VIJANA MPANDA WATAKIWA KUJIAJIRI | JIFUNZE UJASIRIAMALI

VIJANA MPANDA WATAKIWA KUJIAJIRI

NA Walter Mguluchuma, Katavi
Hifadhi ya Katavi, picha na tovuti ya tazamaramanitanzania.com

MKUU wa Wilaya ya  Mpanda, Paza  Mwamlima, amewataka vijana wilayani  Mpanda kujiajiri kuliko  kupoteza muda  kushinda vijiweni.
Mwamlima alitoa kauli hiyo jana alipofungua mkutano wa umoja wa wazee wa mji wa Mpanda uliofanyika ukumbi wa Super City ulioko mjini hapa.
Alisema serikali katika bajeti ya mwaka huu ilitenga sh bilioni moja kwa ajili ya mikopo ya vijana, lakini cha kushangaza badala ya vijana kuunda vikundi ili wanufaike na mikopo, kila kijana anataka kununua pikipiki.
Alisema ni vizuri wazee wakawashauri vijana wao wakafanya shughuli za miradi  za muda mrefu ambazo zinaendana na wakati na  zitakazoleta faida na tija kwa jamii.
Aidha aliwataka wazee wa Mpanda  kutoutumia umoja wao huo kwa misingi ya ukabila wala dini, kwani wakiendesha umoja huo kwa misingi hiyo  watafanya  kukosa upendo  miongoni mwao.
Alisema watu wanaamini wazee ndiye kimbilio la vijana,  hivyo hawapaswi kuwa na mfarakano wa aina yoyote.
Pamoja na hayo, umoja huo umeeleza changamoto wanazokabiliana nazo kuwa ni matatizo ya uongozi, katiba na matatizo ya fedha.
Mmoja wa wazee hao, Kassim Mfaume, alieleza katiba yao ina kasoro mbalimbai  ambapo endapo hazitarekebishwa zinaweza kuleta athari baadaye.
HABARI NA:  Tanzania Daima.


0 Response to "VIJANA MPANDA WATAKIWA KUJIAJIRI"

Post a Comment