MADIBA ALIKUWA MFANO KWANGU, BARAK OBAMA AKIHUTUBIA KATIKA SHUGHULI ZA MWISHO ZA KUMUAGA KIONGOZI HUYO MWAFRIKA MASHUHURI ZAIDI KARNE YA 20 | JIFUNZE UJASIRIAMALI

MADIBA ALIKUWA MFANO KWANGU, BARAK OBAMA AKIHUTUBIA KATIKA SHUGHULI ZA MWISHO ZA KUMUAGA KIONGOZI HUYO MWAFRIKA MASHUHURI ZAIDI KARNE YA 20


Hotuba ya rais Barak Obama wa Marekani katika shughuli za mwisho za ibada ya kumuaga shujaa Nelson Madiba Mandela katika safari yake ya mwisho imepokewa kwa msisimko wa aina yake na maelfu ya watu waliofurika katika uwanja wa mpira wa FNB  ambapo viongozi mbalimbali wa dunia wametoa salamu zao za rambirambi kumuaga akiwemo pia Rais wa Taifa la Tanzania Mh. Jakaya Mrisho Kikwete.

Amemuelezea Mandela kwamba alikuwa ni kioo chake kutokana na kuwa ndiye mtu aliyemvutia tangu utotoni mwake na kumfanya afuate nyayo zake mpaka kuweza kutimiza ndoto za kuja kuliongoza Taifa kubwa la Marekani.

Obama kama kawaida ya Hotuba zake lakini ya leo aliitoa kwa hisia kali zaidi akionyesha huzuni na kuguswa mno huku kila mara akimtaja Madiba na neno Ubuntu, alionyesha kuwagusa sana wananchi wa Afrika ya Kusini pale alipotaja maneno yenye asili yao kama UBUNTU. Ubuntu ni neono la Kingoni ambacho ni kibantu lenye maana ya UBINADAMU (binadamu wote ni sawa). Obama alitamka hasa kile wananchi wa Afrika Kusini walichakitaka tofauti na viongozi wengine waliozungumza.

Alikuwa akimuelezea Mandela kwa mapana utafikiri mwenyewe kazaliwa South, alikuwa akitamka lugha ile ya miaka ya 80, mzee Madiba akiwa kifungoni na muda mfupi baada ya kutoka, akiyataja majina maarufu ndani ya ANC kama vile kina Walter Sisulu, Oliver Tambo kwa kweli watu walishangilia kwa furaha hata kusahau kama ulikuwa ni msiba, utadhani ilikuwa ni sherehe vile. Hata alipokuwa akihutubia Rais wa Africa kusini Jacob Zuma hapakuonekana msisimko kama huo wa Obama.


Pia Rais Obama katika tukio hilo ameshikana mkono kwa salamu na rais Raul Castro wa Cuba, nchi ambayo ni hasimu wa muda mrefu wa Taifa hilo la Marekani. 

0 Response to "MADIBA ALIKUWA MFANO KWANGU, BARAK OBAMA AKIHUTUBIA KATIKA SHUGHULI ZA MWISHO ZA KUMUAGA KIONGOZI HUYO MWAFRIKA MASHUHURI ZAIDI KARNE YA 20 "

Post a Comment