PAPA FRANCIS ATOA SALAMU ZA EID EL FITR KWA WAISLAMU WOTE DUNIANI. | JIFUNZE UJASIRIAMALI

PAPA FRANCIS ATOA SALAMU ZA EID EL FITR KWA WAISLAMU WOTE DUNIANI.


VATICAN CITY
Papa Francis binafsi ametoa salamuza Eid El Fitr kwa Waislamu wote duniani, baada ya kuhitimisha Mwezi mtukufu wa Ramadhani huku akiwahimiza kuheshimiana baina ya Dini zote.


Salamu kama hizi kwa kawaida hutolewa kila mwaka na Vatican lakini tofauti ni kwamba miaka mingine hutolewa na Baraza la Kipapa la mijadala ya kiimani.Hii ni mara ya pili kwa ujumbe binafsi kutolewa na papa tangu mtangulizi wake Papa Yohane Paul II mwaka 1991.

Alitoa wito wa kudumisha kuheshimiana kwa njia ya kutoa elimu. Huku mivutano ya kikanda na kidini ingali ikishika kasi kote duniani, Papa amehimiza umuhimu wa kuheshimiana na umuhimu wa kuwaelimisha vijana wa Kiislamu na Kikristo juu ya upendo na  kuheshimiana.

“Sote tunafahamu kuheshimiana ni jambo la msingi katika mahusiano yeyote yale ya binadamu hasa miongoni mwa watu wanaohubiri imani za dini. Kwa njia hii, urafiki wa kweli na wa kudumu unaweza kukua. Ujumbe wangu kwenu mwaka huu ni kuwataka nyote Waislamu na Wakristo kuakisi matendo yenu ya kiimani na kudumisha ushirikiano na kuheshimiana” Alisema Papa.

0 Response to "PAPA FRANCIS ATOA SALAMU ZA EID EL FITR KWA WAISLAMU WOTE DUNIANI."

Post a Comment