GURUMO, MJASIRIAMALI WA MUZIKI ALIYESTAAFU ANGALI MASIKINI | JIFUNZE UJASIRIAMALI

GURUMO, MJASIRIAMALI WA MUZIKI ALIYESTAAFU ANGALI MASIKINI

Katika kila Nyanja maishani iwe ni kazi , biashara, au hata  vipaji  ni lazima kuwe na watu ambao tunaweza tukawaita  wajasiriamali, kwa maana kwamba watu hao wamejikita vilivyo katika Nyanja husika. Mmoja wao ni Gwiji la muziki wa dansi nchini kwa takribani miaka 50, Maalimu Muhidin Gurumo aliyeamua kustaafu rasmi kazi ya muziki.
Maalim Gurumo kulia na kushoto ni Nyosh El Saadat

Cha kustaajbisha ni kwamba mpaka anastaafu Maalim Gurumo anaishi maisha ya kawaida kabisa tofauti na watu wengi wanavyomdhania, hata anapokwenda kliniki kwa matibabu ya ugonjwa unaomsumbua watu kwenye daladala wanashangaa mno kuona akisukumana na watu licha ya hadhi aliyokuwa nayo kitaifa na kimataifa.Ingefaa Taifa limfikirie hata ingewezekana akapatiwa mahitaji muhimu ikiwa ni pamoja na usafiri wake binafsi.

Akiwa na Tanzania All Stars
Siyo jukumu la serikali peke yake bali hata wadau mbalimbali, watu binafsi, makampuni na watanzania kwa ujumla, tusisubiri mpaka atakapoondoka duniani tuanze kutoa sifa na rambirambi kibao ambazo hata hazitomsaidia kitu wakati huo.

Akiwa na mkewe Bi Pili Saidi
Picha zote zimetoka katika blogu ya burudan.blogspot.com na ukipenda kusoma kwa undani makala juu ya maisha ya Mjasiriamali huyu wa muziki basi tembelea blogu hiyo hapa

0 Response to "GURUMO, MJASIRIAMALI WA MUZIKI ALIYESTAAFU ANGALI MASIKINI"

Post a Comment