ALIKUJA DAR KAMA HOUSE BOY SASA NI TAJIRI | JIFUNZE UJASIRIAMALI

ALIKUJA DAR KAMA HOUSE BOY SASA NI TAJIRI

  • Anamiliki gari, nyumba, ni mfano wa kuigwa

 Sindamka akiwa kazini. Picha na Elias Msuya 

Tatizo la ajira kwa vijana limekuwa sugu hasa kwa nchi zinazoendelea kama Tanzania. Vijana wengi wamekuwa wakikimbia vijijini na kuingia mijini kila mwaka wakitafuta ajira.
Wilfred Sindamka mwenyeji wa wilayani Kibondo Mkoa wa Kigoma, alihamia jijini Dar es Salaam mwaka 1995 akitokea mkoani Dodoma ili kujaribu kutimiza ndoto yake ya maisha. Endelea….
“Nilimaliza darasa la saba mwaka 1993 wilayani Urambo Mkoa wa Tabora ambako ndiko wazazi wangu wanaishi. Ila sikuchaguliwa kuendelea sekondari, hivyo nilifanya shughuli ndogondogo za biashara na kilimo.
“Biashara hizo zilinifikisha mkoani Dodoma mwaka 1994 ambapo nilifanya kazi ya kuuza maandazi, karanga na vinginevyo kwa kuajiriwa na mtu,” anasema Sindamka.
Anasema lengo la kuja Dar es Salaam lilikuwa ni kutafuta kazi na alipata msaada wa mwajiri wake aliyemwelekeza kwa ndugu yake anayeishi Magomeni Makuti jijini.
“Nilifika Dar es Salaam mwaka 1995 kwa mzee mmoja anayeitwa Midasi aliyekuwa akifanya kazi Wizara ya Mambo ya Ndani. Kazi aliyonipatia ni kuwa ‘house boy’. Nilifanya kazi hiyo kwa zaidi ya mwaka mmoja Niliridhishwa na kazi kwa kuwa nilikuwa nakula, kunywa kuoga kama niko nyumbani, lakini sikuwahi kulipwa mshahara kama nilivyoahidiwa,” anasema na kuongeza:
“Hali ile haikunifurahisha, hivyo nilimuuliza mzee Midasi naye akaniambia nimweleze mkewe. Hata baada ya kumweleza, mama alinipiga chenga tu. Kwa hiyo nikaazimia kurudi nyumbani wilayani Urambo.”
Anasema baada ya yule mama kumpa nauli alirejea kwao Urambo lakini mambo yakazidi kumwendea kombo, hadi alipoamua kurejea Dar es Salaam mwaka 1998. 
“Mama alinisikiliza, akauza mbegu zake za karanga kisha akanipa nauli. Hata hivyo safari hii sikutaka kurudia kwa mwajiri wangu wa kwanza ingawa pia sikujua nifikie wapi,” anasema.
Hata hivyo, anasema aliamua kwenda kwa rafiki yake anayeitwa Masanja ambaye walikutana siku za nyuma.
“Tuliwahi kufika hadi Wizara ya Elimu ambapo nilikutana na ndugu niliyemfahamu ambaye aliniambia kuwa maeneo ya Mburahati kuna ndugu zetu nikawatafute na nilipofika niliwapata nikaishi kwao,” anasema.
Juhudi za kutafuta kazi
Sindamka anasema aliamua kumtafuta rafiki yake Massanja aliyekuwa fundi ujenzi maeneo ya Kigamboni. 
“Kuna kazi tulikuwa tukiifanya pale katika kampuni inayoitwa Lemas mtaa wa Samora. Niliendelea na kazi ya ujenzi kwa zaidi ya mwaka mmoja.
Hata hivyo, anasema kuna wakati aliachana na kampuni hiyo na kujiunga na mafundi wengine kwenye kazi za ujenzi.
“Kuna siku nilikuwa nimebeba tofali sita kichwani napandisha juu ya ukuta maeneo ya Tabata, mara ngazi ikavunjika nikanguka chini na kuumia vibaya.”
“Nikaona kazi imekuwa ngumu na maisha yanazidi kuwa magumu. Ilifika mahali nilitamani tena kurudi Urambo ili nikalime, lakini nikajiuliza, mbona wenzangu wanaweza kazi na maisha yanakwenda?”
Baada ya hapo anasema alishauriwa na ndugu yake kufanya kazi kwenye kiwanda cha chuma ambako alilipwa mshahara wa Sh1,200 kwa siku, tofauti na kwenye ujenzi nilikolipwa Sh800 kwa siku.
“Niliifanya ile kazi lakini nikagundua kuwa ni ngumu kuliko hata ya ujenzi. Kulikuwa na moshi ambao ulinisababishia maumivu ya mwili. Kazi zenyewe hazikuwa na vifaa vya usalama, hivyo ilikuwa ni hatari tupu,” anasema.
Baada ya kuachana na hiyo kazi alipata rafiki mwingine aliyeitwa Hassan aliyekuwa na kazi ya kuchomelea vyuma na huo ndiyo ukawa mwanzo wa kujua kazi za vyuma.
“Licha ya ndugu zangu kunikataza kufanya kazi za kuchomelea, bado sikua na jinsi ila kurudi tena kwa Hassan ili nijifunze ile kazi,” anasimulia. 

Kuna wakati walipata kazi kule Mbezi Beach waliyopewa na aliyekuwa mhandisi katika kiwanda cha UFI na alimwambia awe analala kwenye nyumba wanayoijenga naye akakubali. Endelea kuisoma makala hiyo zaidi hapa katika tovuti ya MWANANCHI

0 Response to "ALIKUJA DAR KAMA HOUSE BOY SASA NI TAJIRI"

Post a Comment