WATEJA WANAHITAJI SABABU YA KUNUNUA BIDHAA/HUDUMA ZAKO. | JIFUNZE UJASIRIAMALI

WATEJA WANAHITAJI SABABU YA KUNUNUA BIDHAA/HUDUMA ZAKO.


Unapoanzisha biashara au hata kama biashara yako ni ya siku nyingi, inakubidi ufikirie ni kitu gani kitakachowafanya wateja wanunue bidhaa au huduma zako kuliko za washindani wako. Hii itakusaidia katika kampeni zako za kutafuta masoko.


Sababu ya wateja kununua biashara yako yaweza kuwa kitu chochote kwa mfano, ubora, wingi, bei nafuu, urahisi wa kutumia, upatikanaji, ufungashaji mzuri, kubebeka, au sababu nyingine yeyote ile. Hakikisha unaipa biashara yako sababu ya kipekee itakayowafanya wateja kuinunua kuliko kwenda kwa washindani wako.

0 Response to "WATEJA WANAHITAJI SABABU YA KUNUNUA BIDHAA/HUDUMA ZAKO."

Post a Comment