MISAMAHA YA KODI YAFUTWA NA WAZIRI WA FEDHA, SAADA MKUYA SALUM | JIFUNZE UJASIRIAMALI

MISAMAHA YA KODI YAFUTWA NA WAZIRI WA FEDHA, SAADA MKUYA SALUM

Aklisoma bajeti ya mwaka 2014/2015 Bungeni, Waziri wa fedha Saada Mkuya Salum amesema kwamba misamaha mbalimbali ya kodi ikiwemo msamaha wa kodi kwa makampuni ya michezo ya kubahatisha pamoja kodi ya zuio kwenye ukodishaji wa  ndege kwa walipakodi wasio wakazi yaani non resident na hatua hii inalenga katika kupunguza misamaha ya kodi na hivyo  kuiongezea mapato serikali.

Aidha waziri wa fedha alisema kwamba, serikali itatoa unafuu kwa wafanyakazi kwa kupunguza kiwango cha chini cha kutoza kodi ya mapato ya ajira 'payee' kutoka asilimia 13% ya sasa hadi asilimia 12% na amesema serikali itaendelea kuangalia uwezekano wa kuendelea kupunguza kiwngo hiki hatua kwa hatua ili kuwapa nafuu wafanyakazi.
WAZIRI WA FEDHA SAADA MKUYA SALUM
Kwa upande wa wafanyabiashara wadogo wadogo wanaozidi mauzo ya shilingi milioni nne kwa mwaka lakini wasiozidi milioni 7 na nusu kwa mwaka kiwango cha kutozwa kodi kwenye mapato hasi kimeongezwa kutoka asilimia 2% hadi asilimia 4% kwa wale wanaoweka kumbukumbu za mauzo na kutoka sh. laki moja hadi sh. laki 2 kwa wale wasiokuwa na kumbukumbu za mauzo. Lengo lake ni kuongeza mapato ya serikali kwa shilingi bilioni 31 na mia tano na nne.

Msikilize ‘live’ waziri wa fedha Mheshimiwa Bi Saada Mkuya Salum akisoma bajeti hiyo  ya serikali kwa mwaka 2014/2015 Bungeni mjini Dodoma leo. 

0 Response to "MISAMAHA YA KODI YAFUTWA NA WAZIRI WA FEDHA, SAADA MKUYA SALUM "

Post a Comment