CHANCELOR WA UJERUMANI ANGEL MERKEL NAYE ANUSURIKA KIFO KATIKA AJALI YA KUTELEZA KWENYE BARAFU | JIFUNZE UJASIRIAMALI

CHANCELOR WA UJERUMANI ANGEL MERKEL NAYE ANUSURIKA KIFO KATIKA AJALI YA KUTELEZA KWENYE BARAFU

Habari za hivi punde zinasema kwamba Kiongozi wa nchi ya Ujerumani Chancelor Angel Merkel amepata ajali ya kuanguka wakati akicheza mchezo wa kuteleza katika barafu huko nchini Switzealand na amepatwa na majeraha kidogo katika paja lake. Habari zaidi zinasema kwamba ameumia lakini siyo kwa kiwango cha kumfanya ashindwe kutekeleza majukumu yake ya kila siku ya uongozi. 

Msemaji wake amesema; "Hakuwa akiteleza kwa kasi, na sehemu ya mfupa wake wa paja la kushoto imepata mpasuko kidogo pamoja na michubuko sehemu za mwili, atalazimika kupumzika kwa wiki kadhaa ikiwa ni pamoja na kuahirisha ziara zake kadhaa nje ya nchi"  

Merkel katika mchezo wa kuteleza kwenye barafu.
Angela Merkel huwa ana kawaida ya kucheza mchezo huo mara kwa mara. Hivi karibuni ajali nyingine kama hiyo ilimpata dereva maarufu wa mashindano ya magari ya Formula One, Michael Schumachel ambaye awali hali yake ilikuwa tete lakini baadaye madaktari wakasema hali yake ilikuwa ikiimarika baada ya kumfanyia operesheni kuondoa shinikizo katika ubongo wake.

Chanzo bbc.

0 Response to "CHANCELOR WA UJERUMANI ANGEL MERKEL NAYE ANUSURIKA KIFO KATIKA AJALI YA KUTELEZA KWENYE BARAFU"

Post a Comment