BAJAJI ILIYOUNDWA KAMA POPO ! | JIFUNZE UJASIRIAMALI

BAJAJI ILIYOUNDWA KAMA POPO !

Kwenye baiskeli haipo, wala pikipiki wala gari.

"Bajaji popo"

Mark Stewart akikatiza mitaa huku akiwa amepanda baiskeli-pikipiki yake inayotumia mwanga wa jua anawaacha watu wakizigeuza shingo zao kumtazama.Kila pedali anayopiga, miguu inazunguka kuanzia chini wakati muungurumo wa mota ya umeme-jua ukisikika kwa mbali.

Kile anachoendesha kinaonekana kama chotara ya baiskeli na gari, kikiwa na paneli za jua pekee pamoja na umbo la kisasa. “Ni kijani, chaguo la abiria wa kisasa”. Stewart mwenye umri wa miaka 65 , mtaalamu wa tiba za mionzi na mwanasaikolojia kutoka Camridge aliamua kwenda likizo yake ya majira ya joto kwa usafiri wa baiskeli yake mpya ya ELF badala ya usafiri wa kawaida wa treni na mabasi.

Safari yake nzima kutoka Durhan mpaka Reston ilimchukua siku  5, na maili zipatazo 60. Baiskeli hizi za EFL hufikisha mpaka maili 30 kwa saa (30mph) kwa kutumia pedali pamoja na mota ya umemejua. Na maili 20 kwa saa kwa kutumia umemejua peke yake.

Kwa hakika njiani anakumbana na maswali mengi, lakini Stewart anasema hizo ni changamoto za za kawaida “Sijali namaana kuwa huwa nafurahi watu wanapoizungumzia. Baiskeli-pikipiki hii, inao uwezo wa kusafiri maili 1800 sawa na galoni moja ya petrol, haihitaji bima wala gharama za matengenezo ukilinganisha na gari la kawaida. Na zaidi gharama za matairi pia ni kidogo pia.
‘Teknolojia ya utengenezaji wa hizi baiskeli ilichotwa kutoka teknolojia ya utengenezaji wa ndege,maboti na baiskeli za kawaida’ anasema afisa mtendaji mkuu wa kampuni ya Organic Transit inayozitengeneza.

Mchanganyiko wamajanga ya kimazingira , bei kubwa ya mafuta, mabadiliko ya hali ya hewa na uhamiajiwa watu mijini, vyote huchangia muelekeo wa watu kuhitaji usafiri mbadala, lakini siyo kila mtu atapenda baiskeli ya kawaida ya pedali. Cotter alisema baiskeli-pikipiki hizi  zimetengenezwa  mahsusi kukabiliana na majanga yaliyotajwa.
Lakini wakati EFL zinawekwa katika kundi la baiskeli na kampuni ya Organic Transit, sheria mbalimbali zinasema hii siyo baiskeli bali gari na haitaruhusiwa kupita katika barabara za baiskeli za kawaida.

Kiwanda kinakuwa, kwa siku hutengeneza wastani wa baiskeli 1. Kwa sasa wameshazalisha  baiskeli 75 na wana oda zaidi ya 200 ambazo tayari wmeshachukua advansi. Matarajio ni kutengeneza  baiskeli 4 kwa siku. 

CHANZO : Associated Press, MWANDISHI, Shaquille Brewster  

0 Response to "BAJAJI ILIYOUNDWA KAMA POPO !"

Post a Comment