IJUE BIDHAA YA BEI RAHISI KULIKO ZOTE DUNIANI, KILA MTU ANAMILIKI LUNDO! | JIFUNZE UJASIRIAMALI

IJUE BIDHAA YA BEI RAHISI KULIKO ZOTE DUNIANI, KILA MTU ANAMILIKI LUNDO!

HATUA YA 7 KUELEKEA UTAJIRI
SURA YA 8
MAAMUZI
Kiboko ya Kusitasita
(Hatua ya 7 kuelekea utajiri)

Uchanganuzi sahihi wa wanaume na wanawake zaidi ya 25,000 ambao walipata uzoefu wa kuanguka walisema ukweli  kwamba  ukosefu wa maamuzi ulikuwa karibu na mwanzo wa orodha ya sababu kuu 30 za kuanguka. Hii siyo kauli ya kinadharia tu – ni ukweli kuahirisha  au kinyume cha maamuzi ni adui wa wote ambaye karibu kila mtu ni lazima amshinde.

Utakuwa na fursa ya kujaribu uwezo wako wa kufikia maamuzi kamili na yaharaka wakati utakapomaliza kusoma kitabu hiki na kuwa tayari kuanza kutia katika vitendo kanuni kinachoelezea. Uchunguzi wa mamia ya watu waliojikusanyia utajiri zaidi ya dola milioni moja walifichua ukweli kwamba kila mmoja wao alikuwa na tabia ya kufikia maamui haraka na ya kuyabadilisha hayo maamuzi polepole ikiwa waliyabadilisha.

Watu walioshindwa kujikusanyia utajiri, bila ya kisingizio, walikuwa na tabia ya kufikia maamuzi ikiwa waliyafikia, polepole sana na kuyabadilisha maamuzi hayo haraka na kila mara.

Moja ya sifa bora zaidi ya Henry Ford ilikuwa ni tabia yake ya kufikia maamuzi haraka na kwa ukamilifu, na kuyabadilisha taratibu. Sifa hii ilivuma sana kwa Bwana Ford kiasi kwamba ilimpa hadhi ya kuitwa mbishi sugu. Ilikuwa ni tabia hii iliyomchochea Bwana Ford kuendelea kuzalisha gari lake maarufu Model ‘T’(gari baya zaidi duniani), wakati washauri wake wote na wengi wa wateja wa gari hilo walikuwa wakimshauri kulibadilisha.

Pengine Bwana Ford alichelewa sana kufanya mabadiliko, lakini upande mwingine wa shilingi ni kwamba msimamo wa maamuzi ya Bwana Ford ulizaa utajiri mkubwa kabla ya mabadiliko katika Model T hayajafanyika.Yapo mashaka kakini kidogo sana kwamba tabia ya Ford katika msimamo wa kufanya uamuzi ilimfanya adhaniwe kuwa ni mkaidi, lakini tabia hii ni hitaji katika kufikia maamuzi taratibu na uharaka katia kuyabadilisha.

Wengi wa watu wanaoshindwa kujipatia pesa za kutosha kwa mahitaji yao kwa ujumla huathiriwa kirahisi na maoni ya wengine. Huruhusu magazeti na majirani wambea ‘kufikiria’ badala yao. ‘Maoni’ ndiyo bidhaa rahisi zaidi hapa duniani. Kila mtu ana lundo la maoni tayari kumpatia mtu yeyote atakayeyakubali. Kama unaathiria na ‘maoni’ unapofikia maamuzi, hautafanikiwa katika shughuli yeyote, na zaidi katika kazi ya kugeuza shauku yako mwenyewe kuwa pesa.

Ikiwa unaathiriwa na maoni ya wengine, hautakuwa na hamu ya maoni yako mwenyewe.

Tunza ushauri wako mwenyewe wakati utakapoanza kutia katika vitendo kanuni zilizoelezwa hapa kwa kufikia maamuzi yako mwenyewe na kuyafuata. Usimshirikishe yeyote isipokuwa wanachama wa kundi lako la kushauriana(Master Mind Group),  na uhakikishe katika uchaguzi wako wa kundi hili, unachagua wale tu watakaokuwa katika huruma kamili na mapatano na lengo lako

Marafiki wa karibu na ndugu wakati hawadhamirii kufanya hivyo, mara nyingi humlemaza mtu kupitia “maoni” na wakati mwingine kupitia mzaha ambao unamaanisha kuwa ucheshi, maelfu ya wanaume na wanawake hubeba hali ya kutojiamini maisha yao  yote kwa sababu baadhi ya watu wenye maana nzuri lakini wajinga waliharibu kujiamini kwao kupitia ‘maoni’ au mzaha.

Una ubongo na akili yako mwenyewe. Uitumie na kufikia maamuzi yako mwenyewe. Ikiwa unahitaji ukweli ama taarifa kutoka kwa watu wengine kukuwezesha kufikia maamuzi bila shaka kama utakavyofanya mara nyingi, jipatie ukweli huo au tafuta taarifa unazohitaji kimyakimya bila kufichua lengo lako.

Ni tabia ya watu walio na ujuzi kidogo au wa bandia kujaribu kutoa taswira kwamba wana ujuzi mkubwa. Watu hao kwa ujumla huongea sana na kusikiliza kidogo sana. Fungua macho yako na masikio na kuufunga mdomo wako ikiwa unataka kuwa na tabia ya kufanya maamuzi haraka. Wale wanaozungumza kupita kiasi, hawafanyi kitu kingine chochote. Ikiwa unazungumza zaidi kuliko unavyosikiliza, hujinyimi tu mwenyewe fursa nyingi za kujipatia ujuzi wenye manufaa, lakini pia unafichua mipango yako na malengo kwa watu watakaofurahia mno kukushinda, kwasababu wanakuonea wivu.

Kumbuka pia kwamba kila wakati unapofungua mdomo wako mbele ya mtu mwenye ujuzi mwingi, unafunua kwa huyo mtu akiba yako kamili ya maarifa! Busara halisi kwa kawaida huonekana kupitia staha na ukimya. Kumbuka ukweli kwamba kila mtu unayekutana naye ni kama wewe mwenyewe, anatafuta fursa ya kujipatia pesa. Ikiwa utazungumzia kuhusu mipango yako kwa uwazi mno, unaweza kuja kushangaa utakapokuta kwamba watu wengine wamekuzidi kete lengo lako kwa kuweka katika vitendo kabla yako mipango uliyozungumza bila tahadhari.

Acha moja kati ya uamuzi wako wa kwanza kuwa ni kufunga mdomo na kufungua macho na masikio. Kama kumbukumbu kwako  mwenyewe kufuata ushauri huu, itapendeza ikiwa utanakili usemi ufuatao katika herufi kubwa na uuweke mahali utakapouona kila siku:

IAMBIE DUNIA KILE UNACHOPANGA KUFANYA, LAKINI KWANZA KIONYESHE.

Hii ni sawa na kusema kwamba, “Vitendo na wala siyo maneno ndivyo vyenye maana zaidi”

Uhuru au Kifo Katika Maamuzi
Thamani ya maamuzi hutegemea ujasiri unaohitajika kuyafanya. Maamuzi makubwa yaliyotumika kama msingi wa ustaarabu yalifikiwa kwa kuchukua hatari kubwa ambayo mara nyingi ilimaanisha uwezekano wa kifo.

Uamuzi wa Lincoln wa kutoa tamko lake mashuhuri la Uhuru, lililotoa uhuru kwa watu wa Marekani, ulichukuliwa kwa utambuzi kamili kwamba kitendo chake kingeliweza kuwafanya maelfu ya marafiki na wafuasi wake kisiasa kumgeuka. Alfahamu pia kwamba kutoa tangazo lile kungeweza kumaanisha vifo kwa maelfu ya watu katika uwanja wa mapambano. Mwishowe, ulimgharimu Lincoln maisha yake. Hilo lilihitaji ujasiri.

Uamuzi wa Socrate wa kunywa kikombe cha sumu kuliko kwenda kinyume na imani yake binafsi ulikuwa ni uamuzi wa kijasiri, uligeuza muda mbele miaka elfu moja na kuwapa watu ambao hawakuwa wamezaliwa bado, haki ya uhuru wa kufikiri na wa kuongea.

Uamuzi wa Generali Robert E. Lee alipojitenga na Muungano na kuchukua uelekeo wa Kusini ilikuwa ni moja ya ujasiri kwani alifahamu vizuri kuwa ungeliweza kugharimu maisha ya wengine. Lakini uamuzi mkubwa wa wakati wote, kwa kadri raia yeyote yule wa Marekani anavyohusika, ulifikiwa Philadelphia mnamo tarehe 4 Julai 1776, wakati watu 56 walipotia saini majina yao kwenye andiko ambalo walifahamu vizuri lingeweza kuleta uhuru kwa Wamarekani wote, au kuacha kila mmoja kati ya hao 56 wakinyongwa vitanzini.

Umewahi kusikia juu ya andiko hili maarufu, lakini unaweza kuwa hujapata kutoka kwake somo kubwa katika mafanikio binafsi liliyofunza dhahiri.

Sote tunakumbuka tarehe ya uamuzi huu muhimu sana, lakini wachache wetu tunatambua ni ujasiri kiasi gani uamuzi huo ulihitaji. Tunatambua historia kama ilivyofundishwa, tunakumbuka tarehe na majina ya watu waliopigana, tunakumbuka Valley Forge na Yorktown, tunawakumbuka George Washington na Lord Cornwallis. Lakini tunakumbuka machache kuhusiana na nguvu halisi nyuma ya majina haya, tarehe na sehemu.

Bado tunafahamu kidogo juu ya nguvu isiyoshikika, iliyohakikisha uhuru kwa Wamarekani zamani kabla majeshi ya Washington kufika mji wa Yorktown.

Tunasoma historia ya mapinduzi na kudhania uwongo kwamba George Washington alikuwa Baba wa Marekani, kwamba ni yeye aliyewaletea Wamarekani uhuru wao. Ukweli ni kwamba Washington alikuwa kiungo tu baada ya ukweli, kwasababu ushindi kwa majeshi yake ulikuwa umehakikishwa kitambo kabla Lord Cornwallis hajajisalimisha. Hili halikusudii kumnyang’anya Washington utukufu wowote anaostahili. Lengo lake badala yake ni kutoa usikivu mkubwa kwa nguvu ya kushangaza iliyokuwa sababu ya kweli ya ushindi wake.

Ilikuwa ni kama janga kwamba waandishi wa historia wameruka kabisa hata kumbukumbu kidogo kwa nguvu hii isiyoshindwa iliyozaaa na kutoa uhuru kwa Taifa lililokusudia kuweka vipimo vipya vya Uhuru kwa watu wote wa Dunia. Nasema ni janga kwasababu ni nguvu ileile ambayo ni lazima itumike na kila mtu anayeshinda magumu ya maisha, na kulazimisha maisha kulipa gharama iliyodaiwa.


Hebu tupitie kwa ufupi matukio yaliyozaa hii nguvu. Hadithi inaanzia na tukio la Boston tarehe 5 Machi 1770. Wanajeshi wa Uingereza walikuwa wakipiga doria barabarani wakiwatisha raia waziwazi kwa uwepo wao.


UKIPENDA KUSOMA SURA NA SEHEMU ZOTE ZA KITABU HIKI

0 Response to "IJUE BIDHAA YA BEI RAHISI KULIKO ZOTE DUNIANI, KILA MTU ANAMILIKI LUNDO!"

Post a Comment