BIASHARA 5 ZA MTAJI KIDOGO KUANZIA ELFU 2, KUMI MPAKA LAKI MOJA UNAZOWEZA KUANZA ZIKAKUTOA | JIFUNZE UJASIRIAMALI

BIASHARA 5 ZA MTAJI KIDOGO KUANZIA ELFU 2, KUMI MPAKA LAKI MOJA UNAZOWEZA KUANZA ZIKAKUTOA

Mtaji ni changamoto kubwa sana kwa wajasiriamali wengi wadogo, utakuta mjasiriamali anayo mawazo mengi makubwa lakini anaishia kuzeeka nayo shauri ya kukosa mtaji wa kutosha kuweza kuyageuza kuwa biashara halisi. 

Ni wajasiriamali wachache ambao huwa na bahati ya kupigana kiume, wazungu hupenda kuita, bootstrapping, mpaka wanapata mitaji mikubwa, kwa kudunduliza faida kidogokidogo inayotokana na biashara ndogo wanazozifanya.

Kutumia rasilimali chache zilizomo ndiyo chaguo la mwisho kwa mjasiriamali anayefanya biashara kwa kutumia  mtaji kidogo huku akiwa hana dhamana za uhakika au sifa za kutosha kukopesheka na taasisi za fedha, mabenki nk.

Hata ikiwa mjasiriamali atakuwa na sifa za kukopa bado wengi hawana elimu sahihi ya mikopo jambo linalosababisha waogope kwenda kukopa kwa kuhofia kuja kufilisiwa mali zao kidogo walizokuwa nazo.

SOMA : Biashara ndogondogo 7 unazoweza kuanza bila mtaji

Una mawazo makubwa na mazuri ya biashara, lakini huna mtaji, umejaribu njia zote za kupata mtaji wa kutosha kama vile kukopa, kuingia ubia na mtu, kuuza mali zako ulizokuwa nazo, kupata mfadhili, lakini imeshindika, umekutana na vikwazo vingi. Njia pekee unayoweza kuitumia ili kuweza kujenga hali yako kifedha na hatimaye angalao uweze kuaminika ni kwa njia ya kuanza chini kabisa, na katika kuanza huko chini kabisa itakubidi utafute njia za kukuingizia kipato zilizokuwa rahisi na ambazo hazita kugharimu mtaji au fedha nyingi.

Unaweza ukaamua kutumia njia moja maarufu na ambayo ndiyo iliyozoeleka na watu wengi zaidi ya kutafuta ajira au kibarua na baadaye sasa utakapokuwa umelipwa mshahara ukaanza kuangalia ni kwa namna gani unaweza ukaanza taratibu kuwekeza katika biashara ndogondogo.

Njia ya pili unaweza ukatafuta kwa njia yeyote halali na utakayoona inafaa mtaji mdogo kabisa hata  kuanzia shilingi elfu tano au mbili na kuanza biashara ndogo sana ambayo ndiyo hasa ninayotaka kuzungumzia katika makala yangu hii ya leo. Lengo langu ni kutaka kukupa moyo wewe mjasiriamali uliyekata tamaa na kufikiri kwamba hakuna tena njia ya kutokea baada ya kuona kwamba karibu kila njia unayojaribu kupata mtaji wa kuanzisha biashara ya ndoto yako imefungwa.

Mtaji ni kati ya vitu vigumu mno duniani kupatikana ikiwa hautakuwa mvumilivu na kukubali kufanya kazi kwa juhudi na maarifa huku ukianzia chini kabisa. Haijalishi wewe una umri gani wewe anza chini kisha jifanye ndio kwanza unaanza kushika hela kwa mara ya kwanza, hapa namaanisha tumia pesa unazopata kwa uangalifu mkubwa ukitoa pesa kwa ajili ya vitu muhimu tu, achana na matumizi yasiyoingiza faida. Ni bora ukatembea na kiatu kilichotoboka ukachekwa lakini ukijua unatengeneza mtaji kwanza. Watakaokucheka iko siku watakusalimia kwa heshima.

SOMA: Kuendesha biashara bila mtaji ni sawa na kulima kwa jembe lisilokuwa na mpini.

Ngoja tusiende sana nje ya mada ya leo, sasa nitakutajia zile biashara 5 ambazo, kwa mtaji mdogo kabisa hata shilingi elfu mbili 2, tano, elfu 10 mpaka laki moja(100,000) unaweza ukaanzisha na kwa kutumia rasilimali kidogo kabisa ulizokuwa nazo mchanganyiko na kubana matumizi kwa hali ya juu kabisa (bootstrapping) basi unajikuta polepole unaanza kupata mtaji, biashara inakua, unafungua biashara kubwa kidogo, na sasa wakopeshaji au wabia wakaanza kupigana vikumbo wakikugombea wakukopeshe au kuingia ubia na wewe.

Biashara hizo ni kama vile hizi zifuatazo;

1.Biashara ndogondogo za vitu vya kutafuna kama vile karanga, ubuyu, pipi na ice cream.

Biashara hizi unaweza ukazichukulia rahisi rahisi na kusema, “nitazipanga wapi sina hata kibanda cha genge wala ninapoishi hamna watu wengi”. Usikubali kushindwa kabla hujaanza, hakuna mahali watu wasipopita, wewe unaishi wapi? Unatembea wapi? Hamna mtu hata mmoja?. Huna majirani?

Kila mahali watu hawakosekani, walewale unaokutana nao kila siku wanaweza kuwa wateja wako ilimradi tu wafahamu unacho kitu wanachohitaji. Fikiria ni kitu gani watakachokuwa na mahitaji nacho na uhakikishe kila siku hakikosekani katika yale mazingira wanayoishi au kufanya kazi.

Kuwa mbunifu siyo lazima uwe na duka ndipo uuze bidhaa. Baraza ya nyumba unamoishi au hata ulipopanga panatosha kuweka stuli na ukapanga biashara yako watu wakanunua kama kawaida.

Kwanini nasema mtaji hata wa shilingi elfu mbili (2,000) mtu unaweza ukaanza biashara? Tuchukulie kwa mfano karanga, ukinunua kilo moja unaweza ukazikaanga na kuanza kuuza kwa kutembeza na bakuli au ukazifunga vizuri katika paketi za nailoni.

2. Biashara unazoweza kufanyia nyumbani kama vile kuuza mkaa, mafuta ya taa, kuni na pumba za kulishia mifugo.

Mahitaji niliyoyataja hapo juu yote ni nishati ya kupikia chakula kasoro tu pumba za mifugo kwa sababu hakuna ubishi wowote ule watu wengi Tanzania ni watu wa vipato vya wastani na vipato vya chini, na nishati hizi zote ndizo wanazozitumia kila siku. Hata uwe unaishi wapi vitu hivi vitanunuliwa tu na amini ninachokuambia haviwezi kukaa muda mrefu bila kwisha.

Hali kadhalika pumba nimeitaja makusudi kwani nafahamu watu wengi hufuga kuku, bata na baadhi ya wanyama na ndege wengine wafugwao lakini uwezo wa kununua vyakula maalumu(special food) kwa wanyamana ndege hao ni mdogo, hukimbilia pumba kutokana na urahisi, hivyo piga ua ni lazima uuze.

Uzuri wa vitu vyote hivyo nilivyovitaja hapo juu, unaweza ukavifunga(ukavipack) katika mifuko, chupa kwa upande wa mafuta ya taa ukafahamu kabisa faida yake ni shilingi ngapi kabla hata hujaanza kuviuza.

3. Kuuza matunda na mboga mboga.
Unaweza ukatumia staili ya kutembeza barabarani au ukaweka meza mbele ya mahali unapoishi ukavipanga vizuri pale. Unaweza pia ukatumia kakabati kadogo ka vioo ukaweka matunda safi yaliyomenywa kabisa kwa ajili ya wateja wanaopita njia. Mtaji wake ni kidogo na vinatoka harakaharaka.

SOMA: Njia 7 za kupata mtaji wa biashara.

4. Uuzaji wa samaki na dagaa mchele.
Kila siku watu hutafuta vitoweo, watu wa hali za chini hupenda sana dagaa wabichi waliokaangwa maarufu kama dagaa mchele kwa Dar es salaam. Na hata mikoa mingine nako kuna dagaa wa aina nyinginezo nao watu pia hupenda kununua kwa ajili ya kitoweo.

Wanaomudu kununua samaki nao hununua kila mara, unapomuuzia mtu leo akikuta samaki wako ni wazuri, haitapita wiki, ni lazima akutafuta tena kwa ajili ya samaki wengine. Mtaji wake siyo mkubwa na unaweza kuchagua kuwauzia mazingira ya nyumbani au ukawatembeza majumbani mwa watu kila siku.

5. Biashara za utoaji wa huduma mbalimbali zisizohitaji mtaji mkubwa kama vile udobi, ubebaji wa maji kwa ndoo na madumu na utengenezaji wa bustani za maua(gardening)

Biashara hizi kama kufua na kunyosha nguo “udobi”, mtaji wako ni maji na kipande cha sabuni tu, eneo laweza kuwa ni nyumbani kwako au nyumbani kwa mteja. Kuwabebea watu maji kwa madumu au kwa ndoo utahitaji kuwa na mtaji wa kununulia mkokoteni kiasi kisichozidi shilingi laki moja pamoja na madumu yenyewe, mtaji wa kununulia maji bombani unaweza hata kuteka kwa mkopo ukaja kulipa baada yaw ewe kulipwa.

SOMA: Biashara zinazolipa zaidi duniani.

Kwa ufupi tu nimejaribu kuonyesha biashara ambazo mtaji wake ni mdogo kuanzia shilingi elfu mbili 2 mpaka shilingi laki moja ambazo mtu yeyote anayetaka kuingia kwenye ujasiriamali anaweza akaanza, biashara nilizozitaja hapa zinawakilisha biashara kama hizo nyingi, hivyo siyo lazima mtu anayetaka kuanza chini kabisa basi aanze na zile nilizotaja bali anaweza kuanza hata na biashara nyingine yeyote lakini yenye sifa hiyo ya kuhitaji mtaji mdogo.

……………………………………………………………………….

Ndugu msomaji wa blogu hii, kama kama makala unazosoma humu zinakuvutia, basi ujue na vitabu kutoka self help books Tanzania vitakuvutia na kukunufaisha mara dufu. Vitabu vitatu 3 hapo chini kutoka kwetu hakuna mtu aliyewahi kununua hata mmoja akajutia pesa yake aliyotoa.


1. SHILINGI 20,000/=




2. SHILINGI 10,000/=



3. SHILINGI 5,000/=


1.  Dar es salaam ukihitaji kimoja, viwili au hata vyote 3, Unaweza kuja moja kwa moja ilipo ofisi yetu, Mbezi kwa Msuguri stendi, ukifika tazama kibao cha hospitali ya Bochi kilipo mkono wako wa kulia pana njia, au ni mkabala opp. na yanakosimama Malori makubwa yaendayo mikoani, vuka barabara pana hardware nje.

2.  Ukitaka uletewe ulipo kwa Dar es salaam wasiliana na sisi upate utaratibu. 0712202244 au 0765553030

3.  Wateja wa Mikoani, tunatuma kwa njia ya mabasi na gharama ya kutuma kifurushi ni shilingi elfu 10, hivyo kama utapenda tukutumie kitabu/vitabu tuma fedha kwa ajili ya kitabu/vitabu pamoja na sh. 10,000/= ya usafirishaji wa basi linalofika ulipo.

4.  Kama utapenda kutumiwa vitabu kwa njia ya email(softcopy) popote pale ulipo, bei za vitabu hupungua, cha kwanza ni elfu 10, cha pili elfu 5 na cha tatu elfu 3. Tuma pesa na anuani yako ya email tutakutumia kitabu /vitabu muda huohuo. Namba zetu ni 0765553030 au 0712202244, watsapp: 0765553030


MICHANGANUO YA BIASHARA / BUSINESS PLANS

Unahitaji kuandikiwa mpango wa biashara yako kwa gharama nafuu?

AU

Unahitaji mafunzo kwa ajili ya kuandika mwenyewe mpango wa biashara yako kwa njia rahisi?

Basi wasiliana na sisi bei zetu ni rafiki mno

Simu/whatsapp: 0765553030
Simu/sms:          0712202244



3 Responses to "BIASHARA 5 ZA MTAJI KIDOGO KUANZIA ELFU 2, KUMI MPAKA LAKI MOJA UNAZOWEZA KUANZA ZIKAKUTOA"