SOKA LAIVU BRAZILI LEO: MPAKA HALF TIME BRAZILI NA MEXICO BADO NGOMA DROO | JIFUNZE UJASIRIAMALI

SOKA LAIVU BRAZILI LEO: MPAKA HALF TIME BRAZILI NA MEXICO BADO NGOMA DROO



Hakuna aliyeweza kuliona lango la mwenzake, mpaka timu zote mbili Cameroon na Mexico wanakwenda mapumziko, hali hii imeendelea kuwa hivyo huku kila mmoja akijitahidi kuliona lango la mwenzake bila ya mafanikio. Iwapo Cameroon itatoka sare basi angalao itakuwa na nafuu kidogo kulioko kushindwa. Mechi nyingine inatarajiwa kuchezwa leo hii saa nne usiku baina ya Uhispania na Uholanzi. Dakika ya 57 kidogo Cameroon ijipatie goli lakini ikawa kona.


Mexico wanajipatia bao dakika ya 61 Oribe alipiga mpira kipa wa Cameroon alipourudisha ukapigwa tena na bao likajaa wavuni. Sasa Cameroon wanakuwa na kibarua kikubwa kuona ni jinsi gani watakavyorudisha goli hili. Eso Okoto anaangushwa chini na mpira unapigwa kuelekea lango la Mexico, anagaagaa chini lakini refarii wala hajali kitu, mpira unaendelea. Cameroon kama ilivyokuwa kwa timu nyingi za kiafrika wamekuja kwenye haya mashindano wakiwa na "mzigo mzito mgongoni" mizigo ya migogoro ndani ya timu na club zao nyumbani. Pengine hata ndiyo sababu ya kutokufanya vizuri kila mara.

Mpaka kipenga cha mwisho kinapulizwa, mechi hii ya pili kundi A timu ya Cameroon inatoka kichwa chini huku Mexico ikitoka kifua mbele kwa bao 3 kwa 0.

0 Response to "SOKA LAIVU BRAZILI LEO: MPAKA HALF TIME BRAZILI NA MEXICO BADO NGOMA DROO"

Post a Comment