siyo bure..” alisikika kijana mmoja akisema alipokuwa akiitazama kwa mara ya kwanza katika saluni moja ya Dread maeneo ya Y2K Buguruni.  

0 Response to "SANAA NI AJIRA NA FURSA NZURI KWA VIJANA WAKIJITUMA"

Post a Comment