FURSA ZIPO, CHAGUA UTAKACHO,TENGENEZA MPANGO, TEKELEZA NA KUFUATILIA KWA UVUMILIVU UTAFANIKIWA | JIFUNZE UJASIRIAMALI

FURSA ZIPO, CHAGUA UTAKACHO,TENGENEZA MPANGO, TEKELEZA NA KUFUATILIA KWA UVUMILIVU UTAFANIKIWA

Hii ni jamii ya Kibepari. Iliundwa kupitia matumizi ya mtaji, na sisi tunaodai haki ya kushirikishwa baraka za uhuru na fursa, sisi tunaotafuta kupata utajiri hapa, inaweza kufahamika kwamba siyo utajiri wala fursa vinaweza kupatikana kwetu ikiwa mtaji uliopangiliwa haukutoa faida hizi.

Ikiwa wewe ni mmoja wa wale wanaoamini kwamba utajiri unaweza kupatikana tu kwa kitendo cha watu wanaojikusanya wenyewe katika makundi na kudai malipo zaidi kwa huduma kidogo, ikiwa wewe ni mmoja wa wale wanaodai msaada wa Serikali bila adha za asubuhi na mapema wakati pesa zinapoingia kwako, ikiwa wewe ni mmoja wa wale wanaoamini katika kuuza kura zao kwa wanasiasa kwa malipo ya kupitisha sheria zinazoruhusu kupora hazina ya umma, unaweza ukatulia bila bughudha katika imani yako kwa utambuzi kuwa hakuna mtu atakayekuhangaisha kwa sababu hii ni nchi huru ambapo kila mtu anaweza akafikiri kama atakavyo, ambapo karibu kila mtu anaweza akaishi kwa juhudi kidogo, ambapo wengi wanaweza kuishi vizuri bila ya kufanya kazi yeyote.

Hata hivyo unapaswa kutambua ukweli mzima kuhusu uhuru huu ambao watu wengi kiasi hicho hujivunia na wachache kiasi hicho kuutambua. Mkubwa kama ulivyokuwa, mbali kama unavyofika, faida nyingi kama unavyoweza kutoa, hauleti na wala hauwezi kuleta utajiri bila jitihada

Ipo, lakini njia moja ya kutegemewa  ya kupata na kushikilia utajiri kihalali, na hiyo ni kwa kutoa huduma zenye thamani. Hakuna mfumo uliowahi kuundwa ambao watu wanaweza kisheria kupata utajiri kupitia nguvu ya namba yao tu peke yake, au bila ya kutoa kama malipo thamani iliyokuwa sawa ya aina moja ama nyingine.

Kuna kanuni ijulikanayo kama Sheria ya uchumi, hii ni zaidi ya nadharia. Ni kanuni mtu yeyote hawezi kuipinga. Tia alama vizuri jina la kanuni hii na ikumbukwe kwasababu ina nguvu zaidi kushinda wanasiasa wote na mifumo ya kisiasa. Ipo juu na zaidi ya udhibiti wa vyama vya wafanyakazi. Haiwezi ikayumbishwa au kuhongwa na wapigadili au viongozi waliojichagua wenyewe katika tasnia yeyote.

Zaidi ina vyote, jicho la kuona na mfumo kamili wa hesabu za biashara ambao unatunza hesabu sahihi za miamala ya binadamu wote wanaojihusisha katika biashara ya kujaribu kupata pasipo kutoa. Muda wowote wakaguzi wake huja kuangalia kumbukumbu za watu zote kubwana ndogo na kudai hesabu.

‘Biashara kubwa’, ‘ulanguzi’ au jina lolote lile unalochagua kuupa mfumo uliotupatia uhuru, unawakilisha kundi la watu wanaofahamu, kuheshimu na kujifungamanisha wenyewe na hii sheria ya uchumi yenye nguvu. Uendelevu wao wa kiuchumi hutegemea kuheshimu kwao hii sheria.

Kumbuka pia kwamba hii ndiyo, lakini mwanzo wa vyanzo vilivyokuwepo kwa ajili ya ulimbikizaji wa utajiri. Ni kiasi kidogo tu cha vitu vya anasa na vitu visivyokuwa muhimu vilivyotajwa. Lakini kumbuka kwamba biashara ya kuzalisha, kusafirisha na kutafuta soko la hizi bidhaa chache hutoa ajira ya kawaida kwa mamilioni ya wanaume na wanawake wanaolipwa kwa huduma zao milioni nyingi za dolla kwa mwezi na kuzitumia kwa uhuru katika vitu vyote, vya anasa  na mahitaji muhimu ya lazima.

Sanasana kumbuka kwamba nyuma ya ubadilishanaji wote huu wa bidhaa  na huduma binafsi unaweza kupatikana wingi wa fursa za kujikusanyia utajiri. Hapa uhuru wetu unatusaidia. Hakuna kitu chochote kitakachokuzuia wala mtu yeyote kushiriki katika nafasi yeyote ya juhudi zinazohitajika kufanya hizi biashara. Ikiwa mtu atakuwa na kipaji cha kipekee, mafunzo au uzoefu, mtu huyo anaweza kujilimbikizia utajiri kwa kisi kikubwa . Wale wasiokuwa na bahati wanaweza kujilimbikizia utajiri kiasi kidogo. Mtu yeyote anaweza kuendesha maisha kwa malipo ya kiasi kidogo sana cha nguvu kazi.

Kwa hiyo, hivyo ndivyo ilivyo!

Fursa zimetandaza bidhaa zake mbele yako. Songa mbele chagua kile unachotaka , tengeneza mpango wako, uweke mpango katika vitendo  na uufuatilie kwa uvumilivu. Jamii ya Kibepari itafanya yaliyobakia.

Unaweza ukategemea sana katika hili, - JAMII YA KIBEPARI INAMHAKIKISHIA KILA MTU FURSA YA KUTOA HUDUMA ZENYE THAMANI NA KUKUSANYA UTAJIRI KULINGANA NA THAMANI YA HUDUMA HIYO.

Mfumo huo haumnyimi mtu haki hiyo, lakini hautoi ahadi wala hauwezi kuahidi kitu fulani bure. Sheria ya uchumi yenyewe isiyobadilika hudhibiti mfumo huu, kwamba hautambui wala kuvumilia kwa muda mrefu kupata pasipo kutoa. Sheria ya uchumi ilipitishwa na ASILI! Hakuna mahakama ambayo wavunjaji wa sheria hii wanaweza kukata rufaa. Sheria hutoa vyote viwili, penati kwa uvunjifu wake na malipo stahiki kwa utekelezaji wake bila kuingiliwa au uwezekano wa kuingiliwa na binadamu yeyote.

Sheria hii haiwezi kubadilishwa. Haibadiliki, ipo palepale kama nyota katika mbingu na huwajibika kwa, na ni sehemu ya mfumo unaoziongoza nyota.

Mtu anaweza kukataa mwenyewe kutii sheria ya uchumi?

Bila shaka! Hii ni jamii huru ambapo wote huzaliwa na haki sawa, ikiwemo haki ya kutokutii sheria ya uchumi.

Halafu ni kitu gani hufuata?

Vizuri, hakitatokea kitu mpaka idadi kubwa ya watu wameunganisha nguvu kutamka wazi lengo la kuipuuza sheria hii na  kuchukua kile wakitakacho kwa nguvu. Kisha huja dikteta, akiwa na vikosi vilivyojipanga vizuri na bunduki za rashasha!.

Hatujafikia bado hatua hiyo, lakini tumejifunza vyote tunavyotaka kujua kuhusu jinsi mfumo huu unavyofanya kazi. Labda tutakuwa na bahati ya kutosha kutokutaka uzoefu binafsi wa ukweli unaotisha. Bila shaka tutachagua kuendelea na uhuru wetu wa kusema, uhuru wa vitendo, na uhuru wa kutoa huduma zenye thamani kwa malipo ya utajiri.


Matokeo haya hayapatikani katika uzoefu wa muda mfupi. Ni matokeo ya miaka 25 ya uchanganuzi makini wa njia za watu waliofanikiwa zaidi na watu wasiofanikiwa zaidi Marekani iliopata kuwajua.


UKIPENDA KUSOMA SURA NA SEHEMU ZOTE ZA KITABU HIKI

............................................................................................................................


Mpenzi msomaji unayefuatilia tafsiri hii, na huo ndio mwisho wa Sura ya saba ya kitabu hiki, tafadhali nakusihi usikose mwanzo wa sura mpya ya 8 siku ya Jumatatu.

Pia zile semina zetu kwa mwaka huu za miradi yenye ubunifu itakayoboresha mizunguko yetu ya fedha, bado hazijaanza na pindi zitakapoanza tutakujulisha, kama hukutuma namba yako ya Whatsapp tuma kwa namba 0765553030, muda umebaki mchache sana.

Kupata vitabu bora kabisa vya biashara na ujasiriamali tembelea, SMART BOOKS TANZANIA.

0 Response to "FURSA ZIPO, CHAGUA UTAKACHO,TENGENEZA MPANGO, TEKELEZA NA KUFUATILIA KWA UVUMILIVU UTAFANIKIWA"

Post a Comment