“TUWAKATAE HAWA WAUZA UNGA MAKANISANI, NA MISIKITINI …” | JIFUNZE UJASIRIAMALI

“TUWAKATAE HAWA WAUZA UNGA MAKANISANI, NA MISIKITINI …”

'Makanisani na Misikitini'
Hayo yamesemwa leo asubuhi na Katibu Mkuu wa Shirika la linalojishughulisha na uzuiaji wa matumizi ya dawa za kulevya na utoaji wa elimu ya jinsi ya kuepuka matumizi ya dawa hizo nchini, bwana Fabian J.Mkingwa alipokuwa akizungumza na Capital redio juu ya mada iliyohusu, ‘Juhudi zinazofanywa na serikali pamoja na wadau mbalimbali kuzuia matumizi ya dawa za kulevya zimefanikiwa?


Katika maelezo yake hayo alitilia mkazo sana katika elimu ya kijamii, ustawi wa jamii katika watu kujitambua. Alisema, “Mtu  anapaswa kujitambua aweze kufahamu ,  ‘mimi kama mimi ninatakiwa kuwa nani siku za usoni, nitatakiwa  nipitie hatua zipi ili kuwa kama hivyo ninavyotaka  kuwa’. Lakini pia kutengeneza jamii ya watu ambayo wanapenda kuthamini mafanikio yaliyotokana na hatua halali za kufanikiwa.

Ikionekana kwamba tunamthamini mtu ambaye hatujui fedha kazipataje, tujue kabisa mwisho wa siku watu watamuangalia yule na wengine watafuatilia amepataje mafanikio. Sasa kama amepata mafanikio kwa kuuza madawa ya kulevya , maana yake tutazalisha wauzajiwa dawa za kulevya wengi . Kwa hiyo sisi tutengeneze mazingira ya kuwachukia, kutokuwakubali, hawa wanaofanya biashara  ya dawa za kulevya, hata Misikitini, Makanisani na kwingineko. Kama kuna mtu tunahisi ya kwamba anafanya biashara ya dawa za kulevya,  hata kama ana mafanikio makubwa kiasi gani, tunahitaji fedha zake, sasa tuzikatae hizo fedha zake na tusimthamini kwa sababu ya fedha zake.

Akidharaulika huyu, inawezekana kabisa kwamba tukatengeneza kizazi cha vijana ambao wanajua  kwa kujiingiza katika biashara kama hii watadharaulika”


Bwana Fabian pia amesema kwamba Taasisi yao imeanzisha kampeni iitwayo ‘ACHA KULALAMIKA’ ambayo inalenga kuifanya jamii, ikiwemo serikali yenyewe kuacha kulaamika na kulaumiana kila kitu na badala yake kila mtu atImize wajibu wake katika kutokomeza matatizo mbalimbali likiwemo hili la dawa za kulevya.   

0 Response to "“TUWAKATAE HAWA WAUZA UNGA MAKANISANI, NA MISIKITINI …”"

Post a Comment