MAREKANI YADAI OBAMA ALIKUWA HATARINI MBELE YA MKALIMANI MZUSHI | JIFUNZE UJASIRIAMALI

MAREKANI YADAI OBAMA ALIKUWA HATARINI MBELE YA MKALIMANI MZUSHI

Mkalimani aliyezua tafrani ya aina yake duniani, baada ya kubainika kuwa kumbe hakuwa akiwatafsiria walemavu kile alichokuwa akihutubia Rais Obama, bali alikuwa akifanya mauza uza ameiweka serikali ya Afrika ya Kusini katika hali ngumu baada ya Marekani kuhoji kuwa mtu huyo aliwezaje kupenya mpaka sentimita chache tu kutoka Rais Obama alipokuwa amesimama.
Rais Obama akiwa sentimita chache kando ya Mkalimani huyo wa bandia.
Mkalimani huyo feki, Thamsanqa Jantjie miaka(34) akijibu tuhuma hizo zinazomkabili alidai etia  alipatwa na mauza uza baada ya kuwaona malaika wakishuka pale uwanjani na hivyo kushindwa kumsikiliza vizuri Rais Obama, pia alidai kwamba aliwahi kukumbwa na matatizo ya akili wakati alipokuwa mdogo na hivyo hali hiyo iliweza kumrudia wakati akiwa hapo uwanjani akitafsiriu. 
Thamsanqa Jantjie akijitetea mbele ya waandishi wa habari.
 Inashangaza ni vipi mtu huyo aliyekuwa na historia huko nyuma ya kushindwa kutafsiri katika shughuli nyingine tena ya ANC akapewa tena tenda na kampuni husika katika shughuli nzito kama ile. Je, yaweza kuwa ni udhaifu wetu Waafrika katika kufanya mambo ndiyo maana hata mataifa mengine hawatuamini?

Mkalimani  feki akifanya vitu vyake FNB

0 Response to "MAREKANI YADAI OBAMA ALIKUWA HATARINI MBELE YA MKALIMANI MZUSHI"

Post a Comment