MH.EDWARD LOWASA CHUPUCHUPU KIFO: ANUSURIKA AJALI YA NDEGE ARUSHA | JIFUNZE UJASIRIAMALI

MH.EDWARD LOWASA CHUPUCHUPU KIFO: ANUSURIKA AJALI YA NDEGE ARUSHA

Waziri Mkuu mstaafu Mh. Edward Lowasa

Leo HIi ndege ya Precision Air iliyokuwa ikitokea Dar es salaam kuelekea Arusha almanusura ipate ajali wakati ikijiandaa kutua baada ya mlipuko kusikika uliotokana na kupasuka kwa matairi yake mawili ya nyuma huku ikiwa imebeba abiria wapatao 50 miongoni mwao alikuwepo pia Waziri Mkuu mstafu na mbunge wa Monduli Mheshimiwa Edward Ngoyai Lowasa.

Akizungumza na kipindi cha daladala Radio one Stereo jioni hii Saleh John, mmoja kati ya hao abiria aliisema kwamba, licha ya kishindo kilichosikika hakuna madhara mengine yeyote kwa abiria wala kwa ndege yenyewe na abiria mara tu ndege hiyo ilipotua kila mmoja alionekana kukimbia kutoka ndani ya ndege hiyo. Alisema pia kwamba hiyo ni hitilafu ya kawaida tu iliyotokea.

0 Response to "MH.EDWARD LOWASA CHUPUCHUPU KIFO: ANUSURIKA AJALI YA NDEGE ARUSHA"

Post a Comment