……TEMBA NA CHEGE MKIONA KITU GANI…...SISI, CHAPA NYINGINE……TMK MKIONA KITU GANI…. | JIFUNZE UJASIRIAMALI

……TEMBA NA CHEGE MKIONA KITU GANI…...SISI, CHAPA NYINGINE……TMK MKIONA KITU GANI….



Hayo ni baadhi tu ya maneno katika mashairi ya wimbo “Chapa nyingine” wa Chege ft Gift. Kila aliyeusikiliza wimbo huu hakusita kusifia kukunwa MNO! na kipande hicho anachoimba huyo mwana dada, “….TMK mkiona kitugani…..”

Kwa hakika unaposikiliza audio ama kuangalia video ya wimbo huu wa Chege, “CHAPA NYINGINE” aliomshirikisha Gift hautaweza kujizuia angalao kucheza kidogo hata ikiwa wewe siyo mpenzi kabisa wa muziki, ni ngoma kali, inayodhihirisha ukongwe wa mwanamuziki huyu aliyewahi kuimba pia kibao kilichopendwa sana cha “Tukutane Uswazi Tekawey”

Huu ndio ubunifu unaotakiwa kuigwa na wajasiriamali wengine wote wa muziki wa kizazi kipya ikiwa wanataka kweli kazi zao kuvutia mashabiki wengi wa muziki huo. Chege hakufikia hapa alipo kiurahisi bali ni uvumilivu na kuchapa kazi pasipo kukata tamaa ndiko kunakomfanya afikie hapa alipo sasa hivi. Kumbe kila jambo ili kufanikiwa uvumilivu na kutokukata tamaa ni nguzo muhimu sana.

Sikiliza audio ya wimbo huo hapa chini;

0 Response to "……TEMBA NA CHEGE MKIONA KITU GANI…...SISI, CHAPA NYINGINE……TMK MKIONA KITU GANI…."

Post a Comment