KUSOMA VITABU HIVI VYA MAENDELEO BINAFSI MTANDAONI SASA NI RAHISI MNO! | JIFUNZE UJASIRIAMALI

KUSOMA VITABU HIVI VYA MAENDELEO BINAFSI MTANDAONI SASA NI RAHISI MNO!














Vitabu vyako vya Self Help Books Limited vimerahisishwa ili kuweza kuwapa fursa watu wengi zaidi kuweza kuvisoma bila kikwazo chochote. Kitabu hasa cha "Michanganuo ya Biashara na Ujasiriamali" ambacho ilikuwa ni vigumu kumtumia mtu katika e-mail kutokana na ukubwa wa faili lake sasa wataalamu wetu wameweza kupunguza ukubwa wa faili la kielectronic(compression) mpaka likawa katika ukubwa unaokubalika.

Shughuli hiyo haijaathiri kwa namna yeyote ile ubora wa kitabu chenyewe zaidi ya kukifanya kiwe ‘free’ zaidi unapokuwa ukishusha ukurasa au kupandisha. Kadhalika pia kwenye email inachukua sekunde chache zaidi kukidownloa(kupakua)

Vitabu vingine pia “Mifereji ya Pesa” na “Siri ya biashara ya Rejareja”, navyo vimeboreshwa zaidi kuvifanya visomeke vyema zaidi katika screen za simu za kisasa za Smartphone au Tablets.
Ndugu msomaji, ujuzi wa maswala ya biashara haupitwi na wakati hata siku moa, hivyo nakutia moyo kama bado hukuwa umesoma vitabu hivi vizuri, basi jitahidi kufanya hivyo kwani vimejaa mambo mengi  yatakayokusaidia katika mapambano yako dhidi ya umasikini na uboreshaji wa maisha kwa ujumla. 

Siwezi kuchoka kuhubiri kitu hiki; 
“jifunze kupanga kwa weledi  kila jambo unalolifanya  na hasahasa biashara hata ikiwa kupanga huko utafanya kwa kichwa tu pasipo kuandika katika karatasi, kwani kupanga ndiyo msingi wa karibu kila jambo mwanadamu analolifanya hapa duniani.”

Nadhani Kabla ya kufanya jambo lolote huwa unafikiria kwanza akilini, sasa kuwaza huko ndiko kupanga kwenyewe na unatakiwa ujifunze  namna bora zaidi ya kupanga biashara yako iwe mpya au ulishaianzisha kitambo ikiwa utataka mabadiliko ya kweli na ya haraka.

Achana na kudanganywa eti, “Mipango siyo matumizi”, hiyo ni misemo ya jadi inayozidi kukufanya uamini kupanga hakuna maana wakati kila siku unapanga. Unakuwa hauna tofauti na Ngamia anapojichimbia kichwa mchangani akidhani kakwepa hatari kumbe kiwiliwili kingali bado nje na muda wowote anaweza kutokea adui akamchoma mkuki.

Msomaji wangu ukihitaji kitabu chochote hapo, wasiliana na mimi, unitumie E-mail yako na kiasi cha fedha husika, nami nitakutumia kitabu chako mara moja pasipo kuchelewa popote pale ulipo ndani na nje ya Tanzania. Namba zangu za simu ni 0712 202244 au 0765 553030 Jina ni Peter Augustino Tarimo. 

Ukitaka "Package" nzima yaani kifurushi cha vitabu vyote 3 ni shilingi elfu 18 tu, unapata maarifa ambayo kwingineko unaweza kulipa mpaka elfu 70, linganisha thamani na ubora. Asante sana kwa kusoma.

Napenda pia kukujulisha kuhusu DARASA LA MICHANGANUO YA BIASHARA linaloendelea sasa katika blogu maalumu iliyoanzishwa iitwayo "Michanganuo ya biashara" Kwa taarifa zaidi na jinsi ya kujiunga na darasa hili bonyeza maandishi yafuatayo, Shule ya Michanganuo ya biashara Mtandaoni(TOSBP)

0 Response to "KUSOMA VITABU HIVI VYA MAENDELEO BINAFSI MTANDAONI SASA NI RAHISI MNO!"

Post a Comment