JOKA AINA YA CHATU LAUA WATOTO WAWILI. | JIFUNZE UJASIRIAMALI

JOKA AINA YA CHATU LAUA WATOTO WAWILI.

Liliwafuata juu ghorofani,

Chatu (African  rocks python)
Canada.
Watoto wawili waliouwawa na chatu wametambulika kuwa ni mtu na kaka yake wenye umri wa miaka 5 na 7, CBC News wamefahamishwa. Mamlaka husika zimesema kwamba uchunguzi wa miili ulipangwa kufanyika leo ili kujua ni kitu gani kilichotokea.

Noah Barthe miaka 5 na Cormo  Barthe miaka 7 waliuwawa na Joka hilo, (African rock python) lilipokuwa likitembeatembea juu vyumba vya ghorofani baada ya kutoroka eneo la chini katika tundu lilikokuwa limefungiwa. Watoto hawa walikutwa siku ya jumatatu asubuhi wakiwa wameshakufa. Uchunguzi kama kuna jinai umeanzishwa huku mauaji hayo yakiwastaajabisha hata wataalamu wenyewe wa nyoka.

“Ni maajabu, anasema Lee Parker meneja wa hifadhi ya wanyama aina ya reptilia ‘zoo’ iliyoko Ontario.”Chatu huwa hawana kawaida ya kuua ovyo……haiingii akilini kabisa. Pia meneja mwingine wa hifadhi ya Hamilton Jeff Reynolds alisema Chatu aina ya African Rocks Python siyo wagomvi, naona ajabu sana kuwaua hawa watoto”

Chatu ndio nyoka mkubwa zaidi Africa na huweza kufikia mpaka kimo cha  mita 6. Parker anaongeza, “Hatuwashauri watu kufuga nyoka wakubwa kwa sababu ya hatari inayoweza kutokea, Chatu wa Barnes, Anaconda, Boa……, hawa ni hatari !

0 Response to "JOKA AINA YA CHATU LAUA WATOTO WAWILI."

Post a Comment