Kenya yagundua visima vikubwa vya maji chini ya ardhi | JIFUNZE UJASIRIAMALI

Kenya yagundua visima vikubwa vya maji chini ya ardhi

Eneo la Turkana lenye ukame mkubwa
Serikali ya Kenya imetangaza ugunduzi wa visima vikubwa vya maji chini ya ardhi ambavyo vinaweza kumudu mahitaji ya maji katika kipindi cha zaidi ya miaka hamsini ijayo katika jimbo la Turkana na kwa nchi nzima.
Visima hivyo bila shaka vitaleta afueni kwa wakaazi kwani Turkana ni eneo kame Kaskazini Magharibi mwa Kenya. Eneo hilo pia lina viwango vya juu vya umaskini.

Ugunduzi huo ulitokana na utafiti wa wanasayansi waliotumia teknolojia ya satellite
Visima hivyo vinapata maji kutoka kwa chemichemi za maji kutoka milima ya mbali kwa hivyo maji yake yakitumiwa vyema huenda havitawahi kukauka.

Mamilioni ya wakenya wanakosa maji safi.
Nchi hiyo pia inakabiliwa na msimu tata wa mvua na inakabiliwa na athari za mabadiliko ya tabia nchi.

Utafiti ulifanywa na shirika la Umoja wa mataifa la UNESCO na wanasayansi wa Kenya kwa ufadhili wa serikali ya Japan.

0 Response to " Kenya yagundua visima vikubwa vya maji chini ya ardhi"

Post a Comment