MAAJABU: KISIWA KIPYA CHAOTA BAHARINI KAMA UYOGA | JIFUNZE UJASIRIAMALI

MAAJABU: KISIWA KIPYA CHAOTA BAHARINI KAMA UYOGA


Kisiwa kikiota kama uyoga
Wakati  wanasayansi wakikuna vichwa vyao ni jinsi gani Dunia itazuia kumezwa kwa visiwa na maji ya bahari kama vile kisiwa cha Zanzibar, Madagascar na vinginevyo vingi kutokana na ongezeko la ujoto Duniani linalochangiwa kwa kiasi kikubwa na ongezeko la hewa za viwandani za ukaa ‘co2’ huko nchini Japani ambayo ni nchi ya visiwa vingi kumezuka ghafla kisiwa katikati ya bahari kutokana na mlipuko wenye nguvu wa Volcano.

Kisiwa hicho kinachoota mithili ya uyoga na kuongezeka ukubwa kila dakika inayopita, kimewaacha watu wengi midomo wazi kutokana na kila dakika kubadilika umbo. Kisiwa hicho kimeibuka kilomita 1,000 Kusini mwa jiji kuu la Tokyo miezi 2 iliyopita baada ya mlipuko wenye nguvu wa volcano kutokea chini ya bahari hiyo ya Pasific. Wachambuzi wa mambo tayari wameshasema kwamba kisiwa hicho kinaweza kikaongeza zaidi ukubwa wa nchi hiyo ya Japan katika eneo la bahari maalumu kiuchumi.

Kisiwa kipya kikiungana na cha zamani.
Wataalamu wa volcano wamesema kwamba lava hiyo itaendelea kumwagika na pengine kuweza hata kuungana na kisiwa kingine cha zamani kilichokuwa karibu  nacho. Kwa sasa kisiwa hicho ukubwa wake ni mara 8 zaidi ya ukubwa wakati kilipozaliwa hapo Novemba  20 mwaka jana. Kisiwa cha jirani ambacho kinakaribia kuungana nacho kinaitwa “Nishino Shima” na jina hilo hilo ndilo kisiwa hicho nacho wameamua kiitwe.

Kwa mujibu wa shirika la “NASA” la Marekani, uhunguzi waliofanya angani katika eneo hilo umebainisha kuwa Volcano ya chini ya bahari kwa mara ya mwisho katika eneo hilo ililipuka tena mwaka 1973 na 1974. Kisiwa kinachoishi watu kipo kilomita 130 au maili 80 kutoka kilipo hiki. Wakati Wajapan wengi wanaishii katika visiwa vinne vikubwa zaidi, Taifa hilo linaundwa na takribani maelfu ya visiwa vidogovidogo vilivyotapakaa huku vingine vikiwa katika mgogoro na Taifa jirani la Uchina.

0 Response to "MAAJABU: KISIWA KIPYA CHAOTA BAHARINI KAMA UYOGA"

Post a Comment