DIAMOND PLUTNUMZ: KILA JAMBO LINAWEZEKANA ENDAPO MTU AKIAMUA KUJISHUGHULISHA | JIFUNZE UJASIRIAMALI

DIAMOND PLUTNUMZ: KILA JAMBO LINAWEZEKANA ENDAPO MTU AKIAMUA KUJISHUGHULISHA

Diamond: Tandale akifanya vitu vyake
Mkurugenzi wa Global publishers, Eric Shigongo akizungumza ktk semina hiyo
Eric Shigongo pamoja na wanasemina katika picha

SEMINA ya Ujasiriamali iliyokuwa ikifanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Tandale, jijini Dar es Salaam, kwa muda siku nne,  ilihitimishwa kwa shamra baada ya mwanamuziki wa  Bongo Fleva,  Nasib Abdul Diamond, kutoa burudani ya muziki na kuongea na wakazi wa eneo hilo.

Katika semina hiyo  ilianza Aprili Mosi na kuhitimishwa Aprili 4 mwaka huu ambapo wataalam wa ujasiriamali Eric Shigongo, James Mwang’amba, Dr. Didas Lunyungu na Hassan Ngoma, walitoa mafunzo ya ujasiriamali na namna mtu anavyoweza kujitoa katika umaskini na kupata mafanikio maishani.
Naye Diamond,  alizungumzia jinsi maisha yake yalivyoanzia hapo Tandale na baadaye kuwa ya mafanikio kutokana na juhudi zake anazoendelea kuzifanya katika muziki, hivyo akawataka wakazi wa Tandale kutokukata tamaa.
‘’Nashukuru sana kwa semina hiyo mliyoipata kutoka kwa Eric Shigongo, ambapo mkiifanyia kazi mtaweza kunufaika na kuwaletea maendeleo maana mimi mwenyewe nimetokea Tandale hivyo nitaendelea kuwatia moyo kuwa kila jambo linawezekana endapo mtu akiamua kujishughulisha,’’ alisema Diamond.

(HABARI/PICHA: DENIS MTIMA/GPL)

0 Response to "DIAMOND PLUTNUMZ: KILA JAMBO LINAWEZEKANA ENDAPO MTU AKIAMUA KUJISHUGHULISHA "

Post a Comment