MATAJIRI MATAPELI TANZANIA HADHARANI | JIFUNZE UJASIRIAMALI

MATAJIRI MATAPELI TANZANIA HADHARANI

"Papaa Msofe, Aurora waongoza jeshi"

Baada ya sifa ya Tanzania kuingia doa kutokana na watu wengi maarufu kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya , uchunguzi wa JAMHURI umebaini kuwa matajiri wengi nchini wanatuhumiwa kufanya utapeli wa kutupwa kwa Wazungu kupitia ahadi hewa za kuwauzia madini.

Taarifa nyeti zilizonaswa na JAMHURI zinaonyesha uchunguzi wa kina uliofanywa na serikali umebaini uwepo wa wafanyabiashara wenye leseni halali za udalali wa madini, lakini biashara wanayofanya ni kuwatapeli Wazungu kisha wanatembeza rushwa kwa baadhi ya Polisi na Mahakama  kukatish tama Wazungu waliotapeliwa.


“Ndugu zangu nawaambia  watu hawa hawana woga kabisa. Majina haya unayoyaona  Wizara imefikia uamuzi wa kuyapeleka kwa Mheshimiwa Rais(Jakaya Kikwete), pengine aingilie kati  na kuzilazimisha mahakama na hawa polisi kuhakikisha wahusika wanakamatwa...jina la Tanzania linanuka nje ya nchi sababu ya watu hawa “ kilisema chanzo chetu.

Baada ya kupata orodha ya majina haya , JAMHURI kwa nyakati tofauti liliwasiliana na matajiri wanaotuhumiwa mmoja baada ya mwingine kwa kutumia barua pepe na simu zao za mkononi, na mchezo ukawa ule ule jinsi wanavyowatapeli Wazungu.

Hawa wana utajiri mkubwa ajabu,. Wanaingia kwenye mtandao na kuwadanganya Wazungu kuwa wana madini hadi kilo 600, wanawatumia vivuli vya leseni zao halali walizozipata kutoka Wizara ya Nishati na Madini, kisha Wazungu wanaamini kuwa ni biashara halali, na wanapotuma fedha tu zinaondolewa kwenye akaunti mara moja.

Mtandao huu ni mpana kwani unahusisha baadhi ya watumishi wa benki za hapa Tanzania na nje ya nchi ikiwamo Marekani na Australia, ambako mabillioni ya fedha yanaingizwa kwenye akaunti kwa njia ya utapeli na kuondolewa haraka. Wahusika wanamiliki magari ya kifahari na wanajenga maghorofa.

Maeneo yaliyokithir katika utapeli wa madini ni Dar es salaam, Arusha  na Mwanza. Waraka ulioonwa na Jamhuri unaokwenda kwa Rais unaonyesha kuwa vitendo vinavyoendelea sasa hivi vya utapeli katika biashara ya madini vinaichafua sifa ya Tanzania na kuikosesha serikali mapato yanayotokana na biashara ya madini.


Ukitaka kuisoma habari hii nzima pamoja na majina ya Matajiri wanaotuhumiwa  utaipata katika Gazeti la JAMHURI toleo la leo Septemba 3.

0 Response to "MATAJIRI MATAPELI TANZANIA HADHARANI"

Post a Comment