KUMBE SOKWE HUGAWANA VITU SAWA KAMA BINADAMU. | JIFUNZE UJASIRIAMALI

KUMBE SOKWE HUGAWANA VITU SAWA KAMA BINADAMU.

Tabia ya binadamu ya kugawana vitu imeanza zamani kuliko ilivyokuwa imefikiriwa hapo kabla. Imeanza tangu alipokuwa na umbile kama la sokwe. Katika utafiti uliofanyika  na kuchapishwa katika  jarida la Academy of Science kutaka kugundua ni kwa nini binadamu hugawana vitu, ilibainika kwamba kumbe tabia hiyo hata sokwe nao wanayo tena sawasawa kabisa na ilivyokuwa kwa binadamu.

Sokwe mmoja alipopewa  vidude mkononi  alimgawia mwenzake sawa sawa nay eye mwenyewe, hii inamaana kwamba hata wanapopewa ndizi hufanya hivyo. Utafiti huu ulibaini kuwa sokwe wana tabia ya kugawana hata chakula sawa kwa sawa  na ikitokea mmoja akampunja mwenzake huyo aliyepunjwa hugoma kabisa kupokea.

Wote binadamu na sokwe wanatabia zinazofanana katika kugawana vitu, huwinda pamoja, hugawana vyakula, husaidiana katika kulea watoto nk.
Chanzo BBC.


0 Response to "KUMBE SOKWE HUGAWANA VITU SAWA KAMA BINADAMU."

Post a Comment