KAMERA ZA CCTV ZINGELIWEZA KUKOMESHA UNYAMA HUU | JIFUNZE UJASIRIAMALI

KAMERA ZA CCTV ZINGELIWEZA KUKOMESHA UNYAMA HUU

MAONI YANGU.
Uhalifu unaoendelea nchini hususani visiwani Zanzibar ungeweza kupungua kwa kiwango kikubwa au kumalizika kabisa endapo zingeliwekwa kamera maalumu mitaani za cctv  (videosurveillance systems) ambazo huweza kuwanasa 'live' watuhumiwa wakati wakitekeleza unyama wao.
Mataifa yaliyoendelea ni nadra sana kukuta kitendo kama cha kumwagia mtu tindikali tena hadharani kushindikana kujulikana waliotenda.  Nchi kwa mfano Uingereza serikali za miji mbalimbali zinanaweka bajeti kubwa sana kwenye mifumo hii ili kuweza kukabiliana na uhalifu wa namna hii.

Sasa  matukio hayo yenye sura ya kigaidi yamefika zaidi ya 8, huku jeshi la polisi likidai linafanya uchunguzi. Kuna tukio hili la padre wa kanisa katoliki Padri Joseph Onesmo mwangamba aliyemwagiwa tindikali, Sheha wa Mohamed Omar Said wa Tomondo naye alimwagiwa tindikali, Padri tena wa Kanisa katoliki Parokia ya Mtoni mjini Magharibi  padre Evaristi Mushi yeye aliuwawa kwa risasi.

Padre Ambros Mkenda naye alijeruhiwa vibaya kwa risasi, mmiliki wa Home shopping centre Said Mohammed Saad jijini Dar alimwagiwa tindikali,  wasichana Kate Gee na Kristie Trup wote raia wa Uingereza waliomwagiwa tindikali na kuumia maeneo mbalimbali miilini mwao,  Katibu wa Mufti Zanzibar Shehe Fadhil Sulleiman Soraga aliyejeruhiwa vibaya kwa kumwagiwa tindikali usoni,  na matukio mengine ni milipuko ya mabomu katika mkutano wa chama cha CHADEMA na sherehe za uzinduzi wa parokia kanisa katoliki Olasiti.

Pamoja na uchunguzi huo serikali inaodai unaendelea lakini mpaka sasa hivi hakuna mtuhumiwa yeyote aliyetiwa hatiani na mahakama au kubainika kwa uhakika kabisa ni mtandao gani au kikundi kinachojihusisha na njama hizo au wana sababu zipi zinazowasukuma kutenda matendo hayo yaliyokuwa kinyume kabisa, siyo tu na  haki za binadamu,  bali hata na dini yeyote ile chini ya jua inayomtaja Mwenyezi Mungu.  


0 Response to "KAMERA ZA CCTV ZINGELIWEZA KUKOMESHA UNYAMA HUU"

Post a Comment