Wahitimu wa vyuo vikuu kuwezeshwa mikopo kujiajiri | JIFUNZE UJASIRIAMALI

Wahitimu wa vyuo vikuu kuwezeshwa mikopo kujiajiri

 NA MWANDISHI WETU
Wizara ya Kazi na Ajira kwa kushirikiana na Benki ya CRDB imezindua mpango wa kukuza ajira kwa vijana 30,000 kwa kuwapatia mikopo wahitimu wa vyuo vikuu vya elimu ya juu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wiki hii, Msemaji wa wizara hiyo Ridhiwani Wema, alisema lengo la mpango huo ni kuongeza idadi ya vijana wanaomiliki shughuli rasmi za kiuchumi na waweze kujiajiri na kuajiri wengine na kukuza utamaduni wa kijasiriamali pamoja na ubunifu.


“Serikali imeamua kutoa fursa kwa vijana 30,000 za moja kwa moja kwa wahitimu wa elimu ya juu kwa kipindi cha miaka mitatu na kuwawezesha wenzao wa kada ya uchumi wasiopungua 100,000, ajira hizi zitakuwa ni za moja kwa moja mbali na zile zitakazotokana na mnyororo mzima wa thamani” alisema Wema.

Alisema serikali imekubaliana na benki ya CRDB kuanzisha utoaji wa mikopo kwa vijana mara utekelezaji wa program utakapoanza.


Pia alisema kuwa mpango huo  utatekelezwa na serikali kwa kushirikiana na vyuo vya elimu ya juu nchini, taasisi za fedha na wabia wa maendeleo.
CHANZO: NIPASHE

0 Response to "Wahitimu wa vyuo vikuu kuwezeshwa mikopo kujiajiri"

Post a Comment