‘WEMA SEPETU’ AFUNGUA KAMPUNI YA KITAPELI DAR KUJIPATIA MAMILIONI YA PESA. | JIFUNZE UJASIRIAMALI

‘WEMA SEPETU’ AFUNGUA KAMPUNI YA KITAPELI DAR KUJIPATIA MAMILIONI YA PESA.

Imedaiwa kwamba mrembo, muigizaji nyota nchini Tanzania Wema Sepetu ameanzisha taasisi, ya kitapeli inayojihusisha na utoaji mikopo.Taasisi hiyo kwa jina ‘Saving Foundation Loans’, tayari imelalamikiwa na watu kadhaa kwamba imeshawaingiza mjini kwa kuwaahidi kuwapa mikopo ndani ya dakika 45 lakini ikadhihirika kuwa ni kinyume chake baada ya wahusika kuona kimya hata pale walipokamilisha taratibu zote ikiwa ni pamoja na kujaza fomu kwenye mtandao pamoja na kutuma kiasi cha fedha kupitia mitandao ya namba za simu walizoziweka hapo kwenye tovuti yao.

Akizungumza na Wapo Radio FM kupitia kipindi chake maarufu cha Patapata mmoja wa wahanga hao alisema kwamba tayari amekwisha fikisha taarifa hizo polisi na wameahidi kulifuatilia suala hilo kupitia kitengo chake cha kuzuia uhalifu wa kwenye mitandao “Cyber crime investigation”. WAPO Fm ilipofanya jitihada za kutaka kupata ukweli ikiwa kama kweli mkurugenzi wa taasisi hiyo ni huyu huyu Wema Sepetu tunayemfahamu hatimaye ilibaini ya kwamba siyo kweli, matapeli hao kwa kumtumia msichana aliyeigiza sauti kama ya Wema ndiye anayepokea simu na kujitambulisha kwa wasiwasi kuwa ni Wema Sepetu.

Hata namba wanayoitumia nayo imesajiliwa kwa jina la Wema Sepetu. Mwandishi alipombana kwa maswali aeleze ofisi zilipo na iwapo angeweza kuonana naye ana kwa ana Wema sepetu huyo feki alibabaisha babaisha na kusema “Usinichoshe na maswali” akakata simu na kuingia mitini.

Wapo haikuishia hapo ikamtwangia Wema Sepetu Original, Wema alikana kuhusika na kampuni hiyo akasema kwanza yeye hata kwenye face book yenyewe tangu mwaka jana amesitisha kwa hivyo mtu yeyote asijetapeliwa huko kwa imani kuwa kampuni ni ya Wema sepetu, amewaasa watu kuwafikisha katika vyombo vya sheria matapeli hao wanaotumia jina lake kutaka kujitajirisha bila jasho.

Katika mtandao wao hao ‘Saving Foundation Loans’ wamezuga kwa kujifanya kuwa wao wako “powered by Tanzanian Government sponsored by Tigo (MIC TANZANIA) Registered by TRA (Tanzania Revenue Authority)” Halafu kwenye mawasiliano wanadai eti ofisi zao zinatazamana na Ikulu katika “jengo kuu la Utumishi wa Umma kitengo cha mikopo na uwekezaji jengo namba 360 ghorofa namba moja ofisi ya Customer Service fund”. Taasisi hii pia inafanana na taasisi nyingine inayojiita nayo, “Jakaya Foundation” ambayo tovuti yake inashabihiana sana na hii ya kwao.
 
Watu mana-aswa wanapo ‘google’ kwenye mtandao kuwa makini sana na taarifa mbalimbali wanazokutana nazo huko ikiwa ni kama hizi zinazosababisha kuibiwa au hata uhalifu mwingine wowote ule, kwani siku hizi wahalifu wamekuwa wengi katika mitandao hiyo wakisaka pesa.


0 Response to "‘WEMA SEPETU’ AFUNGUA KAMPUNI YA KITAPELI DAR KUJIPATIA MAMILIONI YA PESA."

Post a Comment